Nikabebe box majuu!!

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
4,781
Reaction score
14,442
Habari gani wangugu?

Mimi ni kijana ambae nimehitimu shahada hivi punde, miongoni mwa vitu ninavyopenda saana ni kusafiri na kuishi mashariki ya mbali kabisa tofauti na nyumbani nikakutane na watu wapya, sauti mpya, tamaduni mpya, Lugha mpya n.k

Nimefanya shughuli zangu kwa jitihada na juhudi kubwa na hadi sasa nina kiasi cha tsh mil 7/= ningependa kufika New zealand, Canada, Australia, Finland, US..

Hivyo kwa waliotayari kutoa mualiko au msaada wa kufika majuu karibuni, Na wale washauri pia karibuni, na wale haters nawahitaji sana kwa changamoto.

Karibuni!!
 
Nisikukatishe tamaa ila majuu hata ajira za mabox hakuna, labda ukafanye kazi za kuzibua mifeleji ya maji machafu, maana hata kazi za hovyo wenyewe wanafanya siku hizi..Goodluck.


bora hata umemueleza ukweli
 
Nisikukatishe tamaa ila majuu hata ajira za mabox hakuna, labda ukafanye kazi za kuzibua mifeleji ya maji machafu, maana hata kazi za hovyo wenyewe wanafanya siku hizi..Goodluck.

Umesoma maandishi yangu vizuri lakini kaka sokwe? Au..
 
Furaha yangu mimi ni kuishi sehemu tofauti na nyumbani kwa miaka kadhaa.

Nataka kuset internatinal mindset kwangu.
 
Heading yako umesema unataka kwenda kubeba mabox mkuu...halafu una million kadhaa unataka kwenda kutembea na unataka mualiko labda ufafanue zaidi...unataka kwenda kubeba box au matembezi?..Kama ni mabox unajiongopea ndugu yangu, Kama matembezi nakushauri hizo m7 zako anzisha biashara hapo nyumbani, itakuwa haina maana utumie pesa kiasi hicho kwa matembezi halafu urudi bongo uanze zero...otherwise unataka kwenda majuu uzamie huko boss.
 
Tafita hela wewe maisha popoteee
 
Dsm muh'fo if you can make it in here you can make it anywhere,mtafute Field Marshall ES anaratibu safari za US Le big show.
 
Mtu anaposema "kubeba box" huwa anamaanisha nini? Naomba maelezo jamani kwani huwa sielewi huu usemi.
 

Graduate ana millioni saba anataka kwenda kubeba boksi Mashariki ya mbali (halafu hajui hata mashariki ya mbali ni wapi), TUNAHITAJI KUANGALIA UPYA MFUMO MZIMA WA ELIMU NA WOTE TULIOWAPA DHAMANA! Hiyo 7M hapa bongo ukifanya kweli utakuwa na zaidi ya 80M ndani ya mwaka mmoja tu! Kama unaenda matembezi hiyo pesa yako ndani ya wiki unarudi bila kitu mfukoni! CHAGUO NI LAKO.
 
Hahahahahaha.Njoo hapa Brussels uolewe mtoto wa kiume,nani kwakwambia bado kuna kazi hizo kwa wageni?labda jaribu Canada kule kwenye mashamba ya mifugo mkuu.
 
Graduate, umesoma kwa kodi zetu, tumekufundisha uzalendo na mengineyo kweli unawaza kuzama nje na kufanya kazi za vibarua
Fursa zote zilizopo hapa za kufuga nyuki, kilimo cha mpunga mahindi pamba nk
Hapa nina wacwac na huo ugraduate wako
 
Kaka mimi nipo Nchi moja kati ya ulizozitaja, nimeanza mwaka wa pili sasa,nimekuja kusoma, ajira sio kama unavyodhania,ni ngumu kweli kweli,si rasmi wala zisizo rasmi,hapa naskilizia nimalize shule nirudi faster,kisheria nchi nyingi ili upate uhalali wa kuishi mfano hapa nilipo either uje kwa gia ya kusoma au uwe umeshapata ajira na utoe details za mwajiri wako huku,pia uonyeshe benki statement yenye salio lisilopungua dola 15,000.
Ukija kwa gia ya kusoma ndio unatakiwa uwe na mshiko mrefu zaidi maana certificate tu ya mwaka mmoja itakucost si chini ya dola 10000
Bado hujalipa kodi ya nyumba, hapa napoishi ni bei ya chini dola 135 kwa wiki na ni chumba sio nyumba nzima.
Bado hujala bado hujalipa nauli! Komaa na bongo tengeneza pesa ukienda huko unakotaka uende kutembea na kurudi, kuna wabongo wapo huku zaidi ya miaka 10 hakuna cha maana wamefanya, mafanikio makubwa kununua magari tu ambayo yapo ya bei rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…