Kitambulisho cha taifa na faida ya kusajili laini za simu

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Desemba 27, mwaka jana, Rais John Magufuli akiwa mjini Chato katika Mkoa wa Geita, alifanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole huku akiwataka Watanzania wote kukamilisha mchakato huo, kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Baada ya kusajili laini yake, alitangaza kuongeza muda wa siku 20 za usajili huo kuanzia Januari 1, 2020 hadi Januari 20, 2020, badala ya ukomo uliokuwa umetangazwa kuwa ni Desemba 31, 2019.

Rais Magufuli alifikia hatua yake kutokana na huruma kwa watanzania, baada ya kuona kuwa upo uhalisia kuwa wengi licha ya kutaka, lakini walishindwa kufanya usajili huo katika muda uliokuwa unamalizika kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wengine kuugua na wengine kutokuwa wamekamilisha upataji wa namba ama Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Talfa (NIDA).

Aliwataka Watanzania hao kutumla vizuri muda wa nyongeza kwani utakapoishia, hakuna kisingizio kitakachokubalika ndiyo maana hapo hapo, alilagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanla (TCRA) kuhakikisha laini ambazo hazitasajiliwa hadi Januari 20, zinazimwa. Hata hivyo, bado watu wanaendelea kuhangaika huku na huko kutafuta namba au vitambulisho hivyo, na wanaendela kupata ingawa wengine kutokana na mahitaji ya kupata kitambulisho hicho, 'hawajul watoke' vipi.

Aprili 23, 2019, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alisema mfumo mpya wa usajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole haulengi kuwazula wananchi kutumla laini zaidi ya moja, bali unakusaidia kudhibiti utitiri wa laini za simu na uhalifu wa mtandao. Mfumo wa kusajili laini kwa kutumia laini za vidole (Biometric Registration) ulizinduliwa Machi 1, 2018 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kuwapo vitendo vya watumiaji wa huduma hiyo kughushi vitambulisho au kutumia vitambulisho vya watu wengine.

Akiwa bungeni Dodoma, alimwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuruhusu watoa huduma za simu za mkononi kupeleka madawati maalumu ili kuwezesha wabunge kufanya usajill wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. TCRA wanatekeleza mfumo huo kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) ambapo utasaidia kupata takwimu sahihi za watumiaji wa simu za makononi na huduma za fesha kwa ajili ya kuweka mipango zaaa ya kuendeleza sekta na uchumi wa Taifa.

FAIDA ZA KUSAJILI SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE

Rais Magufuli anasema miongoni mwa falda za kusajili laini za simu kwa alama za vidole kuwa ni pamoja na usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu. Kwa mujibu wa uchunguzi, miongoni mwa njla wanazotumia matapeli na aliyoidokeza rais, ni pamoja na kulaghai watu kuwa kuna tatizo hasa kifo au ugonjwa wa ghafla hivyo, kumtaka mtu atume fedha il wamsaldie wanayedai ni mwathirika hasa watoto wa shule. Uchunguzi umebalni kuwa, matapeli wengine hutuma ujumbe kwa watu ukisema: "Ile pesa tuma kwa namba hli na litakuja jina.."

Hata hivyo, licha ya matapeli na wahalifu wengi wa kutumia simu kukamatwa na vyombo vya dola, bado wameendelea kusababisha usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha. Ifahamike kuwa, kupuuza kazi ya usajili wa laini za simu, itasababisha wahusika kukatiwa mawasiliano na hivyo, kujikuta wamejitenga na jamii inayowazunguka wakiwamo ndugu, jamaa, marafikl na wateja wa kazi au bishara.

KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Kwa mujibu wa NIDA, wanaosajiliwa na kupata vitambulisho hivyo sambamba na alama za utambulisho wa utalfa, ni watu wote wenye umri kuanzia miaka 18, raia wa Tanzania na wageni wanaoishi kihalali nchini.

Kwa mujibu wa NIDA, fomu za kujisajili zinapatikana kwa mwajiri, ofisi ya Serikali ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya NIDA. Hakikisha umejaza fomu hiyo vipengele vyote kwa kalamu nyeusi na kuweka viambatanisho muhimu vitakavyokutambulisha umri, makazi na uraia. Uchunguzi wa makala haya umebaini kuwa, awali watu wengi hawakuzingatia faida za kuwa na kitambulisho cha taifa ndiyo maana sasa wanapata tabu kwa mtindo wa zimamoto ili wawezeshe simu zao kutozimwa,

Hata hivyo, mbali na kuwezesha kukamilisha usajili wa laini za simu ambao kitambulisho cha taifa ni hitaji kuu, zipo faida nyingi za vitambulisho hivi. Hizo ni pamoja na kuchochea usalama na amani kwa maendeleo ya kljamii na kluchumi ya taifa. NIDA hutoa vitambulisho vya aina tatu ambavyo ni vitambulisho vya uraia, vitambulisho kwa wageni wakazi na vitambulisho vya ukimbizi. Lengo kubwa la kutoa vitambulisho vyote hivi ni li kuweza kufahamu watu wanaolshi nchini kihalali.

Falda nyingine zitokanazo na kuwa na kitambullsho cha urala/ ukazi au ukimbizl ni pamoja na kutumika kuongeza wigo wa mapato ya Serikali, kusaidia kumtambua mhusika kirahisl anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya; pamoja na kurahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki na asasi mbalimball za fedha nchini.

Nyingine ni kusaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki, kuwezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyingine kwa kutumia majina tofauti, kufanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa Tanzania anastahili kupata kirahisi, kwani kupltia kitambulisho mtu atatambulika kirahisi kwamba nani ni nani; yuko wapi na anafanya nini katika taifa.

Imebainika pia kuwa vitambulisho hivi ni muhimu kwani vitasaidia kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya Serikali, vitaimarisha utendaji kazi serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostaafu, vitarahisisha kazi ya kuhesabu watu (sensa) na vitarahisisha kazi ya kuhuisha daftari la wapiga kura, ambayo kwa sasa hufanyika mara mbill kabla ya uchaguzi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli hivi vitambukisho vinao umuhimu mkubwa ila tatizo serikali haikujipanga kabisa kuvitoa kwa wakati
 
Back
Top Bottom