sijasema mafuta yapande bali ni kwa gari zisizo za abiria tu. Hivyo kama una taxi au daladala bado utaendelea kununua mafuta kwa bei ya sasa.
Unataka ninunue gari mara ngapi na magari mangapi???fanya juhudi na wewe ununue gari lako sio kuleta mawazo ya wivu kwa waliojinyima na kununua.ninahakika ungekua umejibana na umenunua usafiri wako usingeandika huu upupu
Tanzania hakuna magari mengi isipokua tu ni miundombinu haitoshi. Kuna nchi zina mara 3 ya idadi ya magari ya Tanzania lakini mambo safi.
Hapa cha msingi kemea ufisadi ili hela zitumike kutengeneza miundombinu na sio kukomoa raia wanaojibana ktk matumizi yao. Pia serikali itoke Dar iende inakotakiwa kua, wakihama vigogo wa serikali na magari yao foleni hakuna.
Kumbuka kigogo mmoja akihama familia zaidi ya 3 zitahama i.e familia ya shamba boy, fundi magari,e.t.c na zaidi ya magari matatu yatahama i.e la mke, la watoto, la mshua mwenyewe e.t.c
Naheshimu mawazo yako mukubwa pamoja na ya wengine.
Lakini kwanza ni vema ikafahamika kuwa price ya mafuta or any other goods haiwezi kuwa discriminatory as you suggest.
Pili hata kama ingekuwa ni hivyo how will the sellers control mauzo in this free market era?Utathibitishaje kuwa mnunuzi haendi kuweka katika gari private?
Inabidi kuweka mazingira yatakayodiscourage watu kuja mjini na magari binafsi kwa kuboresha usafiri wa public. Inabidi daladala ziwe, fast, timely, efficient, affordable na reliable. Hili likiwezekana (nchi nyingi za Afrika hatuwezi kwa sasa) ndipo inaweza kuwekwa ushuru fulani kwa watu wenye magari private wanaoingia katikati ya jiji(Hili limefanyika London-UK).
Zaidi ya hapo kuongeza bei ya fuel kwa miji ni impossible (price discrimination).
Nawasilisha.
Unacheza kweli wewe.....uchumi wa wapi huo? Msoga? Watu wa daladala si wataacha biashara ya kubeba abiria na kuanza kulangua mafuta? Simple..... dereva atakuja na dumu atanijazia kwa hiyo 2,000 yako halafu ananiuzia kwa 2,500....kiko wapi!!
Tulishasema sana hapa kitambo....tatizo si wingi wa magari ila uchache wa barabara...serikali ijenge barbara zaidi na kupanua zilizopo
Jamani wana JF mnaona athari za kusoma shule za kata??????? Je bei ya mafuta kwa magari yanayosafirisha vyakula toka mashambani iweje??? kwa sababu nayo si ya abiria.
hahahha, myopic thinking! Hii kitu labda ilishawahi kufanyika nchi gani na ikafanikiwa? maana ni moja ya vitu ambavyo haviwezekani, hata kidogo waulize watu wa Public Economy/Finance watakusaidia huwezi ukawa na policy kama hii. Kuna njia nyingi tu zingine ambazo ni nzuri zaidi katika kupunguza foleni moja nzuri na rahisi ni kuwa na road toll especially kwa gari private zinazoingia mjini hii itasaidia sana kupunguza foleni. Ingine rahisi ni kuboresha tu usafiri wa umma ivi unaifkiri hata kwa bei ya mafuta ya sasa ivi kama tungekuwa na public transport ambayo iko efficient unafikiri ungeona watu wanakimbizana mjini na magari yao private? Thubutu.
Sasa kwa sisi wenye pick ups ambazo tunatumia kama usafiri binafsi tutawekwa kundi gani? Kaa chini na fikiria zaidi, ila nafikiri hufai kufanya kazi ya ushauri unaweza kupoteza nchi aisee:mod:
mkuu una roho ngumu bado unaendelea kutetea hoja yako, ukimaliza foleni ya barabarani kwa mpango huo unapandisha gharama za matibabu maana hospitalini na penyewe kuna foleni za kufa mtu, halafu ukitoka hapo unapandisha gharama za kuchukua na kuweka hela benki maana nako ni balaa, kisha unapandisha gharama za kuwaona tra maana nako ni foleni kwa kwenda mbele, kisha unapandisha ada mashuleni na vyuoni maana madarasa na mabweni hayatoshi watu wanalala hadi wanane chumba kimoja, halafu hakuna kukamata wahalifu maana nafasi magerezani hazitoshi na mahakama za kusikiliza kesi na kutoa hukumu ni chache na mahakimu na majaji ni wachache.
Kazi kweli kweli nchi hii kila mahali foleni hadi dukani kwa mangi na kwenyewe upandishe bei ya vitu.
Bei ya Lita Moja ya Diezel na Petrol kwa Gari ambazo si za ABIRIA IWE SHILINGI 12,000 KUANZIA TAREHE 01 JUNI 2011.
Wagonjwa mahututi na wajawazito wanaokwenda hospital watawaweza kweli kwenda hospital kwa hali hii?,au mwenzetu ni FISADI haujui ugumu wa maisha ulivyo sasa,sie wenzako ni akina PANGU PAKAVU!!,so usiwe mubinafsi bana!
HahahaTunakokwenda italazimu mtu ulale sehemu yako ya kazi, uwe unakwenda kuona familia weekend only. ole wao wale wenye wifu na wenye ndoa changa, lazima mtabebana.