Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

Hapo juu nimekusoma kwamba baada ya wewe kuzaliwa aliambiwa (istoshe niliambiwa kwamba nilipozaliwa aliambiwa ila kwasabau ya system ya jeshi ya wakati huo hakuweza kusema juu ya hatma yangu, so alimwacha mama kwenye wakati mgumu sana na hapo ndipo walipopotezana kimawasiliano) sasa kama ni kweli walipotezana kimawasiliano kwa maoni yangu Baba mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae angehangaika huku na kule kumtafuta mama ili kujua mwanae anaendeleaje maana ni miaka mingi imekatika hata kama system ya jeshi ilikuwa ngumu bado angeweza kumtafuta mama ili kujua hali ya mtoto wake. Kuwa makini sana kama unataka kuendelea na hili maana unaweza kuwaumiza watu wengi sana ukiwemo wewe mwenyewe.

Anza kwa simu kwanza kama unaweza kupata namba ya simu ya ofisini kwake ujitambulishe uone mwelekeo wake. Kama hukuridhika na maongezi yenu ya simu basi achana naye.

rafiki yanu mpenzi thanks a lot.

kuhusu ishu ya yy kuwa mzito naenda kutafuta unafuu labda ajishuku tu manake ukweli sina shida kiviile ya maisha na si kwangu tu hata kwa wanangu najimudu kimtindo.
nafsi yanu sijui kwann inaniimbia sana juu ya kumtafuta huyu baba, mpaka nakosa amani kabisa lkn naogopa sana nisije nikamuudhi baba mlezi na mama yangu. Lkn nafikir kuna sababu za yy baba mzazi kujua kwamba mm ni mwanae ama unasemaje hapo??[/QUOTE]
 
Duh! Kama yote hayo ni ya kweli basi pole sana. Pia naielewa kiu ya nafsi yako kutaka walau kujua zaidi juu yake na yeye kujua juu yako.

Kama una njia ya kuwasiliana naye mimi sioni ubaya wowote ukiamua kumtafuta kwa lengo la kujuana zaidi. Ila nadhani pia itakuwa ni busara kama ukianza kulonga na bi mkubwa kwanza umsikize naye maoni yake kuhusu hicho kiu chako. Na itakuwa vizuri zaidi ukipata maoni ya baba mlezi pia naye umsikie.

Kama unaweza kuanza na bi mkubwa basi anza naye yeye kwanza. Yeye anaweza pia akawa kiungo muhimu kwa baba mlezi katika kupoza hali ya hewa.

Baada ya kusikia maoni yao nadhani utakuwa na wewe umeshapata ramani ya jinsi mwelekeo mzima utakavyokuwa.

dah!! hakya mama tena.............. sasa nikimwambia mama yangu mzazi akigoma ndo iwe basi sio?? manake kumweleza baba hili siwez abadani nitamuumiza sana mzee wa watu ambaye hata jina alinipa lake.
 
swali zuri sana hili.
bada ya kuambiwa na watu nikachunguza kwa mama nikakuta ni kweli ingawa mama hakuniambia yy.
niliambiwa na mdogo wake na mama (ma'mdogo) ukweli na alinionyesha hadi picha ya baba ambazo walipiga na mama wakati wako na uhusiano. kutoka hapo nikaanza kuangalia nilivyosadifu na ndugu zangu nikagundua kuna utofauti mkubwa sana.

lkn pia nilipochukulia tarehe ya mama kufunga ndoa na niliyozaliwa iliacha gap kubwa sana na niliwah kuisoma kadi ya mama ya kliniki akiwa na mimba yangu iliandika jina la huyu baba mzazi. sijawah kumwambia mama hili manake niliiona kwa bahati mbaya tu kabatini mwake.

istoshe niliambiwa kwamba nilipozaliwa aliambiwa ila kwasabau ya system ya jeshi ya wakati huo hakuweza kusema juu ya hatma yangu, so alimwacha mama kwenye wakati mgumu sana na hapo ndipo walipopotezana kimawasiliano.

kam unahisi utamuhuzunisha baba mlezi achana na mpango ulionao halafu nashangaa huyo baba mzazi mpaka wakati huu hakumbuki kuwa aliacha mtoto hata angeanza kukutafuta kama mwanae kapiga kimyaaa. achana nae ndugu waswahili wasema mpende akupendae asiyekupenda.......! piga kimya kwani maishabila yeye yaliwezekana na yatawezekana milele
 
Hapo juu nimekusoma kwamba baada ya wewe kuzaliwa aliambiwa (istoshe niliambiwa kwamba nilipozaliwa aliambiwa ila kwasabau ya system ya jeshi ya wakati huo hakuweza kusema juu ya hatma yangu, so alimwacha mama kwenye wakati mgumu sana na hapo ndipo walipopotezana kimawasiliano) sasa kama ni kweli walipotezana kimawasiliano kwa maoni yangu Baba mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae angehangaika huku na kule kumtafuta mama ili kujua mwanae anaendeleaje maana ni miaka mingi imekatika hata kama system ya jeshi ilikuwa ngumu bado angeweza kumtafuta mama ili kujua hali ya mtoto wake. Kuwa makini sana kama unataka kuendelea na hili maana unaweza kuwaumiza watu wengi sana ukiwemo wewe mwenyewe.

