Nifanyeje mpenzi wangu arudi?

Nifanyeje mpenzi wangu arudi?

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
381
Peoplee,

Natumaini nyote mu wazima wa afya. Ninawasalimu wote.

Ndugu zangu, ninakuja hapa kuomba msaada. Najua wapo watakaonibeza kwa maneno ya kashfa lakini inapaswa mtambue kuwa nina shida.Mimi ni mwanamke mwenye mpenzi wa muda mrefu sasa miaka mitatu imepita.

Miaka miwili iliyopita mwenzangu alinipenda sana na kunijali.Baada ya muda huo, bahati mbaya sana mpenzi wangu alikorofishana na kaka yangu ambapo kaka yangu alimwambia kuwa hatumii akili. Chanzo cha ugomvi wao ni kutaka kunitoa mimi out wakati nikiwa mgonjwa ambapo ni mimi niliyeomba kutolewa.

Kaka zangu hawajui juu ya uhusiano wetu zaidi ya urafiki wa kawaida.Ugomvi huo mwenzangu ameuweka moyoni na kumuharibu kabisa akili yake.Kila siku tunagombana, yale mapenzi tena yamepungua na kubaki 000.5 percent.Tulipokaa chini kuongelea hilo alinijibu kuwa yeye atasuluhisha na kila kitu kitakuwa sawa.

Tumekaa zaidi ya mwezi sasa na hali inazidi kuwa mbaya zaidi. Binafsi sitaki kusikia hata swala la kuachana nae bali nahitaji kutatua tatizo ili hizo chuki juu yangu ambazo si za msingi ziondoke kabisa. Ameniruhusu mimi nitafute suluhu lakini sijui wapi pa kuanzia mbali na kuwapatanisha yeye na kaka zangu. Ni jambo la siku moja tu.
Mbali na hilo kipi nifanye ili aweze kurudi kuwa kama zamani?

Naombeni mnisaidie wanasaikolojia mliopo humu tafadhalini sana
 
Mtambulishe full stopu.

Nilikuwaga najua wewe Me. Jamani muwe mnatanabaisha kama wewe ni K au M.
Tuko radhi kutambulishana lakini hii ugomvi umeleta madhara makubwa kwetu. Unamtambulisha mtu ambaye ana furaha nawe. Lakini huyu siku hiz ni hasira tu. Tukimaliza hili tu process za ndoa zitafuata. Ila nikishindwa inanipasa niachane nae tu aendelee kutafuta wengine.
 
Mbn naiona insh ndg san wew ndo unaikuza watambulishe bas
 
True love also die because of this day
 
Niambie nini cha kufanya. Maana nimeanza kumpa tizi za salamu mpk basi ili siku nisipotuma animiss. Sa sijui nakosea
Hiyo nayo ni mbinu ila tafuta kitu anachopenda ukifanye maybe itasaidia find the most one and do it
 
Ni swala la kuongea nae kwanza, halafu uongee na hao kaka zako. Mwisho kabisaa wakutanishe wote wapatane halafu fanya utambulisho. Tumia nafasi yako kama mwanamke kudumisha amani, upendo na mshikamano
 
Hilo neno"Hutumii akili" ni dharau kubwa,pengine wamesema hivyo na kusindikiza na maneno mengine ya shombo!,waeleze ukweli kaka zako mahusiano yenu na jinsi unavyomuhitaji huyo jamaa,waeleze kinagaubaga jinsi jamaa yako alivyokerwa na kujisikia unyonge kwa maneno yao ya hovyo ya siku ile kama wana busara watamuita mchizi na kumaliza sitofahamu iliyopo...
 
Hongera kwa kiomba ushauri kwani huu ni uamuzi sahihi, nami naomba nichangie kadili ya maelezo yako.

Lakini kwenye andiko lako hujatuambia umri wako na wake. Katika maisha yangu ya kutoa ushauri Mara nyingi nazingatia sana umri,kwasababu kuna baadhi ya ishu huwa ni za utoto tu. Mfano hii ya jamaa yako kuzira baada ya kuambiwa hatumii akiri. But ngoja nichangie kidogo.

Inaonekana kuna sintofahamu kati ya ndugu zako na huyo jamaa, kinachosababisha huo mgogoro ni huo urafiki wenu. Wao wanakilinda wewe kama ndugu yao,na kwasababu ulimtambulisha kwao ni rafiki basi nao wantreat kama rafiki yako na ndio maana ni wakali ili kukulinda. Ungewaambia ukweli toka mwanzo labda ungepunguza na kuondoa sintofaham hii.

