Kitabibu, miezi 6 bado siyo tatizo. Itachukuliwa kama tatizo iwapo baada ya mwaka 1 wa ngono bila kinga hakutakuwa na ujauzito. Kwa sasa hata ukienda hospitali km daktari anaijua kazi yake vizuri atawarudisha mkaendelee tu na mchezo mpaka mwaka uishe. Kama una wasiwasi na hali yako kwa sababu yoyote ile unayoijua, wahi kupima mwenyewe. Ni rahisi sana kumpima mwanaume kuliko mwanamke.
Fahamu mzunguko wa mwezi wa mwenzi wako. Kama uko regular (haubadiliki badiliki kila mwezi) basi ni rahisi kupata ujauzito (km nyote hamna tatizo). Akiingia mwezini, anza kumhesabia. Siku ya kwaza ya mwezi (kutoka damu) iwe 1, siku ya pili iwe 2, hesabu hivyo hivyo hata baada ya kutoka. Hata akitoka, endelea kuhesabu mpaka siku anaingia tena. Akiingia tena unaanza kuhesabu 1. Mzunguko wake kwa mwezi huo utakuwa siku zote ulizohesabu kuanzia siku ya 1 mpaka siku 1 kabla ya kuingia tena mwezini. Kwa shemeji yako hapa huwa ni siku 28. Kwa huyo wa kwako inaweza kuwa tofauti. Mhesabie tena mwezi wa pili, wa tatu, nk. Kama mzunguko wake ni regular hesabu yako itakuwa ni siku zile zile kila mwezi. Kwa shemeji yako hapa ni hiyo hiyo 28.
Sikiliza sasa jinsi ya kumpa ujauzito. Wanawake hutoa yai siku 14 kabla ya kuingia mwezini. Kama mwanamke ana mzunguko regular ni rahisi kujua hiyo siku ya 14 katika mzunguko. Wa kwangu mzunguko wake ni siku 28. Kwa hiyo siku ya 14 baada ya siku ya kwanza kwenda mwezini najua yai lake litakuwa tayari. Lakini kumbuka mbegu za kiume zinakuwa hai ktk mwili wa mwanamke hadi siku 3. Kwa maana hiyo hata ukiziweka ktk mwili wake siku 3 kabla ya yai kutelemka, bado kuna uwezekano wa kumpa ujauzito. Na yai nalo linadumu ktk mwili wa mwanamke hadi siku 3 hizi. Kwa hiyo siku zenye uwezekano wa ujauzito ni 7 katika mzunguko wa mwakamke. Siku 3 kabla ya siku ya yai kushuka, siku 1 ya yai kushuka na siku 3 baada ya kushuka. Ukiweka mbegu zako mwanzoni mwanzoni mwa siku hizo 7, uwezekano mkubwa ni mtoto wa kike. Ukiweka mwishoni mwisho, uwezekano mkubwa ni wa kiume. Mbegu ya X (ke) hutembea taratibu lakini haifi haraka. Mbegu ya Y (me) inakimbia haraka, kuchoka na kufa haraka.
Njia ya uhakika ya kujua km mkeo yuko tayari ni kutumia ovulation kit. Zinauzwa katika pharmacy lakini sina uhakika kama pharmacy za Bongo zipo. Inapima kwa njia ya mkojo na unaweza kuifanyia nyumbani wewe mwenyewe. Iko kama kipimo cha UKIMWI cha nyumbani. Ina maelekezo mazuri (kwa Kiingereza) ya jinsi ya kuitumia na kujua majibu yanapokuwa positive ama negative. Ikiwa positive unaweka mbegu siku hiyo ndani yake. Kwa sababu itakuwa gharama kupima kila siku katika mzunguko, inabidi ukisie siku zile za katikati katika siku zile 7 "hatari" ili upime mara 2-3 hivi na kupata majibu chanya.
Kuna watu wamesema fanya ngono naye kila siku. Hilo ni kosa. Mbegu kama zilivyo za mahindi, zinahitaji muda kukomaa. Kufanya ngono kila siku kunaweza kuwa na matokeo hasi kwa mtu anayetafuta mtoto.