Night Unlimited

Night Unlimited

Mbona mi natumia muda wote.fanya hivi:ukishajiunga wajanja night jiunge na bando nyingne hata zile za cheka ya 499tsh.then ikishfika saa 12 kama gb yako haikuisha utaendelea kutumia mchana kutwa na utadownload files za kutosha tu
files za kotosha within 1gb au hizo za kutosha ni gb ngapi?
 
zantel unlimited ya mwezi 300, 000 hahahha hawa wapemba wanaakili hivi hivi vodacom unlimited yao ya 40000 ni full au nao gb 2 speed inashuka

voda unlimited ni unlimited data tu na sio unlimited speed. megaboksi ya elf 10 kwa mwezi ina speed kushinda hio voda ya 40,000. hio ya zantel ni unlimited sema nayo kama eneo speed si nzuri ya zantel pia haina maana.
 
hahahahahahaaaaaa dah! shukran mkuu hawa jamaa hawako serious kabisa na data business, miaka ya nyuma walikuwa wanasifika kwa spidi ila sasa i think ndo wako katika rank za mwisho.. naona kiujumla bongo data ishakuwa ishu ngumu, hivi airtel bado wanauza Gb1 kwa ile bundle ya 1000???

WALIKUWA WANAJIUNGA VIPI IYO ya 1gb iyo hapo kale
 
dar zantel wana speed kuliko mtandao wowote. kujua speed ya mtandao usitumie na kifurushi tumia vocha then nenda speedtest. minimum speed nilikua napata 4mbps.

Mkuu mi naishi Kibamba huku aibu wapo slow
 
lina maana pana.
-unlimited browsing
-unlimited download and browsing
-unlimited speed

kuna unlimited nyingi. kuna bundle zina speed 2kbps lakini ni unlimited data japo speed mbovu.

inabidi wewe mteja ndio ujue unahitaji nini

hizo ni lugha za kibiashara tu. za kudanganya wateja. unlimited maana yake ni unlimited kila nyanja. kuanzia speed, browsing hadi downloading.
ukiweka kizingiti tu kulimit kitu maana yake tayari limited. sasa isp anakupa day unlimited browsing kisha akulimit kudownload au speed kisha bado iwe unlimited? it is limited to speed or any factor whatsoever
 
zantel unlimited ya mwezi 300, 000 hahahha hawa wapemba wanaakili hivi hivi vodacom unlimited yao ya 40000 ni full au nao gb 2 speed inashuka
correction: sio wapemba ni wahindi ndio wapangaji wa zantel. tena wahindi wa kununuliwa toka india.
vodacom ya elfu 40 speed inashuka baada ya 2GB
 
hizo ni lugha za kibiashara tu. za kudanganya wateja. unlimited maana yake ni unlimited kila nyanja. kuanzia speed, browsing hadi downloading.
ukiweka kizingiti tu kulimit kitu maana yake tayari limited. sasa isp anakupa day unlimited browsing kisha akulimit kudownload au speed kisha bado iwe unlimited? it is limited to speed or any factor whatsoever

hakuna unlimited ya kila nyanja ipo unlimited ya ki category kama nilivyotaja.

mfano nikinunua bundle ya unlimited unayosema wewe nikatumia kwenye computer mbili basi speed itagawanyika nayo. tuseme isp ananipa 10mbps basi speed ya computer ya kwanza na ya pili ukizijumlisha utapata 10mbps na sio 20mbps hivyo maana ya neno unlimited imeshaharibika

inshort unlimited speed haiexist sababu tunatumia shared connection. leo unapata 20mbps sababu kwenye mji wenu wapo watu 100 tu wanaotumia mtandao, ila siku wakiongezeka wakawa watu 2000 speed inashuka hadi 1mbps labda mtandao waongeze capacity ya minara yao.

na wanaposema unlimited browsing wapo sahihi kaka sababu ni browsing na sio streming na sio downloading ni wewe sasa mteja kujua maana ya neno browsing ili ujue kama ni kifurushi kinachokufaa.

kama ni mtu wa enterprise mobile data si mahala pako inabidi uwe na wifi au isp wa enterprise sababu wao peke yao ndo wanatoa true unlimited ya kila nyanja kuanzia browsing, streaming, downloading na hata uploading.
 
Back
Top Bottom