Bado ni kitendawili waliofaidi mabilioni ya Justine Kasusura

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Jumapili January 17 2021

Kwa miezi 12 baada ya Ijumaa ya tarehe 2 Agosti, 2001, hakuna jina lililotawala vyombo vya habari kama la Justine Kasusura, aliyedaiwa kupora dola za Marekani milioni mbili (Sh4.4 bilioni) bila kutumia nguvu kubwa.

Kiasi cha fedha alichodaiwa kupora, staili aliyotumia na ukubwa ambao tukio hilo lilipewa na vyombo vya habari kumelifanya lisifutike kirahisi kwenye kumbukumbu za wengi.

Kasusura aliyekuwa ameajiriwa na kampuni ya ulinzi ya Knight Support alidaiwa kupora fedha hizo muda mfupi baada ya kuzipokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa njiani na mfanyakazi mwenzake kuelekea benki ya Citibank.

Hadi kesi dhidi ya Kasusura aliyekamatwa miezi mitano baada ya tukio inamalizika, Jeshi la Polisi lilidai kuambulia Sh256,000 tu mikononi mwake.

Kutopatikana fedha hizo kumeacha fumbo. Ni wapi fedha hizo zinazotosha kumlipa mkandarasi atakayejenga upya miundombinu ya eneo zima la Jangwani ziliishia? Ni nani hasa waliofaidi fedha hizo?

Uporaji ulivyotekelezwa

Tukio zima lilianza hivi; asubuhi ya tarehe 2 Agosti 2001, Kasusura na mfanyakazi mwenziwe, Said Hamisi, walioajiriwa na Knight Support walielekezwa na meneja wa kampuni hiyo aliyeitwa Doren kwenda Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kupokea mzigo na kuupeleka katika benki ya Citibank katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Kama ilivyokuwa kawaida ya kampuni hiyo, Kasusura, aliyeajiriwa kama dereva, alikabidhiwa bastola na risasi kadhaa huku mwenzake akikabidhiwa simu ya mkononi ili kufanikisha mawasiliano.

Safari kutoka makao makuu ya Knight Support iliyokuwa eneo la Victoria ilianza vizuri. Wakiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege walisimama mara moja tu kujaza
Mafuta

Wakiwa uwanja wa ndege, walikutana na maofisa wa kampuni ya Dahaco iliyoshughulika na mizigo ya kutoka nje ya nchi. Baada ya mazungumzo mafupi majira ya saa nne asubuhi Kasusura aliitwa na kusaini nyaraka kadhaa kabla ya kukabidhiwa mzigo walioufuata.

Kasusura aliuweka mzigo huo nyuma ya nyuma ya gari hilo aina ya Toyota Hilux Double Cabin lililofunikwa pande zote na kufunga kwa ufunguo. Wakati wakiondoka, Kasusura alimfahamisha Doren kwa njia ya simu kuwa walikuwa wakiondoka uwanjani hapo na kwamba aliweka mzigo huo nyuma ya gari na kufunga kwa ufunguo.

Walipotoka eneo la uwanja wa ndege, waliona gari likiwa limeegeshwa pembeni mwa barabara. Kasusura alikwenda moja kwa moja na kuliegesha gari akiendesha mbele ya gari hilo aina ya Toyota Land Cruser.

Hapa Kasusura alimweleza mfanyakazi mwenzake kuwa “biashara imekwisha” na kumtaka afungue boksi walilopokea uwanja wa ndege huku akimwelekezea bastola.

Alipoona mwenzake anasuasua, Kasusura alichukua funguo na simu ya mkononi kutoka kwa mwenzake na kuchukua ule mzigo akisaidiwa na watu wengine wawili waliokuwa kwenye gari walilolikuta pale.

Baada ya Kasusura na wenzake kutoweka na wenzake, Hamis aliomba msaada na kuripoti tukio hilo kituo cha Polisi Stakishari.

Taifa lashtuka

Siku iliyofuata aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana aliutangazia umma tukio la uporaji wa fedha za Citibank.

Alisema tayari askari walikuwa wamejipanga kila kona ya nchi kumsaka mhalifu huyo, huku akiwaambia kutoa taarifa endapo watamwona au watahisi uwepo wake mahali popote.

Kasusura akamatwa Mbeya

Miezi mitano ilipita bila Kasusura kukamatwa. Habari zake ziliendelea kutawala vyombo vya habari

Taarifa za uwepo wa Kasusura mkoani Mbeya zilitolewa na msiri wa polisi.

Akiwa nyumbani kwake majira ya saa tatu usiku tarehe 24 Disemba 2001, Inspekta wa Polisi Richard Tadei alipokea taarifa kuwa katika nyumba ya kulala wageni ya Three in One iliyoko eneo la Soweto mkoani Mbeya alikuwapo mhalifu hatari aliyekuwa akitafutwa na polisi.

Baada ya kufanya ufuatiliaji na kujiridhisha kuwa mtu aliyekuwa akiishi katika hoteli hiyo alikuwa Kasusura, Inspekta Richard aliandaa askari wenzake na kuweka mtego wa kumnasa Kasusura.

