Nikaenda Arusha na ujiko, nikaharibu mbaya…!

Nikaenda Arusha na ujiko, nikaharibu mbaya…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Arusha-Town-clock.jpg

Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kutia timu katika jiji hili la Arusha.......

Ilikuwa ni mwaka 1999, nilienda jijini Arusha kumfuatilia binti mmoja, ambaye alikuwa ni binamu wa rafiki yangu. Ukweli ni kwamba huyu rafiki yangu alikuwa ananifagilia sana kwa huyu binamu yake ili niweze kumwoa. Niliwahi kumwona huyu Binti mara moja tu mwaka 1995 alipokuja Dar kwa mjombake, yaani kwa wazazi wa huyu rafiki yangu.

Kuanzia pale nilimpenda na nilimwambia huyu binamu yake, naye akanishauri nisubiri amalize masomo, ila kuanzia wakati ule akaniambia atakuw akichombeza kwa huyu binamu yake. Ni kweli mwaka 1997 huyu rafiki yangu alienda Arusha kimasomo kwenye chuo kimoja cha uhasibu. Akiwa kule akawa ananijulisha kuhusu binamu yake na namna ambavyo amemweka sawa na amekubali kuwa inawezekana nikawa mume bora.

Tuliendelea na mawasiliano na huyu binti na rafiki yangu, hadi mwaka huo wa 1999 nilipoamua kwenda Arusha. Huyu rafiki yangu alikuwa hajajua rekodi yangu ya unywaji pombe, kwani alipoondoka nilikuwa nakunywa kidogokidogo tu. Lakini pamoja kwamba, nilikuwa nimefikia kunywa ile ya ki-mbwa-mbwa, nilijua nikifika Arusha nitajiheshimu.
Basi nilienda Arusha na nikafikia nyumbani kwao na yule binti kwa mgongo wa binamu yake alikuwa likizo na alikuwa akiishi hapo kwao. Rafiki yangu aliniambia ni vyema sana nikionyesha heshima na adabu kubwa, kwani alishaniwekea ujiko mwingi kwa familia ile kuwa nina adabu na heshima kubwa.

Siku tatu tu baada ya kufika Arusha, siku hiyo tukatoka kwenda kutembea na rafiki yangu akiwa na mpenzi wake na yule binamu yake ambaye ndiye mtarajiwa wangu. Hizi siku tatu nilijinyakulia sifa kubwa kwamba, nina adabu sana kutoka kwa wazazi wa binti na hata binti mwenyewe.
Tulikwenda katika Baa moja maarufu pale Arusha mjini tukala nyama choma huku tukishushia na Bia. Kufika saa tano usiku nikawa wimbideki.

Hii ni kwa sababu siku tatu nilizokaa bila kunywa, zilinipa kiu ya ajabu. Basi rafiki yangu aliponiambia twende nyumbani nilianza kugoma, huku nikisema hovyo. Nilimwomba Yule binti tukalale gesti maana bia zilishashuka chini na aliposema siyo vizuri kulala nje ya nyumbani kwao kwa sababu hajawahi kufanya hivyo, nilimwita changudoa, mshamba wa Arusha.
Lakini hiyo ilikuwa trela tu, kwani picha ilikuwa nyumbani. Nilikubali kwenda nyumbani kwenye mishale ya saa 6 usiku.

Kufika nyumbani, nikaanza kelele mtindo mmoja, maneno yenyewe matusi kibao. Wakwe watarajiwa na ndugu wengine wakaamka na kuuliza kulikoni. Niliwaambia waende ndani wakalale au nitaangusha vita. Wakati huo nilikuwa nimejisaidia haja ndogo kwenye suruali na kila mmoja alikuwa analiona hilo. Yule rafiki yangu na mchumba mtarajiwa na wakwe pamoja na ndugu wengine wa familia ile walikuwa wakinitazama wasiamini kinachotokea.


Nilibwata na baadaye kujilaza kwenye kochi hapo sebuleni. Asubuhi sikusubiri kukumbushwa kwani mengi nilikuwa nayakumbuka. Sikuaga wala nini, nilichomoka na mkoba wangu na kurejea Dar. Nilimwacha rafiki yangu akiwa bafuni , nikaondoka bila hata kunawa uso. Hata hivyo nashukuru, urafiki wetu uliendelea na kuanzia siku ile hadi leo, niliamua kuacha kabisa kunywa pombe.

marejesho naomba usisome hii maneno aisee……….

Hii ilimtokea afki yangu............