Anza kwa simu kwanza kama unaweza kupata namba ya simu ya ofisini kwake ujitambulishe uone mwelekeo wake. Kama hukuridhika na maongezi yenu ya simu basi achana naye.

rafiki yanu mpenzi thanks a lot.

kuhusu ishu ya yy kuwa mzito naenda kutafuta unafuu labda ajishuku tu manake ukweli sina shida kiviile ya maisha na si kwangu tu hata kwa wanangu najimudu kimtindo.
nafsi yanu sijui kwann inaniimbia sana juu ya kumtafuta huyu baba, mpaka nakosa amani kabisa lkn naogopa sana nisije nikamuudhi baba mlezi na mama yangu. Lkn nafikir kuna sababu za yy baba mzazi kujua kwamba mm ni mwanae ama unasemaje hapo??[/QUOTE]

dah!! ngoja kwanza nifuate ushauri huu nipime kwanza kina cha maji nione kikoje.
 
Wewe kwanza huna uhakika kama kweli huyo baba yako umesikia kutoka kwa wambea maana wa kuthibitisha hilo ni mama yako, pili huna tatzo lolote umeolewa na una elimu yako na maisha yanaenda sawa, swali unafikriri huyo mheshimiwa akijua kuwa wewe ni mwanae utafaidika nini? atakuuliza ulikuwa wapi mpaka umeona amekuwa waziri.... kama mama yako angeona kuana umuhimu wa kukuonyesha baba yako angekuwa amekuonyesha, suala la kufanana ni waswahili wananogesha mambo yawezekana hata huyo siyo baba yako... Ushauri wangu so long as umepata malezi bora bila kuwepo huyo baba mpaka hapo ulipofika huna haja ya kuanza kuhangaika tulia na mume wako mpende saana pia zidisha mapenz kwa mama yako over!.....
nakubaliana na wewe kabisa kwa hili.
tatizo ni kwamba myo wangu ndio unaoumia tu kwamba nataka tu ajue kwamba ana mtoto mkubwa kama alimwacha kwa makusudi ama bahati mbaya basi atajua kwamba nina ishi. sitaki kitu kwake wala hata jina sitaki manake ninalotumia halijawah kuwa disgrace kwangu ila tu nataka kutua mzigo uloko kifuani mwangu.
 
dah!! hakya mama tena.............. sasa nikimwambia mama yangu mzazi akigoma ndo iwe basi sio?? manake kumweleza baba hili siwez abadani nitamuumiza sana mzee wa watu ambaye hata jina alinipa lake.

Mimi nadhani ni vyema kumhusisha mama kwa namna fulani. Kwa nini ufanye siri? Kwani unachotaka kufanya ni kibaya sana hadi mama asijue? Na huoni kwamba ukifanya nyuma ya mgongo wake ni sawa na kumsaliti?

Kwangu ni afadhali upate maoni yake na akatae kuliko wewe kufanya nyuma ya mgongo wake.
 
Watoto wakike kwanini mna hila jamani eee?
Huko kupepesa mapaka ukajua huyo anaekulea sio babayako haijakutosha
sasa umeamua kumuendea huyo uliyoambiwa ni baba yako.
Una uhakika gani na hayo maneno?
Na kwanini usitafute utaratibu wa kumuuliza mama yako kwanza?

mimi ni mama ninachoamini ni hivi anayejua ukweli kuhusu mtoto ni wanani haswa huwa ni mama mwenyewe nasio baba ingekuwa umepewa go ahead na mamayako ningekusapoti sana ila ni maneno ya mtaani au kwa vile umeshajua ni kiongozi eee?:disapointed:

mbona sio ishu kujua kama huyu ni baba ama sio?? na pia simtafuti kisa ni kiongozi manake kwa miaka alokaa naje na mapaka kurudi kuwa kiongozi ningebabaika kumtafuta. leo hii sitak hata jina lake manake nililonalo halijawah kuwa disgrace kwangu lkn nataman ajue kwamba ule mtoto alomwacha yupo anaishi. je hilo ni kosa??
 
Sidhani katika muda na wakati kama huu,unahitaji kitu chochote kutoka kwa huyo waziri sijui.Ila ninachoona wewe unahitaji ukamilifu tu,ambao katika umri ulionao hautakusaidia sana.Hili suala ni zito na laweza kuwa tofauti na mategemeo yako,labda la kujiuliza mpaka leo,ni kiti gani kilichosababisha huyo baba asikutafute?!.Nina imani baba mlezi anaujua ukweli lakini hakutaka kuharibu.Itakuwa si vema nawe umuharibie katika kipindi hiki baada ya kukua na kujitambua na kuota mapembe.The one million dollar question is,what will be the reaction,and how u gonna solve it??!!
 