Bila kujua siku zake zinahesabika, usiku wa manane siku ya mkesha wa Krismasi ya tarehe 24 Desemba, 2001, Kasusura aliingia kwenye chumba chake namba 101k hotelini hapo akiambatana na mwanamke.

Alipofungua mlango alikutana na askari ambao tayari walikuwa wamejificha sehemu mbali mbali ndani ya chumba hicho. Wengine walikuwa wameizingira hoteli. Alipofungua tu mlango, Kasusura alijikuta akiangukia mikononi mwa askari.

Ushahidi uliotolewa mahakamani na nyaraka nyingine zinaonyesha Kasusura alikutwa na Sh256,000 tu baada ya kupekuliwa.

Haikuwa mara ya kwanza kukamatwa

Kabla ya kukamatwa Kasusura, uvumi ulisambaa kuwa Kasusura amewahi kukamatwa mara kadhaa lakini amekuwa akiponyoka mikononi mwa polisi kwa nguvu ya fedha.

Taarifa hizo zilizidi kuvuma kiasi cha kumuibua hadharani aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Omar Mahita na kutangaza kuwa askari watano walikuwa wakihojiwa kwa tuhuma za kumkamata na kumwachia Kasusura.

Siku chache baadaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Adadi Rajabu, alitangaza kufukuzwa kazi kwa askari wote waliotuhumiwa kumkamata na kumwachia Kasusura.

Ashtakiwa Kisutu

Tarehe 7 Januari, 2002 Kasusura na wenzake sita walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam katika kesi ambayo ilivuta hisia za watu wengi.

Walishtakiwa kwa kosa la kula njama, unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi na kupokea mali ya wizi.

Ahukumiwa

Ijumaa ya tarehe 30 Machi, 2007, Hakimu Mkuu Mfawidhi Sivangilwa Mwangesi ambaye sasa ni jaji wa Mahakama ya Rufani alimhukumu Kasusura kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi. Pia, alihukumiwa kuchapwa viboko 12.

Mahakama Kuu yatupa rufaa yake

Mara tu baada ya kuhukumiwa, Kasusura alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga kutiwa hatiani na kufungwa. Mwezi Juni, 2010, Jaji Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa hiyo ikidai haikuwa na hoja za kutosha kuishawishi kutengua uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Kutupwa kwa rufaa yake hakukumkatisha tamaa. Juni 4, 2015, Kasusura alikata rufaa ya pili katika Mahakama ya Rufani huku akiwasilisha sababu tisa kwa nini anapinga kifungo dhidi yake.

Ashinda rufaa

Tarehe 3 Mei, 2016 Mahakama ya Rufani ilikubaliana na hoja za Kasusura kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kumhukumu miaka 30 jela.

Ilisema wakati akidaiwa kutenda kosa hilo mabadiliko ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu yanayoelekeza kifungo cha miaka 30 kwa mtu anayetiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha yalikuwa hayajaanza kutumika. Mahakama ilikubali hoja ya Kasusura kuwa maelezo yake ya onyo alimodaiwa kukiri kosa yalipokelewa mahakamani kinyume cha utaratibu uliowekwa na Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Mahakama iliona maelezo ya onyo ya Kasusura yalikuwa batili kwa kuwa yalirekodiwa baada ya muda wa kisheria kupita.

Kasusura alikamatwa tarehe 24 Disemba, 2001 lakini maelezo yake yalichukuliwa tarehe 26 Disemba, 2001.

Mahakama pia ilikubaliana na Kasusura kuwa kushindwa kwa upande wa mashtaka kuwaita maofisa wa benki ya Citibank waliokuwa wamiliki wa mzigo ulioibwa kulileta shaka kubwa kuhusu aina na kiasi cha fedha zilizokuwa ndani na mzigo huo.

Uamuzi wa kuwachia Kasusura ulitolewa na majaji Mbarouk Mbarouk, Sauda Mjasiri na Semistocle Kaijage ambaye sasa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ni nani aliyefaidi mabilioni yaliyodaiwa kuporwa na Kasusura? Si Kasusura wala Jeshi la Polisi wameweza kujibu swali hili miaka 20 tangu tukio hilo litokee.
 
Hao majaji watatu waliomwachia wachunguzwe ukwasi walio nao, si ajabu wamegawana walau kabilioni kamoja
 
Kuna mzee mmoja bwashee, ndie alihifadhi/ kumwekea Kasusura minoti yake, jamaa kila akidakwa huko mikoani na Polisi anamtwangia mzee, mzee anatuma minoti,.... movie likasoooonga,mzee akaona huu ujinga...alipodakwa kwa mara ya mwisho akamwambia feza hakuna imeisha!.... movie ndo ikaishia hapo.
 
Sielewi kwanini Mwandishi wa habari hii ameshindwa kuimalizia vizuri.. Kasusura yuko wapi kwa sasa? Je alimuhoji chochote kuhusu hizo fedha..hatujui labda zilipelekwa nje ya nchi na jamaa alivyoshinda rufaa alienda huko!!!
 