CC to: Mungi, Erickb52, Filipo, Preta, Lizzy, Babu DC Dark City, Don Mangi, Arushaone, Liverpool, Kaizer, Madame B, MadameX, cacico, gfsonwin, Lisa, nivea, Suprise, king'asti, snowhite, amu, BADILI TABIA, MwanajamiiOne, FirstLady 1, Remmy, lara 1, Smile, Kipipi, Asnam, jouneGwalu, Mwita Maranya, Asprin, Bishanga, The Boss, watu8, Ruttashobolwa, Mentor, Filipo, Paloma, Jiwe Linaloishi, SnowBall na wakuda wenye kupenda udaku………LOL

 
He! Mtambuzi, kumbe ndiyo wewe mchumba wangu wa zamani uliyefanya vituko nyumbani kwetu Arusha? Umenikumbusha mbali sana. Pole sana, ila hata hivyo nashukuru Mungu kuninusuru na wewe kwa kunionyesha picha halisi ya maisha ambayo ningeishi baada ya kuolewa nawe.
 
Poooole. (is all l can say).


Yaani eti unampa pole Kaunga?

Pole ya kitu gani.....hapa mtu kafanya makossa ya kupuuzi kabisa....anastahili adhabu na siyo kuonewa huruma...

1. Nani alimweleza kuwa unaweza kwenda kulala kwa wakwe watarajiwa??....Hakujua kwamba hilo lilikuwa kosa kubwa la kiufundi, kwani pale kuna watu wazima ambao wanaweza kusoma maandishi hata kama kitabu kimefichwa kwenye box la mbao?

2. Eti akaenda kunywa pombe huku akijua kwamba ana weakness ya kutawala unywaji..

3. Alikuwa anatumia wakala kutafuta mchumba....

4.......

Nadhani anahitaji adhabu huyo kaka....

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Kwani nani alikuambia kwamba ni mimi?
Hii ilimtokea afki yangu na mimi nimeona nisimulie tu hapa JF, unikome kabisa wewe binti............LOL

Mwambie huyo rafiki yako hana adabu...

Halafu kaniudhi sana kwa kweli....

Basi tu, siwezi kusema mengi kwa heshima yako mzee mwenzangu Mtambuzi..

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Kwani nani alikuambia kwamba ni mimi?
Hii ilimtokea afki yangu na mimi nimeona nisimulie tu hapa JF, unikome kabisa wewe binti............LOL

ni wewe mwenyewe mbona ujasema ni rafikio ,una mikasa wewe mzee ,unajua wachagga wanasema mbege ni chakula lakini wakikila wanalewa kaka wewe ulivojinyea Mtambuzi na kujikojolea hahaahahahah
 
Last edited by a moderator:
Yaani eti unampa pole Kaunga?

Pole ya kitu gani.....hapa mtu kafanya makossa ya kupuuzi kabisa....anastahili adhabu na siyo kuonewa huruma...

1. Nani alimweleza kuwa unaweza kwenda kulala kwa wakwe watarajiwa??....Hakujua kwamba hilo lilikuwa kosa kubwa la kiufundi, kwani pale kuna watu wazima ambao wanaweza kusoma maandishi hata kama kitabu kimefichwa kwenye box la mbao?

2. Eti akaenda kunywa pombe huku akijua kwamba ana weakness ya kutawala unywaji..

3. Alikuwa anatumia wakala kutafuta mchumba....

4.......

Nadhani anahitaji adhabu huyo kaka....

Babu DC!!

Watu wenye fani zenu, yaani mimi sikuona makosa hayo kabisa niliishia tu kumuonea huruma na ushamba wake! LOL
 
Yaani eti unampa pole Kaunga?

Pole ya kitu gani.....hapa mtu kafanya makossa ya kupuuzi kabisa....anastahili adhabu na siyo kuonewa huruma...


1. Nani alimweleza kuwa unaweza kwenda kulala kwa wakwe watarajiwa??....Hakujua kwamba hilo lilikuwa kosa kubwa la kiufundi, kwani pale kuna watu wazima ambao wanaweza kusoma maandishi hata kama kitabu kimefichwa kwenye box la mbao?

2. Eti akaenda kunywa pombe huku akijua kwamba ana weakness ya kutawala unywaji..

3. Alikuwa anatumia wakala kutafuta mchumba....

4.......

Nadhani anahitaji adhabu huyo kaka....

Babu DC!!

ubabu wako unatokana na hekima zako! Hata sio umri kama kibabu Asprin!
 
Last edited by a moderator:
Na kweli huyu si wewe...
Maana najua hujaacha kunywa pombe wewe...a.k.a DOMPO ze red one!!!!!:glasses-nerdy:
 
Back
Top Bottom