NewDawnTz
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 1,667
- 362
Japo bado sijaona njia nyeupe na sahihi zaidi, NINA KILA SABABU YA KUWASHUKURU WANA JF mliotoa mawazo yenu juu ya nini nifanye kuhusiana na suala zima la dogo kama nilivyoandika hapa chini.
Baada ya kumtext dogo na kumwambia tunaheshimu uamuzi wake na niko tayari kumsikiliza na kumuelewa bila kumu-offend amenitafuta na nimeongea nae kwa muda mrefu sana.
Alichoniambia ni kwamba alifanya uamuzi huo binafsi kwani alifikia mahali kutambua kuwa hawezi kukaa nae tena na lijiona kumpenda zaidi huyu mwingine waliesoma nae chuo.
Ukweli ni kwamba dogo is like he doesn't care juu ya mwenzake aliemuacha mwanza. Ni kama anacheza mchezo Fulani wa kuigiza mpaka nikahisi au HILI TOTO LIMELOGWA NINI. Eti ananiambia alishindwa tu kumuacha na kumwambia hamtaki kwa sababu tayari alishampa mimba na hivyo amekubaliana na mke wake mpya kuwa aendelee kukaa nae kwa muda mpaka apone kidonda kasha amuambie kuwa ameoa mwanamke mwingine na hivyo hana mpango wa kukaa nae ila amuachie tu mtoto aendelee kutunza yeye akaendelee na mipango mingine ya maisha.
Pia anasema aliamua kutokututaarifu sisi wala wazazi wake kwa sababu anasema tungemtibulia na mpango wake ni kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ndio ataweka wazi kwa kila mtu juu ya uamuzi wake. Mawazo yake itakuwa siri kama anavyotaka kichwani mwaka huku akisahau kuwa mama yake yuko kwenye constant contact na wazazi wa binti. Ndo maana nasema limelogwa hili toto.
Kwa ushauri wenu nimeonelea nimtume tu mke wangu week hii akamchukue toka Mwanza aje tuishi nae kwa muda huu. Dogo nimemwambia kuwa atampigia simu na kumtaarifu kuwa amwambie binti aambatane nasi kasha anipe jibu kama amekubali ili wife ndio akamchukue.
KWA WALE AMBAO HAWAKUISOMA AWALI STORY NI HII HAPA CHINI
Here is the story:-
Nina kijana mmoja ambae ni mtoto wa kwanza wa mama mdogo ambae alikuwa anaishi mojawapo za wilaya mkoani Arusha. Huyu kijana alikuwa na rafiki yake wa kike toka mwaka 98 walipomaliza elimu ya Msingi na kwa ukomavu wao wa wakati ule wakakubaliana wataoana siku za usoni baada ya yeye kumaliza masomo. Matokeo yalipotoka dogo akapata shule ya sekondari na akaenda kusoma (binti hakubahatika na wazazi hawakuweza kumsomesha) na baada ya kumaliza kidato cha 4 mwaka 2002 matokeo yake hayakuwa mazuri akawa tu yuko nyumbani. Hata hivyo aliamua baadae kurisiti baadae kupata credit zinazotakiwa. Mwaka 2006 aliamua kuendelea na chuo cha ualimu kuchukua Grade IIIA ya ualimu na baadae kupangwa Mwanza kufundisha.
Katika kipindi hiki chote binti alikuwa bado yuko nyumbani akipangua kila aina ya kaushawishi kanakokuja ili kuhakikisha anadumisha na kulinda kile alichokubaliana na mwenzake kuwa amngoje na akimaliza masomo angekuja wafunge wote ndoa.
Katika wakati wote dogo alijiandaa kuwa angemuoa na mwaka 2009 mwishoni alikuja nyumbani kutuambia kuwa yuko tayari kufunga nae ndoa hivyo tujiandae kwa maswala ya kuonana na wazazi wake. Hivyo tukawa tumekaa tayari tunangoja tusikie atakapotuambia yuko tayari twende na akawa ametuunga na huyu binti ili tuendelee kumtia moyo kwamba mwenzake yuko tayari kumuoa na amngoje. HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HADI JUZI.
Mwanzoni mwa mwaka huu dogo alituomba muda akamilishe maswala yake kadhaa kisha atakuja kutuambia rasmi ni lini mipango ianze. Wakati huu akaenda pia na kwao binti ili kumkumbushia kuwa bado anaikumbuka ahadi ile na kwa bahati (sijui ni mbaya au nzuri) wakakutana kimwili na binti akapata ujauzito.
UTATA ULIPO:
Jana jioni nikapigiwa simu na rafiki wa karibu wa dogo akinitaarifa ya kuwa kijana wetu huyu wiki iliyoisha amefunga ndoa ya kiserikali na binti mwingine ambae walisoma wote chuoni. Hii inamaanisha alifanya kinyemela na wala sisi hatuna taarifa yoyote. Rafiki yake huyu mwenyewe anadai tarifa hii hakuwa nayo bali alizipata news lately na kutafuta ushahidi na akagundua ndoa ilifungwa Bomani na kusherehekewa Kijenge Arusha ambako yeye yupo ikawa rahisi kwake kuthibitisha.
Hivi sasa ninapoandika, yule binti hajui kama mwenzake kaoa mwingine na kibaya ni kwamba kijana alimbeba mwenzake akampeleka kwenye nyumba anayokaa Mwanza na amemuacha huko akiwa amemwambia amekuja Arusha tu kwa majukumu kadhaa na atarudi mwakani mwanzoni wakati shule zinafunguliwa.
Kwa sasa binti anamtoto mchanga na amejifungua wiki chache tu zilizopita huku mshono wa operesheni ukiwa mbichi.
Sasa mimi ndie nilieko kati yao kama mwangalizi na mtu ambae ninapaswa kuchukua jukumu lolote, nimekaa usiku kucha kichwa kinaniuma najiuliza maswali mengi

- Kwa nini dogo kanificha na kafanya upumbavu wote huu???
- Kwa nini amemchezea mwenzake na kumdanganya namna hii???
- Na kinachoniumiza zaidi ni nafanya nini mimi hasa nikimuweka huyu binti ambae nilitarajia ndo atakuwa shemeji yangu?? Je nimwambie sasa, je sitamuumiza kwa mshono alionao sasa??? huyu kijana nawezaje kuficha na inakuwaje??