Ilikuwa Ijumaa ya Augost 3, 2001 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, ALFRED TIBAIGANA, alitangaza kutokea unyan'ganyi wa fedha kiasi cha U$D 2 Milioni (Tsh 4,400,000,000/=) uliofanyika majira ya saa 5 asubuhi nje kidogo ya "Airport" ya JKIA Augost 2, mwaka huo.

RPC TIBAIGANA alimtaja mtuhimiwa was wizi huo ni JUSTINE KAKURU KASUSURA, ambaye aliiuwa dereva wa gari la Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support yenye makao makuu yake eneo la Victoria, Dar es salaam.

Kamanda TIBAIGANA alisema mtuhumiwa huyo ametoweka na fedha hizo kusiko julikana na msako mkali umeanza nchi nzima hususan maeneo ya mipakani.

Aidha alitoa rai kwa wananchi na wasamaria wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo. Lakini ilipita miezi 5 bila kukamatwa.

Kipindi cha miezi 5 bila kukamatwa kilizuwa gumzo kwa wananchi wengi wakiamini kuwa huenda kakimbilia nje ya nchi, lakini taarifa za siri zilipatikana na kusaidia kukamatwa kwake usiku wa manane, Jumatatu ya Desemba 24, mwaka 2001 katika Hoteli ijulikanayo kama "Three In One" iliyoko maeneo ya Soweto, Mbeya.

Inadaiwa KASUSURA alifika hotelini hapo siku ya Jumapili, Desemba 23, 2001 saa 12 jioni akitokea Sumbawanga akijifanya mfanyabishara akiwa amevalia kofia kubwa kuficha uso wake na kupewa chumba Na. 101K ambapo katika rejista alijisajili kwa jina bandia la JOHN LAIZER na kulipia chumba malazi ya siku moja kwa Sh 3,500/=.

Jioni yake baada ya kakamilisha taratibu za chumba alitoka kwenda kujivinjari na ndipo Askari walipoingia chumbani kwakwe kukuwekea mtego was kumnasa.

KASUSURA akiwa amekwisha ianza Kristmas alirejea huku usiku akiwa kalewa na kimwana wake na mara baada ya kuingia ndani, alikutana uso kwa uso na askari walioibuka kutoka uvunguni na kabatini na kumtia nguvuni kilaini.

Hate hivyo baada ya upekuzi alikutwa na akiwa na Sh 200.000/= tu!

FB_IMG_1683589826453.jpg
FB_IMG_1683589822551.jpg

Bado ni kitendawili waliofaidi mabilioni ya Justine Kasusura.

Justine Kasusura akitoka katika jengo la Mahakama kuu jijini Dar es Salaam ambapo rufaa yake ya kwanza ilisikilizwa na kutupwa.

Kiasi cha fedha alichodaiwa kupora, staili aliyotumia na ukubwa ambao tukio hilo lilipewa na vyombo vya habari kumelifanya lisifutike kirahisi kwenye kumbukumbu za wengi.

Kwa miezi 12 baada ya Ijumaa ya tarehe 2 Agosti, 2001, hakuna jina lililotawala vyombo vya habari kama la Justine Kasusura, aliyedaiwa kupora dola za Marekani milioni mbili (Sh4.4 bilioni) bila kutumia nguvu kubwa.

Kasusura aliyekuwa ameajiriwa na kampuni ya ulinzi ya Knight Support alidaiwa kupora fedha hizo muda mfupi baada ya kuzipokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa njiani na mfanyakazi mwenzake kuelekea benki ya Citibank.

Kiasi cha fedha alichodaiwa kupora, staili aliyotumia na ukubwa ambao tukio hilo lilipewa na vyombo vya habari kumelifanya lisifutike kirahisi kwenye kumbukumbu za wengi.

Hadi kesi dhidi ya Kasusura aliyekamatwa miezi mitano baada ya tukio inamalizika, Jeshi la Polisi lilidai kuambulia Sh256,000 tu mikononi mwake.

Kutopatikana fedha hizo kumeacha fumbo. Ni wapi fedha hizo zinazotosha kumlipa mkandarasi atakayejenga upya miundombinu ya eneo zima la Jangwani ziliishia? Ni nani hasa waliofaidi fedha hizo?

Uporaji ulivyotekelezwa
Tukio zima lilianza hivi; asubuhi ya tarehe 2 Agosti 2001, Kasusura na mfanyakazi mwenziwe, Said Hamisi, walioajiriwa na Knight Support walielekezwa na meneja wa kampuni hiyo aliyeitwa Doren kwenda Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kupokea mzigo na kuupeleka katika benki ya Citibank katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Kama ilivyokuwa kawaida ya kampuni hiyo, Kasusura, aliyeajiriwa kama dereva, alikabidhiwa bastola na risasi kadhaa huku mwenzake akikabidhiwa simu ya mkononi ili kufanikisha mawasiliano.

Safari kutoka makao makuu ya Knight Support iliyokuwa eneo la Victoria ilianza vizuri. Wakiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege walisimama mara moja tu kujaza mafuta.

Back
Top Bottom