Nigeria: Wanafunzi Waislamu wamuua kwa mawe mwanafunzi mwenzao wakimtuhumu kumkashifu Mtume Muhammad

Status
Not open for further replies.

let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
3,264
7,815
Nigeria: Wanafunzi Waislamu wamuua kwa mawe mwanafunzi Mkristo wakimtuhumu kumkashifu Mtume Muhammad

Wanafunzi Waislamu katika mji wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Sokoto Alhamisi wamempiga mawe mwanafunzi Mkristo hadi kufa na kuchoma maiti yake baada ya kumshtumu mwanafunzi huyo wa kike kwamba alimkashifu Mtume Muhammad, polisi wamesema.

Darzeni ya wanafunzi wa chuo cha elimu cha Shehu Shagari walifanya vurugu baada ya mwanafunzi mwenzao Deborah Samuel kutoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo waliiona kuwa inamvunjia heshima Mtume Muhammad, msemaji wa polisi huko Sokoto Sanusi Abubakar amesema katika taarifa.

Wanafunzi walimuondoa kwa nguvu muathirika kwenye chumba cha usalama ambako alikuwa amefichwa na viongozi wa shule, wakamua na kuchoma jengo hilo, Abubakar amesema.

Abubakar amesema washukiwa wawili walikamatwa kufuatia tukio hilo.

Sokoto ni miongoni mwa darzeni ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria ambako sheria kali ya Kiislamu au Sharia inatekelezwa.

=====================

Kuna binti uko naijeria jana katiwa keberiti live na Mobu ya watu wa {}kwa Madai kuwa Kakufuru.
Atiku Abukakari kaingilia kati anataka haki itendeke waliojihusisha na mauaji ya Deborah wawajibishwe kisheria.

Then ona vile watu wa Dini walivyoreact



20220513_161623.jpg
 
Penye Dola ya kiislamu basi lazima iwepo mahakama na awepo kadhi(hakimu), kesi zinahukumiwa na kadhi kwa mujibu wa sheria za kiislamu, baada ya kuisikiliza kesi.

Hivyo kama muislamu atajichukilia sheria mkononi na kumhukumu mtu, basi atakuwa amevunja sheria hata kama aliyemhukumu ni kafiri.
 
Northern Nigeria sio mahali pa kukalika kama wewe ni mkristo. Katiba ya majimbo hayo yanafuata ' Shariah law' kama ile ya Islamic State. Wanapolisi wa Kidini wanaitwa Hisbah, ole wako wakupate unakula nguruwe ama unakunywa pombe hatakama wewe ni mkristo.
 
Habari iliyokamilka inasema Deborah alinunuliwa Dela baada ya kukufuru, ama?
Kwa mujibu wa "The Guardian"..

According to a source, “she was having an argument with some of her schoolmates over their ongoing examination and when she was asked how she managed to pass her exams, she said it was Jesus.

“She was asked to withdraw the statement and apologise, which she refused."

Baada ya kukataa kufuta hiyo kauli wakampiga mpaka akafa kisha kumchoma moto.
 
Kuna mambo watu wanachanganya.

Katika Quran kumetajwa madhambi makubwa na hukmu zake kwa mwenye kuyafanya, lakini hiyo haina maana basi muislamu yeyote anaweza kuhukumu kwa kuwa anajua hukumu hizo, hapana.

Hizo ni fujo na huo sio uislamu.

Hukumu za kiislamu zinatolewa na kadhi baada ya kusiliza kesi.

Hukumu ya mwizi ni kukatwa mkono, lakini sio Kila anayeitwa mwizi ni mwizi, na sio Kila kinachoibwa kinathamani na mwizi kukatwa mkono, hivyo sio Kila mwizi anakatwa mkono.

waliofanya hivyo, wamemkosea, na huo sio uislamu, ni wajinga.

Katika uislamu hakuna hukumu ya kuchoma moto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom