Nikiangalia uso wa Tundu Lissu namsoma namna hii...

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195
Ni pekee ninayemwona ana udhati wa moyoni wa upendo wa nchi yake. Ameshaongea mengi ambayo ni makubwa na yanaweza hata kumgharimu kwa vyovyote vile lakini ameyasema. Ni mtendaji wa uhakika, hana hata chembe ya kashfa yeyote, ana uwezo mkubwa kiakili na hawezi kukosa kazi nzuri zaidi ya hii ya siasa anayoifanya akaishi maisha yake mazuri mno.

Kwao anakubalika ni mtu wa watu na hajibagui nao anapokuwa kule, nina uhakika na hili kwa kuwa ni mtani wangu ambaye ni rafiki yangu ndugu yake amenieleza hili. Tundu Lisu, nimewahi kuongea naye tukiwa kwenye mkutano wa wanasheria Arusha, ukweli he is a son of peasant and of the people.

Hata ndugu yake Alute naye sio mtu wa kudharaulika, ana hekima sana na ndiyo maana yeye na mdogo wake pamoja na kuwa vyama tofauti bado wapo pamoja na wanacheza siasa nzuri. Nakumbuka katika mkutano wa hivi karibuni kule Arusha Alute akichangia kujadili presentation ya Lisu alimwuliza inakuwaje sisi Tanzania tunataka Katiba yetu ipunguze nguvu ya Raisi katika maamuzi wakati Katiba za wenzetu kama Marekani wameimarisha nguvu za Raisi katika Katiba (Have you contemplated the effects of having a weak president in decision making?). Tulipotoka nje ya mkutano nilimchombeza Lisu kuhusu hoja ya kaka yake ambayo hakupata nafasi ya kuijibu mkutanoni na akaniambia ama kaka yake hakumwelewa vizuri kuhusu hilo ama yeye hakuelewesha vizuri.

Wana JF kikubwa ninachotaka kusema, ukweli unabaki pale pale kwamba kwangu mimi Tundu Lisu ndiye mwanasiasa ninayeamini ana utashi wa dhati na ni msafi hadi moyoni mwake. Kama huwa anapitia JF basi atambue kuwa kuna mtu angalau anamtazama katika taswira ya namna hii na ajiimarishe katika hili bila kujalisha anaweza kuja kuwa Raisi wetu ama la! Thawabu zake kwa Mungu zipo.
 

Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
0
Mkuu hilo ni kweli kabisa halina ubishi mungu ampe maisha marefu, anapoongea Tundu Lisu hasa katika mabo yenye mshiko katika mustakabari wa taifa roho huwa inasuuzika kabisa huwa nashangaa Spika anavyojitutumua kumkatisha hata sipati picha ni kwanini inatokea hivo
 

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,254
1,195
Mpambanaji na mpiganaji wa kweli, kwa historia tu, huwa halipwa na wanadamu, bali Mungu ndiye mlipaji! Basi tumuimbee mpambanaji Mh. Tundu Lissu aendelee na moyo huo huo na Mungu ampe ujasiri zaidi, Amen!
 

kinai

Senior Member
Oct 13, 2012
159
0
Namkubali sana Tundu Lisu. Ni bingwa wa kujenga hoja, jasiri na mwerevu. Hana papara katika kufikia malengo yake. Kikwete aliwahi kusema mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu ni heri dr slaa awe rais lakini sio Lisu aingie bungeni. Moto wa Lisu bungeni tumeuona. Ukiwa na Lisu upande wako ni kama timu ya mpira wa miguu yenye wachezaji 10 na ikashinda timu pinzani yenye wachezi 11. Angalia anavyomtesa spika makinda, mwanasheria mkuu wa serikali Werema na Wenyeviti wa bunge- ni kama anawachezea nusu uwanja
 

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,261
0
Yuko makini sana, hii humsabishia kupewa sikio na kila mwenye huruma na nchi hii.
 

Tony Almeda

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
397
0
Siku zote alie nje ya kiwanja ndio anakosoa mchezaji, ngoja aingie yeye uwanjani utaona jinsi atakavyocheza, likipigwa raggae yeye atacheza blues.

Na huyo Lissu wenu ndio itakavyokuwa, mtasema afadhali ya Mrema......!
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,495
1,250
Alikosea tu kumpa dadayake kiti maalum kule bungeni. Vinginevyo ni mjengaji mzuri wa hoja na ni imara sana katika kuzisimamia.
 

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,683
1,225
super sub ya dk slaa bungeni, huwa nnaridhika na michango yake bungeni, nnampa nyota tano, big up mkuu tunakukubali saana
 

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,856
1,500
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Tundu Lisu ni mzalendo wa kweli. Tukipata watu kama 100 wa harakati kama yeye, hakika nchi hii tutaikomboa. Angalau wakulima tutapata hata kaniki ya kufunika miili yetu.
Hakuna barometer ya uzalendo.
 

socratess

Member
Apr 22, 2012
37
0
umeongea vizuri kaka,ila hapo kwenye mabo umeteleza kidogo nadhani ulitaka kuandika neno Mambo,naomba kuwasilisha
 

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,068
2,000
kama Dkt hagombei 2015 basi jembe tunalo!sipati picha LISSU akichukua nafasi ya currently Vasco Da Gama.Magamba makuu yote yatakimbilia uhamishoni kwasababu si mtu wa kumung'unya maneno na vitendo ndo mwake.
 
Top Bottom