Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 16,927
- 13,011
Wakuu mtusaidie sisi vijana wa 90s .
Huyu jamaa alihusishwa na mabilioni, sijui alikwapua benki au vipi?
Nilikuwa nasikia sikia tu story zake .
Pasco Na wengine ,mtujuze profile ya huyu jamaa Na alichofanya.
=======
Huyu jamaa alihusishwa na mabilioni, sijui alikwapua benki au vipi?
Nilikuwa nasikia sikia tu story zake .
Pasco Na wengine ,mtujuze profile ya huyu jamaa Na alichofanya.
=======
Mkuu Deo Corleone,
Ilikuwa Tar 2 Mwezi wa Nane mwaka 2001(2 August 2001) siku ya Alhamis, Justine Kasusura akiwa na wenzake watatu wafanyakazi wa Knight Support walikuwa uwanja wa ndege JKNIA wakichukua USD 2mils zilizokuwa zinatoka Marekani na kupelekwa tawi la Citibank(DSM). Ndipo Pepo la wizi lilimuingia Kasusura na kuwaweka wenzake chini ya ulinzi na kupiga hizo fedha.
Kasusura is still serving 30 years behind bars for armed robbery and theft.
Kuweka kumbukumbu sawa,alikua ni mtumishi wa Knight Support Tanzania LTD makao makuu pale Victoria (Dar es salaam),idara ya usafirishaji wa mali na pesa. Siku ya tukio Baba yangu mzazi ndiye aliyekuwa dereva wakiwa na kasusura kwenda airport kupokea pesa hizo.
Ulikua ni mchoro wa muda mrefu kati ya Kasusura,mke wa mkurugenzi wa Knight Support na akina urassa. Baada ya kupokea pesa na kutoka nje ya eneo tu,ndipo kasusura akatoa silaha na kumuwekea Mzee wangu kichwani apaki gari pembeni... zikafika gari za akina urassa wakachukua pesa zote na kutokomea. Mzee wangu akaenda kutoa taarifa kituoni,akachukuliwa na kuwekwa ndani kusaidia upelelezi. Kesi iliendelea akiwa gerezani keko,hadi kasusura alipokamatwa ndipo akaachiwa huru.
Ramani ya wizi: Siku ya tukio escotter wa zamu alijifanya anaumwa,ndipo Mke wa Mkurugenzi akaagiza Kasusura aje ashike zamu,akakabidhiwa silaha...ndipo mchezo ulivyokuwa.
Kesi yake ilikuwa na jambo moja kuu nalo ni jinsi alivyoteswa akiwa mikononi mwa polisi.Na ni Abdalla Zombe aliyeifanya shughuli hiyo.
Nikikumbuka maelezo na nikiskia Abdallah Zombe,naichukia dunia!!!!!!!
I wish kama ningepata fursa ya kufuatilia maisha binafsi ya Zombe.