Nigeria na Tanzania ni nchi zitakazowekewa vikwazo vya usafiri na Marekani

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,568
Marekani ina mpango wa kuziongeza nchi nyingine saba zikiwemo Tanzania na Nigeria kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake wanatarajiwa kuwekewa vikwazo na vizingiti vya kuingia nchini humo.

Vyombo vya habari vya Marekani likiwemo gazeti la Wall Street Journal vimeripoti kuwa, mbali na Tanzania na Nigeria, nchi nyingine ambazo zinatarajiwa kuwekewa vikwazo vya usafiri na Washington ni pamoja na Sudan, Eritrea, Myanmar, Belarus na Kyrgyzstan.

Inaarifiwa kuwa, katika baadhi ya nchi hizo, viza za usafiri zinaweza zisifungiwe kabisa bali itakuwa vigumu kupatikana na kwa masharti, zikiwemo viza za biashara na za matembezi.

Maafisa wa utawala wa Rais Donald Trump wamesema bado orodha haijakamilika kwani mpaka Jumanne jioni Ikulu ilikua bado inajadili kuongeza au kupunguza nchi nyingine moja au mbili; ambapo pia nchi nyingine kwenye orodha hiyo zitafungiwa kushiriki bahati nasibu ya kupata uraia wa kudumu wa Marekani 'Green Card.'

Utawala wa Trump unadai kuwa, umechukua hatua hiyo kwa kuwa baadhi ya nchi katika orodha hiyo zinaongoza kwa raia wake kupitiliza muda wa kukaa Marekani kinyume na muda ulioanishwa kwenye viza zao.

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2017 Donald Trump alipiga marufuku raia kutoka katika nchi saba za Kiislamu kuingia nchini Marekani. Nchi hizo ni pamoja na Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.

Hata hivyo utawala wa Trump ulilazimika kuangalia upya orodha na hatua hiyo ya kibaguzi baada ya malalamiko ya jamii ya kimataifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom