Nigeria yaahidi kuwatafuta wanafunzi

Nigeria yaahidi kuwatafuta wanafunzi

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,572
Reaction score
53,586
Juhudi za kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Boko Haram, zimepewa kipaombele katika mkutano wa serikali kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.
Mkutano huo uliongozwa na Rais Goodluck Jonathan.
[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



Mkutano wenyewe uliodumu kwa saa sita, ulihudhuriwa na maafisa wakuu wa usalama , mawaziri na maafisa wakuu wa serikali kutoka pande zote..upande wa waisilamu na wakristo.
Wanaouhudhuria walikubaliana kuwa mgogoro kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, Kaskazini mwa nchi sio vita vya kidini bali vita dhidi ya raia wa Nigeria.
130920141800_nigeria_security_304x171_ap_nocredit.jpg
Juhudi za serikali kupambana na Boko Haram Nigeria zimeonekana kupatwa na changamoto nyingi


Wanafunzi zaidi ya miambili walitekwa nyara wiki jana na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram na kuwapeleka msituni.
Baadhi ya wasichana hao walifanikiwa kutoroka lakini wengine wengi wangali wanazuiliwa.
Wapiganaji hao wamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini humo wakidai kuwa wanapigania kile wanachosema ni misingi ya dini ya kiisilamu.
Kundi hilo pia lilikiri kufanya shambulizi baya katika kituo cha basi mjini Abuja wiki jana ambapo zaidi ya watu 70



Nigeria yaahidi kuwatafuta wanafunzi - BBC Swahili - Habari
 
Back
Top Bottom