sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,013
- 8,369
Hiii ni kweli kama umemaliza degree na huoni umuhimu wake we warudishie cheti wakupe ada uliyolipa ili uanzishe biashara.
===
Oludare Alaba; ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha LAUTECH cha nchini Nigeria akihitimu katika Kitivo cha Kilimo ambaye amezua mjadala mitandaoni baada ya kusambaa kwa video yake akizua kasheshe katika sehemu ya mapokezi ya chuo hicho.
Oludare alikuwa akirudisha cheti chake cha digrii katika chuo hicho ili arejeshewe pesa zote alizozitumia kama ada ya masomo yake.
Katika video hiyo, Oludare anaonekana akilalamika kwamba masomo aliyoyapata katika chuo hicho hayajamfaidi kivyovyote na ndiyo maana alitaka kurejeshewa ada yake.
Video hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti huku baadhi wakitumia misemo kumshauri kwamba mtu huwezi ukaila keki yako na bado ukataka kuwa nayo mkononi.
Baada ya video hiyo kusambaa, watu mbalimbali walimfikia na wengine kutaka kujua ni kwa nini aliamua kuchukua uamuzi kama huo wa kuzua kioja katika chuo chake cha awali.