Mchumba wako alijiegesha kwa uzi wa buibui. Kunakitu kinaendelea kati yenu ambacho kinamkera mmoja wenu, hivyo huyo mchumba wako alikuwa anatafuta kijisababu cha kuharibu uhusiano wenu. Baadhi ya sababu ninazo fikiri kuwa ni chanzo cha hayo ni

A. Labda ulimwambia no kufanya mapenzi mpaka ndoa,

B. Hujiwezi uwanjani na amekuchoka

C. Umepoteza mvuto kwake,

D. Kampata mwingine na alitaka apate kanafasi ka kuvunjia uhusiano

E. Huenda alichokitaka kesha pata na hana hamu na wewe

F. Huenda nyie wote ni watoto ndio maana mnazira kwa ishu za kijinga tu. Rejea sababu maelezo yako, eti kuambiwa atumie akiri anazira hahahahahaha

G. Labda alipigwa biti na kaka zako juu yako na kutishiwa kutekwa na kuteswa kama akiendelea kuwa nawe

Possibilities hizo ni zangu tu kwani ni siri yenu wewe na yeye. Lakini nimejikita huko kwasababu ishu iliyopelekea tatizo hili ni dogo sana kwenye ulimwengu wa mapenzi. Yaani mtu uambiwe hutumii akiri ndio ususe!! Watu wanapigwa,wanatukanwa,wanafanyiwa figisu za kila aina bado wana kaza tu.

Yakufanya kwasasa

1: Kaa nae na umwambie atoe suluhisho mapema ili kama uhusiano umefika mwisho ukajua kabisaa

2:Rasmisha mahusiano yenu hata kwa baadhi ya ndugu km mashangazi au bibi kwa pande zote. Akikataa vunja mahusiano

3: Waeleze kaka zako uhusiano wenu nje ya urafiki,ila kama wewe ni mwanafunzi pole yako.

4: Wakutanishe kaka zako na huyo jamaa ili kusuruhisha ugomvi wenu

5: Vaa moyo wa ujasiri na uwe na moyo wa kufanya maamuzi magumu ikibidi,maana huyo jamaa si salama kwa maisha yenu ya ndoa kwa baadae.

6: Jaribu kuwa karibu na mwenzi wako na kumfariji, huenda akakupa sababu ya yeye kubadirika.

Akikataa jua hiyo sababu ya kuvunja mahusiano yenu.

Binafsi nimeishia hapo
 
Peopleeeeeeeeeeeeee
Natumaini nyote mu wazima wa afya. Ninawasalimu wote.
Ndugu zangu, ninakuja hapa kuomba msaada. Najua wapo watakaonibeza kwa maneno ya kashfa lakini inapaswa mtambue kuwa nina shida.
Mimi ni mwanamke mwenye mpenzi wa muda mrefu sasa miaka mitatu imepita.
Miaka miwili iliyopita mwenzangu alinipenda sana na kunijali.
Baada ya muda huo, bahati mbaya sana mpenzi wangu alikorofishana na kaka yangu ambapo kaka yangu alimwambia kuwa hatumii akili.
Chanzo cha ugomvi wao ni kutaka kunitoa mimi out wakati nikiwa mgonjwa ambapo ni mimi niliyeomba kutolewa. Kaka zangu hawajui juu ya uhusiano wetu zaidi ya urafiki wa kawaida.
Ugomvi huo mwenzangu ameuweka moyoni na kumuharibu kabisa akili yake. Kila siku tunagombana, yale mapenzi tena yamepungua na kubaki 000.5 percent.
Tulipokaa chini kuongelea hilo alinijibu kuwa yeye atasuluhisha na kila kitu kitakuwa sawa.
Tumekaa zaidi ya mwezi sasa na hali inazidi kuwa mbaya zaidi. Binafsi sitaki kusikia hata swala la kuachana nae bali nahitaji kutatua tatizo ili hizo chuki juu yangu ambazo si za msingi ziondoke kabisa.
Ameniruhusu mimi nitafute suluhu lakini sijui wapi pa kuanzia mbali na kuwapatanisha yeye na kaka zangu. Ni jambo la siku moja tu.
Mbali na hilo kipi nifanye ili aweze kurudi kuwa kama zamani? Naombeni mnisaidie wanasaikolojia mliopo humu tafadhalini sana
Je ni hilo tu? Usikute kaka zako walishamfata kwa kisa kingine, jamaa asemi. Anyway, kwanini usimtambulishe? Kwa sababu mimi nitaongea na marafiki zake Dada yangu tofauti na shemeji yangu. Shemeji atakuwa na value fulani hivi. Ingekuwa kaka zako wanajua yeye ni nani, maybe wasinge badilishana lugha mbaya.

Huyo jamaa yako namsoma. Maana kaka(familia) zako ni fence. Mahusiano yenu ni nyumba. Kama familia ya babe wako haikupendi, hapo chomoa tu. Trust me. My mom na ndugu zake father hawapatani kivile. Naijua shida mama aliyoipataga.

Conclusion:
Fanya mpango umwambie jamaa wewe ndio uta suluhisha. Mpeleke home, waite kaka zako, waambie who he is to you. Waombe msamaa since utawaambia the whole situation. Kama kaka zako wana hekima, wataomba msamaa. Na everything will be good. Hata ingekuwa mimi, sipatani na mashemeji zangu, ningesepa kiroho safi. Maana hao ndo walinzi wenu. Kama hazipandi ujue mbele kubaya. Take my advice, build back their relationship. Introduce him as your boyfriend. Everything will be good.

-callmeGhost
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom