Night Unlimited

Night Unlimited

mshihiri

Senior Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
138
Reaction score
89
Sasa unaweza kuperuzi usiku mzima ukijiunga na bundle zetu za Night Unlimited.
Ukiwa na Tsh 450, unapata kifurushi cha Night Surfer 1GB na kwa Tsh 900 unapata kifurushi cha Night Surfer 2GB ambapo ukiwa na kifurushi hichi pia unaweza piga Zantel kwenda Zantel bila kikomo.

Vifurushi vyote hivi vinadumu kuanzia saa tano usiku hadi 12 asubuhi.
Jiunge sasa kwa kupiga *149*07# kisha chagua namba 7. Au jiunge kupitia tovuti yetu www.zantel.com
 
Zantel punguzeni gharama za internet hata hivyo spidi yenu iko chini sana kwenye maeneo yangu. (gprs) afadhali kama hata mngekuwa na Edge. Fanyeni roaming
 
Mkuu tangu lini GB mbili ikawa Unlimited ?, mimi mlinipoteza mlivyofuta Unlimited ya Siku Tatu kwa Elfu 15, tena tabia yenu mbovu sana mnafuta vitu kimya kimya tu, Sasa hio tena kuanzia saa Tano usiku ?, si bora niendelee na Banjuka Unlimited ya Kweli ya Lisaa lizima kwa 650 tena kuanzia saa tatu.
 
Kuna siku niliona kwenye Tv wanaburuza nyaya za optic kutoka baharini nikaamini watakuwa ndio ma ISP Wenye kiwano cha juu, nilinunua modem yao nikawa nina subscribe bundle ya unlimited kwa siku 3. Cha kushangaza, wakawa wanapandisha bei kila kukicha na mbaya zaidi speed inakuwa kubwa mwanzoni ukishadownload kama mb 500 tuu,m kichefuchefu kinaanza.speed kama ya konokono au kinyonga.

Mimi ninawashauri waboreshe huduma ya internete kwa bara watapata wateja wengi na visiwani wabakie na mawasiliano ya simu.Vilevile watengeneze menue ambayo ni userfriend ya kujiunga na bundle
 
mshihiri

Kama unafanya kazi Zantel hivi huwa mnafanya kazi kwa kulazimishwa au kujitolea au hamlipwi..., mlivyotoa Unlimited siku Tatu hamkumwabia mtu, alafu kwenye website mkawa bado mnaziita Mono, Regular n.k. Wakati sasa hivi plan zinaitwa w2g na vitu kama hivyo..

sasa wewe unasema kwa maelezo zaidi mtu aende hapa Zantel | Part of Etisalat

Uliona shida gani kumuelekeza mtu kwenye link ya moja kwa moja kuliko yeye ndio aanze kutafuta hayo maelezo yapo wapi?
 
Last edited by a moderator:
Kuna siku niliona kwenye Tv wanaburuza nyaya za optic kutoka baharini nikaamini watakuwa ndio ma ISP Wenye kiwano cha juu, nilinunua modem yao nikawa nina subscribe bundle ya unlimited kwa siku 3. Cha kushangaza, wakawa wanapandisha bei kila kukicha na mbaya zaidi speed inakuwa kubwa mwanzoni ukishadownload kama mb 500 tuu,m kichefuchefu kinaanza.speed kama ya konokono au kinyonga.

Mimi ninawashauri waboreshe huduma ya internete kwa bara watapata wateja wengi na visiwani wabakie na mawasiliano ya simu.Vilevile watengeneze menue ambayo ni userfriend ya kujiunga na bundle

Kwa Speed mkuu inategemea na maeneo mimi kipindi kile nilivyokuwa natumia nilikuwa nikuweka EVDO only inakuwa na kasi mpaka mwisho, ila inategemea upo wapi, nilishaitumia hii nilivyokuwa Arusha Speed ikawa mbovu kwelikweli lakini nilivyokuwa Mwanza Speed ilikuwa nzuri tu.., Tatizo ni hawa jamaa kubadilisha vifurushi kila siku na kupandisha bei kila kukicha bila kutoa hata taarifa..., sasa hivi Unlimited wanayo moja tu ya mwezi kwa Laki Tatu.., sasa mtu kweli unatumia internet kuliko hata pango lako la nyumba ?
 
Hivi unlimited maana yake ni nini!? Huenda silijui vizuri hili neno!

lina maana pana.
-unlimited browsing
-unlimited download and browsing
-unlimited speed

kuna unlimited nyingi. kuna bundle zina speed 2kbps lakini ni unlimited data japo speed mbovu.

inabidi wewe mteja ndio ujue unahitaji nini
 
Mi napenda zaidi unlimited downloading Na unlimited speed. Na kwa upande huu bado Vodacom nawapa credit ingawa upande wa downloading wameanza ku-limit mfano sahivi wajanja mia 5 unapata 1gb
 
lina maana pana.
-unlimited browsing
-unlimited download and browsing
-unlimited speed

kuna unlimited nyingi. kuna bundle zina speed 2kbps lakini ni unlimited data japo speed mbovu.

inabidi wewe mteja ndio ujue unahitaji nini
Nimeupenda sana ufafanuzi wako, ila hawa wajomba hawafafanui kwenye matangazo yao ilitujue wanazungumzia kipi kati ya hivyo ingawa kipengele cha unlimited download najua haiwezekani
 
Nimeupenda sana ufafanuzi wako, ila hawa wajomba hawafafanui kwenye matangazo yao ilitujue wanazungumzia kipi kati ya hivyo ingawa kipengele cha unlimited download najua haiwezekani

Mbona wameandika mkuu, soma tangazo wanasema unlimited ku-surf, sasa sijuwi kama kuna mtu anahitaji kitu kama hicho.

Unlimited downloading inawezekana kabisa, kipindi fulani airtel walikuwa nayo kwa sh 200 tu na ilikuwa 24hrs yaani mchana na hata usiku, baadaye Vodacom kupitia wajanja night offer kwa sh 200 pia ulikuwa una download utakavyo ila usiku tu ambayo kwa sasa wamebadili kwanza wamepandisha bei ni sh 500 na wamelimit to 1gb
 
Sasa hivi tumeshikwa pabaya sana, Zantel wameziba matundu, Tigo megabox wamebana kuanzia jana hamna tena unlimited surfing,
Ila nawapongeza tigo kwa kuboresha huduma za internet, Hawa wengine kina Zantel wanazingua sana yaani unlimited ya mwezi kwa laki tatu!!! me nawashauli ni bora tu waifunge kampuni yao maana tokea nianze kutumia simu sijawi wasiliana na mtu mwenye line ya Zantel.
 
Hawa Zantel ni MAJANGA matupu sijui hata wanafanya nini kwa market,yaani they better go back to Zanzibar period wanauzi sana,yaani modem Yao ni kimeo cha mwisho-I HATE ZANTEL
 
Inabidi sasa turudi kwenye vile vitu vyetu vya zamani,ila humu ndani nadhani watu walishahamisha kambi,sioni kabisa watu wakipost ule ujuzi
 
Inabidi sasa turudi kwenye vile vitu vyetu vya zamani,ila humu ndani nadhani watu walishahamisha kambi,sioni kabisa watu wakipost ule ujuzi

Kwa sasa hivi hamna cha basi la blue, kijani wala jekundu yote kwisha kazi, kilichobaki ni kupakuwa kwa urefu wa kamba yako tu.
 
Duh..unlimited ya wapi hiyo?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom