Nijizuieje nisile RUSHWA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nijizuieje nisile RUSHWA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Jun 18, 2011.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ndg zangu wana JF na watanzania kwa ujumla. Na mika mingi tangu nimalize elimu ya juu hapa TZ nikabahatika kupata kazi. Kazi yangu ni inahusika na kutoa huduma kwa wateja sasa kabla hata sijaomba wala kuonyesha dalili za kuitaka rushwa wateja wamekuwa wakiniwekea katikati ya forms zao kiasi cha fedha kila mara nacho kifanya kwa vile kuna number zao za simu nawapigia na wakija nazirudisha zile fedha. Kwa sasa nakaribia kushindwa uvumilivu kwa vile kodi za nyumba ziko juu sana sana, nimekopa bank ili nijenge nimepata milioni 3 na nusu viwanja hatua 20x20 ni mil 5 je nitajenga kweli? Na shirika halina hata mpango wa kuongeza mishahara.

  Wakati mwingine nashawishika Kula rushwa ila namwona kama Dr. Slaa ananiambia endelea tu watanzania wanakuona. Naona naharibu imani yangu na Mungu wangu.kwa sasa sahani ya chakula cha mchana imefikia TZS 3500-5000 na 3500 kwa maeneo ya ofisi yetu ni kwa mama ntilie. Wenzangu mnafanyaje mkipambana na hali kama hizi??

  Cha kushangaza wenzangu niliotoka nao chuo wenye kipato almost sawa wana majumba makubwa Boko na Mbweni. Maisha sio mchezo.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kama inawezekana omba ubadilishwe kitengo ili uepukane na ushawishi.
   
 3. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  we kula rushwa bana, nchi yenyewe hii hata usipokula wenzio wanakula, kwa hiyo ili kuwe na uwiano, rushwa lazima itumike, kwa mfano kama hii bajeti iliyopita inasema adhabu za barabarani zitakuwa elfu 50,000, nani atatoa hiyo pesa instantly? si bora nimshikishe traffic police 5000 nisave 45000,elfu ishirini yenyewe ilikuwa kimbembe, rushwa is there to stay, Takukuru am soree
   
 4. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kama ushafikia uamuzi vile..
  Ushauri wangu: decide the end, then ponder the means.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  endelea mkuu, kamata mshiko ukajenge (lakini suilewee na kuhonga)... ndio mtindo wa maiswha huo siku hizi
   
 6. s

  sugi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  we zibamande tu,ndo utaratibu wa nchi yetu kwa sasa,yaan kila sehemu rushwa tu,ukiacha wewe wenzio watapokea tu!no body cares in this goddamn country,she i full of shit!huwez kujenga nchi peke yako bwana,4get about it,ni bora tuharibu kabisaaaaa!then baadae wote tuone kuwa rushwa c nzuri na tukubaliane wote kuiacha,kuliko wengine wanaacha wengine wanakomaa nayo,na kufisdi nchi,this is nonsense!
   
 7. s

  sugi JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  "takukuru my ass"
   
 8. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hongera kwa kuwa mwadilifu na mwaminifu! Na Mungu abariki kazi ya mikono yako!
   
 9. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ushauri wa kula rushwa ni wa kijinga saana. Tamaa hazisaidii katika dunia hii. Unajenga nyumba kisha unajua ninaishi ndani ya rushwa. Unakula chakula, unajua nakula rushwa. Ndugu yangu kama umeandika haya kwa yakini, basi nakusihi saana fikiria kujiendeleza au tafuta means ya kuwa hata na biashara nyingine uongeze kipato, utaishi kwa amani saana.
  Maisha au mali inayopatikana kwa rushwa haina amani wala raha bali ni karaha tu. Behaviorists wanasema kwamba, ukipata kitu kwa jasho lako mwenyewe basi utunzaji wake ni tofauti na ule ambao unapatikana kwa njia tofauti. Labda nikutolee mfano kwenye very basic level; Leo kampuni ya simu ikisema kutuma meseji ni free basi hata kama hauna shida utahangaika na simu yako ili uipate ile free. Vivyohivyo, kipato kwa njia ya rushwa kitakufanya uanze kutafuta matumizi na hata kama utaamua kutoa sadaka haisaidii kitu.
   
 10. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zingatia ushauri huu.Kumbe kuna wa TZ wenye akili.Mungu abariki kazi za mikono yako ANFAAL.
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu nilishtuka baathi ya comment hapo juu kuhusu kupokea na kula rushwa. Nilivyosoma hii post yako nimepata nguvu ya kupingana na hali ya kishawishi kibaya. Nimeandika hii post serious kabisa sio kwamba ni utani. Nashukuru kwa kunionya na kunitia moyo. Pia Wat TZ tusipende kutia wenzetu katika majaribu unavyomshindilia mtu hela huku hana unamweka kwenye wakati mgumu.
   
 12. d

  deezle23 Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  zitwange tu chamwenzio sio chakwako.
   
 13. s

  sugi JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  mwambie mkuu,haelewi!
   
 14. s

  sugi JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  unaonekana bado hujawahi kwenda sehemu nyeti ukaombwa rushwa,kama vile hospitali,mahakamani,polisi na sehemu nyingine,ipo siku utakwenda sehemu hizi utakosa huduma,au utaipata kwa muda ambao utakuumiza,tulia tu,kupokea rushwa kutakuja automatically!wala hutatuomba tena ushauri humu,utaanza kuzitwanga kimya kimya tu!
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  usitoe wala kupoke rushwa,rushwa ni adui wa haki,tokomeza rushwa

  ila kama wanakupa kama kukukirimu haina noma pokea na kula lakini kama lengo ni wao kukutaka wewe kuwarahisishia kazi zao SEMA HAPANA,ila kama ni baada ya kazi YAANI baada ya wewe kumaliza kazi ya kuwahudumia na wakafurahia kwa kukupa chochote haina shida pokea
   
 16. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mhhhh!!!...watu wenye attitude kama ya kwako, ndo mnaosababisha nchi yetu iwe kama ilivyo leo....:(
   
 17. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Thanks for uadilifu...ushauri wangu kama unaona temptation zimezidi..Omba uhamisho kwenda mikoani au vijijini...kule watu hawana hata hiyo hela ya kutoa rushwa..

  Pia kama kweli unayo nia ya kutopokea rushwa ..huwezi kulinganisha ujenzi versus mapato + time.....Fanya unachoweza..Fikiri kujenga kutokana na kipato chako ..itachukua miaka mingi na rafiki zako watakucheka..lakini kaza buti ..inawezekana..
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  chukua hela hizo,.rushwa unaijua wewe?kama hiyo wanayokupa wateja ni rushwa anayopokea rostam,lowassa,chenge,jk na vigogo tuiiteje?kama yako ni rushwa basi yao ni mauaji kwa risasi,utaiacha hiyo hela na barabara ya kuingia mtaani kwenu itaendelea kuwa ya vumbi...this is what they made us,..iam a ma made nigga...uzalendo umeshaisha nchi hii.
   
 19. s

  sugi JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  nisaidie mkuu kumuelimisha huyu bwana,naona hanielewi kabisaaaaa,anjaribu kujaza maji kwenye gunia!yupo kwenye tanzania ya akina sokoine bado,hajui sasa ni akina rostam,chenge lowassa nk,watanzania amkeni tushirikiane kubomoa ili baadae wote tufeel uharibifu,kama kuijenga upya nchi tuamue wote,sio wachache wanajenga halafu wengine wanabomoa!
   
 20. s

  sugi JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  mbegu huharibika ili kutoa mmea mzuri,sasa kama wakubwa wanabomoa,c bora tuwasaidie kubomoa ili tuharibu kabisaaaaa,halafu baadae tukiona madhara kwa pamoja tutafeel na kuwa responsible kwa nchi yetu,nakuambia wengine hawafeel kabisa nchi hii,rostam,lowassa utawazungumziaje wewe?lazima tuzungumze lugha moja,na hii itakuja automatically kama we will all get a pain in an ass
   
Loading...