Mimi nadhani ni vyema kumhusisha mama kwa namna fulani. Kwa nini ufanye siri? Kwani unachotaka kufanya ni kibaya sana hadi mama asijue? Na huoni kwamba ukifanya nyuma ya mgongo wake ni sawa na kumsaliti?

Kwangu ni afadhali upate maoni yake na akatae kuliko wewe kufanya nyuma ya mgongo wake.

ahsante sana kwa mawazo na ushauri mzuri kama huu.
 
Pole sana gfsonwin, mie kwa maoni yangu achana naye huyo. Ataona kwa kuwa unajua ni mtu mzito ndani ya Serikali basi unatafuta mali toka kwake kitu ambacho kinaweza kisiwe na ukweli wowote. Pia anaweza kukukana kabisa na hiyo kukuumiza zaidi na pia Baba aliyekulea pia inaweza kumuumiza kwa kuona kwamba pamoja na jitihada zake zote za kukulea kama mwanae toka uzaliwe hadi sasa umekuwa mtu mzima bado humkubali kama ni Baba yako wa kweli.

sista gfsonwin ushauri wangu na mimi ni huu hapa naona BAK kanisemea
 
Last edited by a moderator:
Sidhani katika muda na wakati kama huu,unahitaji kitu chochote kutoka kwa huyo waziri sijui.Ila ninachoona wewe unahitaji ukamilifu tu,ambao katika umri ulionao hautakusaidia sana.Hili suala ni zito na laweza kuwa tofauti na mategemeo yako,labda la kujiuliza mpaka leo,ni kiti gani kilichosababisha huyo baba asikutafute?!.Nina imani baba mlezi anaujua ukweli lakini hakutaka kuharibu.Itakuwa si vema nawe umuharibie katika kipindi hiki baada ya kukua na kujitambua na kuota mapembe.The one million dollar question is,what will be the reaction,and how u gonna save it??!!

hapo bold ndipo ambapo pananipa hofu kabisa
 
kam unahisi utamuhuzunisha baba mlezi achana na mpango ulionao halafu nashangaa huyo baba mzazi mpaka wakati huu hakumbuki kuwa aliacha mtoto hata angeanza kukutafuta kama mwanae kapiga kimyaaa. achana nae ndugu waswahili wasema mpende akupendae asiyekupenda.......! piga kimya kwani maishabila yeye yaliwezekana na yatawezekana milele
thanks mkuu...................ila kweli manake mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba.
 
Hapa kuna tatizo kubwa sana kati ya mama yako na baba yako wa kibaiolojia

Huenda ndo maana hakuambii ukweli

Ila hiyo excuse ya jeshi hainiingii akilini

Kama najua ana mtoto kwanini asiulizie?

Mpaka leo yuko jeshini?

Au zile system sipo mpaka leo?
sio kwamba ile system inaendelea mpaka leo. lkn sasa nilifikiri kwamba alishindwa kuwasiliana na mama may be kwasababua ya mawasiliano t. hata hivyo siwez kumsemea sana lkn tu nilihitaj na mm kuwa mkamilifu basi
 
Mimi nadhani ni vyema kumhusisha mama kwa namna fulani. Kwa nini ufanye siri? Kwani unachotaka kufanya ni kibaya sana hadi mama asijue? Na huoni kwamba ukifanya nyuma ya mgongo wake ni sawa na kumsaliti?

Kwangu ni afadhali upate maoni yake na akatae kuliko wewe kufanya nyuma ya mgongo wake.

Aisee mkuu nina experience na similar case, mama aliumia sana sana sana na yet hakumpa mtoto go ahead ya kumtafuta huyo baba, tena akamwambia wazi ,ukifanya hivyo mimi na wewe basi'. Ilibidi mtoto afyate mkia, uzuri ni mkubwa na anaishi kivyake kama sista gfsonwin

Binafsi I strongly disagree with what she plans to do. Frankly speaking, uhusiano wake na mama yake na baba aliyemlea hautakuwa mzuri akisha fanya hivyo!
 
Last edited by a moderator:
Ongea na mama, ongea na baba mlezi. Waambie dhamira yako na uwaambie sababu hasa ya wewe kutaka kumfahamu baba mzazi.. Pia uwaahidi kuwa hutobadilika hata kama utagundua kuwa baba yako mzazi... Najua kuwa unao uwezo wa kukaa nao na ukawaambia wakakuelewa vizuri sana..

Pia ujaribu kuwashirikisha kaka na dada zako ambao mmechangia Mama.. Waambie kuwa hauna dhamira mbaya.

Usijaribu kufanya jambo hlo kwa kificho tafadhali. Unaweza kuanzisha migogoro na chuki ambazo si nzuri..

Najua ukimwambia mama kabla kabla hujafanya ulichoamua ataweza kuumia ila itakuwa mbaya zaidi pale ambapo utamficha halafu agundue mwenyewe.
 
Back
Top Bottom