Nifanyeje uridhike CHARTY Mpenzi?

Nifanyeje uridhike CHARTY Mpenzi?

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Chonde chonde niambie, nini unachokitaka,
Kingine nikufanyie, ambacho utaridhika,mpenzi wangu charty
Niambie nitulie, nimechoka kuteseka,
Nifanyeje uridhike, nambie basi nijue.

Ulitaka yako nyumba, nyumba nayo nikajenga,
Mkopo nikaubamba, wewe uache kupanga,
Ukakataa Kibamba, hutaki wala Ukonga,
Ukataka Mikocheni, nikakopa uridhike.

Nikasema njoo Mbeya, haraka ukakataa,
Ukadai ni kubaya, wataka kuishi Dar,
Nami nikasema haya, nikuridhishe haswaa,
Bado wataka Ulaya, Dar hapajakufaa.

Mara ukataka gari, huzitaki daladala,
Tena gari la fahari, hutaki hizo Corolla,
Nikuridhishe vizuri, nikaenda kopa hela,
Gari umeshalipata, wasema hujaridhika.

Nguo nzuri uzipate, likawa lako sharti,
Tena Mlimani City, vinginevyo varangati,
Kabidi nijikung’ute, ‘sije kukuudhi switi,
Nami pesa nikakopa, nguo uweze nunua.

Ukataka simu kali, bei yake milioni,
Tena ukataka mbili, zote ziwe iPhone,
Waijua yangu hali, lakini hatwelewani,
Simu hizo nimekupa, bado wataka vingine.

Ukataka iPad, laptop huitaki,
Nami nikajitahidi, nikakopa pesa benki,
Nikuridhishe waridi, moyoni ‘lotamalaki,
Wasema huna furaha, bado sana kuridhika.

Ndege ukataka panda, tena ya Lufthansa,
Eti unachokipenda, kutalii Ufaransa,
Moyo sasa wanidunda, utadhani nina kansa,
Sikai nikatulia, mahabuba huridhiki.

Nimefanya kila jambo, nadhani nakuridhisha,
Kumbe wafata mkumbo, wapo wanokufundisha,
Nateseka joto tumbo, mwenzangu unajirusha,
Nini zaidi nifanye, nawe uache nitesa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kibo10 naomba tuheshimiane, tusije tukafikishana mbali, hivi unajua hata bundle analotumia charty limelipiwa na nani?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kibo10 naomba tuheshimiane, tusije tukafikishana mbali, hivi unajua hata bundle analotumia charty limelipiwa na nani?
Shardcole kuna kitu kikubwa kimejificha hapa na nadhani si vema nifunguke hadharani hapa charty mwenyewe anajuwa hali yangu na majukumu yangu kwake!
 
Last edited by a moderator:
Mkomalie tu ila kama mdau alivyotanabahisha hapo juu kwamba msije kurudi kulee kwa Flora na Vicky (?)
 
Mkomalie tu ila kama mdau alivyotanabahisha hapo juu kwamba msije kurudi kulee kwa Flora na Vicky (?)

Hahaha Skype haitowezekana unajuwa mtoto wa kiume kubwaga moyo wote pwaaa..kama nilivyofanya mimi nimjuavyo charty ataupokea tu kwa mikono miwili!
 
Last edited by a moderator:
Hahaha Skype haitowezekana unajuwa mtoto wa kiume kubwaga moyo wote pwaaa..kama nilivyofanya mimi nimjuavyo charty ataupokea tu kwa mikono miwili!

Lakini tayari kuna mwanadamu anaitwa Shardcole kashatia neno hapo juu lakini naona umemjibu kiaina sasa sijui bado kuna usalama huko muendako?
 
Last edited by a moderator:
Lakini tayari kuna mwanadamu anaitwa Shardcole kashatia neno hapo juu lakini naona umemjibu kiaina sasa sijui bado kuna usalama huko muendako?

Rudi mtazame tena Shardcole amenyoosha mikono na kanitakia kila la kheri!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom