Nigeria: Wataalam wa Umoja wa Mataifa waitaka Nigeria kumuachilia huru jamaa asiyeamini kuwepo kwa Mungu

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Jopo la wataalam wa umoja wa mataifa limezitaka mamlaka nchini Nigeria kumuachilia huru mwanamume mmoja aliyekamatwa mwaka mmoja uliopita siku kama ya leo .

Mubarak Bala alikamatwa baada ya malalamishi kufikishwa katika kituo cha polisi katika jimbo la kaskazini mashariki la Kano kudai kwamba alikuwa amemfanyia kejeli mtume Mohammed kupitia ujumbe aliyoweka kwenye Facebook .

" Kukamatwa na kuzuiliwa kwa Bw. Bala sio tu ukiukaji wa haki zake za kimsingi lakini pia kunaathiri uhuru wa kimsingi nchini Nigeria'.Jopo hilo la umoja wa mataifa limesema kupitia taarifa .

Watalam hao wamesema wamefadhaishwa kwamba mamlaka za Nigeria hazikutii agizo la mahakama kuu disemba tarehe 21 mwaka jana la kumuachilia Bw. Bala

Mahakama ilikuwa imeagiza kwamba aachiliwe kwa dhamana na alipwe fidia ya ($650, £460) kwa sababu haki zake zilikiukwa

Kikao cha mahakama kilitarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu lakini hakikufanyika kwa sababu wafanyikazi wa idara ya mahakama wamegoma. Watalaam hao wa umoja wa mataifa wameitaka serikali kuhakikisha kwamba maamuzi ya mahakama yanaheshimiwa

Bwana Bala sio wa kwanza kujipata pabaya katika mkono wa sharia kuhusiana na imani kwani mwaka jana mwanamuziki Yahaya Sharif-Aminu, mwenye umri wa miaka 22 alihukumiwa kifungo cha kunyongwa kwa kulifanyia mzaha jina la mtume Mohammed .

Mahakama ya juu ya sheria ilimpata na kosa hilo katika jimbo la Kano baada ya wimbo mmoja aliyotunga kusambazwa kupitia Whatsapp mwezi machi mwaka huo .

Bwana Sharif-Aminu hakukana mashtaka hayo na alipewa fursa ya kukata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa .

Majimbo mengine kaskazini mwa Nigeria ambako kuna idadi kubwa ya waislamu yanatumia sheria za kawaida na zile za kiislamu -sharia .

Ni hukumu moja tu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya Nigeria ya sharia ilitekelezwa tangu sheria hizo zirejeshwe nchini humo mwaka wa 1999.
 
Kumbe serikali ya Nigeria ni ya hovyo hivi? Kwani kuamini au kutoamini katika Mungu unaihusu nini serikali kama siyo upumbavu wa jumla?
 
Wangemuliza Afande Sele na mashehe walioamini kwenye albadir vipi wamefikia wapi?
 
Ndo maisha ya sasa
Nadhani sisi waafrika tuna tatizo mahala,hivi bongo zetu walizichukua wagalatia na waquresh wa mecca Nini?
Yaani watu weusi bongo zao kama zimefungiwa kwenye makabati ya roma au zefungiwa pale kwenye kaaba haiwezekani umuhukumu mtu kisa tu haamini kitu ambacho hakijawahi onekana
Dini ni bangi zinazoleta ugonjwa hatari wa akili aisee!
😂😂😂😂
 
Nadhani sisi waafrika tuna tatizo mahala,hivi bongo zetu walizichukua wagalatia na waquresh wa mecca Nini?
Yaani watu weusi bongo zao kama zimefungiwa kwenye makabati ya roma au zefungiwa pale kwenye kaaba haiwezekani umuhukumu mtu kisa tu haamini kitu ambacho hakijawahi onekana
Dini ni bangi zinazoleta ugonjwa hatari wa akili aisee!
😂😂😂😂
Hata hatuelewi aliye ficha uwezo wetu wa kufikiri ni nani yaani hatuelewi chochote.
 
Back
Top Bottom