Nikiachiwa kwenye ruling naweza kamatwa tena?

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,596
4,890
Wakuu habari za usiku ....nina kesi mahakama ya mkoa mwanza na kesi ipo hatua za mwisho baada ya polisi kusua sua na ushahidi toka 2010 mpaka leo na mara kadhaa hakimu anamwonya mwendesha mashtaka kuwa anachelewesha kesi ili tu aniachie kwa kifungu kidogo 225 ili tu wanikate tena kulingana na mwenendo wa kesi leo polisi wamefunga ushahidi kwa kulazimishwa na hakimu sasa swali langu naweza kukamatwa tena kama nitaachiwa kwenye ruling?....na ruling imepangwa mwezi ujao.....msaada tafadhali kwa wajuzi wa sheria...natanguliza shukrani.
 
Wakuu habari za usiku ....nina kesi mahakama ya mkoa mwanza na kesi ipo hatua za mwisho baada ya polisi kusua sua na ushahidi toka 2010 mpaka leo na mara kadhaa hakimu anamwonya mwendesha mashtaka kuwa anachelewesha kesi ili tu aniachie kwa kifungu kidogo 225 ili tu wanikate tena kulingana na mwenendo wa kesi leo polisi wamefunga ushahidi kwa kulazimishwa na hakimu sasa swali langu naweza kukamatwa tena kama nitaachiwa kwenye ruling nikafunguliwa kesi hiyo hiyo tena?....na ruling imepangwa mwezi ujao.....msaada tafadhali kwa wajuzi wa sheria...natanguliza shukrani.
 
Mita 50 ndo unakamatwa nje ya mita 50 hukamatwi hlf pale hakimu anapotaja hukum hyo tu nyoosha kidole uombe ulinzi wake mpk utakapotoka mahakamani yani ile hta hajamaliza ushanyoosha mkono na akikubali umgande hata akiingia chooni usimuache
 
Hivo ndio ninavojua sina experiance sana wajuzi watakuja kutoa maoni yao zaidi
 
Wakuu habari za usiku ....nina kesi mahakama ya mkoa mwanza na kesi ipo hatua za mwisho baada ya polisi kusua sua na ushahidi toka 2010 mpaka leo na mara kadhaa hakimu anamwonya mwendesha mashtaka kuwa anachelewesha kesi ili tu aniachie kwa kifungu kidogo 225 ili tu wanikate tena kulingana na mwenendo wa kesi leo polisi wamefunga ushahidi kwa kulazimishwa na hakimu sasa swali langu naweza kukamatwa tena kama nitaachiwa kwenye ruling?....na ruling imepangwa mwezi ujao.....msaada tafadhali kwa wajuzi wa sheria...natanguliza shukrani.
Kama walileta shahidi hata kama ni mmoja kwenye ruling ikionekana huna kesi ya kujibu utaachiwa kwenye kifungu na.230 cha CPA na hutaweza kukamatwa na kushitakiwa kwa makosa waliyokuwa wanekushitaki lakini kama utaachiwa kwenye kifngu na.225(5) kwa maana kwamba upande wa mashtaka wamechelesha ushahidi unaweza kukanatwa tena na ukashitakiwa kwa makosa yaleyAle
 
Hata hivyo kama wanefunga ushahidi na kama ushahidi wao utaonekana haukukufanya kuwa na kesi ya kujibu lazima utaachiwa kwenye kif na. 230 Kama nilivyoainisha Hapo juu
 
Kama walileta shahidi hata kama ni mmoja kwenye ruling ikionekana huna kesi ya kujibu utaachiwa kwenye kifungu na.230 cha CPA na hutaweza kukamatwa na kushitakiwa kwa makosa waliyokuwa wanekushitaki lakini kama utaachiwa kwenye kifngu na.225(5) kwa maana kwamba upande wa mashtaka wamechelesha ushahidi unaweza kukanatwa tena na ukashitakiwa kwa makosa yaleyAle

Sasa mkuu chomile hapo kwenye kifungu 225 chote sheria imezungumzia kuachiwa kabla ya Ruling.
Na mathalani, kwenye kifungu cha 225(5) sheria imezungumzia Nolle Prosequi ambapo ni lazima iwe pleaded by the prosecution before and during the proceedings and NOT after the ruling.

Kama mtuhumiwa katolewa baada ya rulling then section 225 haiwezi kufanya kazi yoyote.
Ila kama prosecution itakata rufaa basi huyo jamaa anaweza kuwekwa ndani tena.
Lakini ikiwa na mahakama ya Rufani basi ndiyo imetoka hakuna kesi tena hapo.
 
MTOTO WA KUKU ,
Kingine mkuu wangu anayeomba kifungu 225 cha CPA kifanye kazi na kesi ihairishwe ni Upande wa mwendesha mashitaka.
Sasa kama hakimu kalazimisha hao jamaa waingize ushahidi na umalizike na wao wakakubali basi imekula kwao.
Jambo la kuweka kichwani ni kwamba Muendesha mashitaka ndiye anyetakiwa kuomba Nolle Prosequi na mahakama haitakiwi kuuliza ni kwanini Upande wa mwendesha mashitaka unaomba.

Nolle Prosequi kwa kifupi ni ombi ambalo mwendesha mashitaka analilita kwenye mahakama hasa pale anapohisi kwamba kesi yake inakosa ushahidi wa kutosha. Hivyo kwa kipindi hicho ni lazima mtuhumiwa aachiwe lakini haimaanishi kesi imeisha: Ushahidi ukipatikana mtuhumiwa atashitakiwa tena kwa kesi hiyo hiyo.

Sasa kwenye kesi yako ni busara kama mwendesha mashitaka angeomba Nolle Prosequi mapema, hapa mahakama isingemkatalia. Kwa sasa hawezi kufanya kitu kama ruling ishapitishwa na mahakama.
Nolle Prosequi ni kabla ya kesi na wakati kesi inaendelea na siyo vinginevyo.

Hao State Attorneys wasikuletee figisu zisizo na msingi.
Hebu tafuta advocate wako mwenyewe kama vipi.
 
Kweli kabisa, ila mwendesha mashtaka anataka atumie hiyo nafasi kuomba kuondoA shauri chini ya kifungu hicho 225 ili akikamilisha ushahidi wamkamate tena jamaa
 
Mrejesho wana jamvi:-kama nilivyouliza hapo nyuma leo mahakama imeniachia kwenye ruling na hakuna mtu alienikamata nimewapita mapolisi kama hawanijui...asanteni wana jamvi wale wote waliochangia huu uzi mungu awabariki sana na heshima kwenu.
 
Hongera sana
 
Kama ni kesi ya jinai(criminal case) kwa kawaida kwa mujibu wa sheria ya Taratibu za Makosa ya jinai(Criminal procedure Act[cap 20 R.E.2002] mtuhumiwa anaweza kuachiwa katika hatua yoyote ya kesi ispokuwa HUKUMU.Mtuhumiwa anaweza kuachiwa pale tu ambapo mahakama haijaona kesi ya msingi(rule of case to answer-premafacie case) au pale ambapo muendesha mashtaka wa jamhuri(DPP) ameiamuru mahakama isiendelee kusikiliza kesi hiyo ispokuwa kesi iwe imefikia wakati wa hukumu,rejea kifungu cha 91(1)(2) cha sheria ya taratibu za makoza ya jinai(CPA),pia mtuhumiwa anaweza kuachiwa huru endapo muendesha mashtska(PUBLIC PROSECUTER) amejiudhuru kuendelea kuendedha kesi(ame-withdraw) ispokuw tu endapo upande wa utetezi umetoa ushahidi basi muenfesha mashtaka haruhusiwi kujiudhuru na mshtakiwa hawezi kuachwa huru,rejea kifungu cha 98(1)cha sheria hiyohiyo.
 
Back
Top Bottom