Nifanye nini katika hali hii??????

Ni kweli funza dume. Iwish i manage to do what you advice. The problem is dogo is more than a brother to my aunt.

And you know what, jukumu lilikuwa mikononi mwangu la kufanikisha dogo kuoa huyu binti na mimi sina huruma na dogo kama nilivyosema awali ila kinachoniumiza ni binti wa watu!!!

Na hapa natafuta kitu sahihi cha kufanya ili kumsaidia. You know what, try to be in the shoes of this lady and you will know about it.

Hapa mke wangu mwenyewe kachanganyikiwa anajaribu kuhisi angekuwa yeye ingekuwaje baada ya kupata taarifa hizi hasa akizingatia kawa muaminifu na kumngoja mwenzio kwa kipindi cha zaidi ya kumi na moja (11 years waitning in vain))???
kaka duniani kuna matatizo sana ila maji yakishamwagika hayazoleki mshauri huyo binti cha kufanya kisheria kwa kuwa amezalishwa hayo mengine yakukaa miaka 11 unamsubiri sio issue kabisa ktk dunia ya mapenzi watu wanaacha wake zao walioishi nao na kuzaa watoto kibao tena baada ya kulipwa mafao ya uzeeni sembuse huyo mwenye mtoto mmoja tu

naendelea kukushauri achana nao hao watu utaumiza kichwa bure na hautasaidia kwa chochote kama vp mtunze huyo mtoto wa ndg yako kama unamwonea huruma ila sio unaanza kumtafuta huyo dogo wakati ameshaoa na anaendeleza maisha yake na mkewe. Husiingile sana mambo ya watu utakufa bure siku si zako kwa presha ya kujitakia
 
nilikua nasisitizia tu hapo kaka angu yaani nini funza yeyote ajiweke kwenye nafasi ya huyo dada halafu apime maumivu yake
imeshatokea sasa utafanyaje inabidi tu akubali matokea na asonge mbele. Hii ndio uwa inadumaza w/wake tatizo likitokea mtu anashindwa kulikabili na kuishia kuudhunika maisha yote wakati kumbe angeweza kuli-handle na kulitupa kule na kupiga moyo konde ili kuendelea na maisha
 
What you want me to say again Maty??? Ninachomwambia Funza Dume ni kujaribu kuwa kwenye nafasi ya huyu dada halafu ataona maumivu yake. Jana mke wangu alilia kila akifikiri na kibaya ni pale tunapowaza mpaka kumuhamishia Mwanza what was he intending. Nini kiko kichwani mwake??/

Its sad men. Take time. Yana mwiso..:redfaces:
 
A%20S-alert1.gif


Waungwana Japo kazi bado pevu, NINA KILA SABABU YA KUWASHUKURU WANA JF mliotoa mawazo yenu juu ya nini nifanye kuhusiana na suala zima la dogo kama nilivyoandika hapa chini.
Baada ya kumtext dogo na kumwambia tunaheshimu uamuzi wake na niko tayari kumsikiliza na kumuelewa bila kumu-offend amenitafuta na nimeongea nae kwa muda mrefu sana.


Alichoniambia ni kwamba alifanya uamuzi huo binafsi kwani alifikia mahali kutambua kuwa hawezi kukaa nae tena na lijiona kumpenda zaidi huyu mwingine waliesoma nae chuo.
Ukweli ni kwamba dogo is like he doesn't care juu ya mwenzake aliemuacha mwanza. Ni kama anacheza mchezo Fulani wa kuigiza mpaka nikahisi au HILI TOTO LIMELOGWA NINI. Eti ananiambia alishindwa tu kumuacha na kumwambia hamtaki kwa sababu tayari alishampa mimba na hivyo amekubaliana na mke wake mpya kuwa aendelee kukaa nae kwa muda mpaka apone kidonda kasha amuambie kuwa ameoa mwanamke mwingine na hivyo hana mpango wa kukaa nae ila amuachie tu mtoto aendelee kutunza yeye akaendelee na mipango mingine ya maisha.



Pia anasema aliamua kutokututaarifu sisi wala wazazi wake kwa sababu anasema tungemtibulia na mpango wake ni kuwa mwanzoni mwa mwezi ujao ndio ataweka wazi kwa kila mtu juu ya uamuzi wake. Mawazo yake itakuwa siri kama anavyotaka kichwani mwaka huku akisahau kuwa mama yake yuko kwenye constant contact na wazazi wa binti. Ndo maana nasema limelogwa hili toto.

Kwa ushauri wenu nimeonelea nimtume tu wife week hii akamchukue toka Mwanza aje tuishi nae kwa muda huu. Dogo nimemwambia kuwa atampigia simu na kumtaarifu kuwa amwambie binti aambatane nasi kasha anipe jibu kama amekubali ili wife ndio akamchukue.


:painkiller:

Wandugu kuna utata mkubwa umetokea na umenichanganya mpaka sielewi nifanye lipi.

Here is the story:-


Nina kijana mmoja ambae ni mtoto wa kwanza wa mama mdogo ambae alikuwa anaishi mojawapo za wilaya mkoani Arusha. Huyu kijana alikuwa na rafiki yake wa kike toka mwaka 98 walipomaliza elimu ya Msingi na kwa ukomavu wao wa wakati ule wakakubaliana wataoana siku za usoni baada ya yeye kumaliza masomo. Matokeo yalipotoka dogo akapata shule ya sekondari na akaenda kusoma (binti hakubahatika na wazazi hawakuweza kumsomesha) na baada ya kumaliza kidato cha 4 mwaka 2002 matokeo yake hayakuwa mazuri akawa tu yuko nyumbani. Hata hivyo aliamua baadae kurisiti baadae kupata credit zinazotakiwa. Mwaka 2006 aliamua kuendelea na chuo cha ualimu kuchukua Grade IIIA ya ualimu na baadae kupangwa Mwanza kufundisha.

Katika kipindi hiki chote binti alikuwa bado yuko nyumbani akipangua kila aina ya kaushawishi kanakokuja ili kuhakikisha anadumisha na kulinda kile alichokubaliana na mwenzake kuwa amngoje na akimaliza masomo angekuja wafunge wote ndoa.

Katika wakati wote dogo alijiandaa kuwa angemuoa na mwaka 2009 mwishoni alikuja nyumbani kutuambia kuwa yuko tayari kufunga nae ndoa hivyo tujiandae kwa maswala ya kuonana na wazazi wake. Hivyo tukawa tumekaa tayari tunangoja tusikie atakapotuambia yuko tayari twende na akawa ametuunga na huyu binti ili tuendelee kumtia moyo kwamba mwenzake yuko tayari kumuoa na amngoje. HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HADI JUZI.

Mwanzoni mwa mwaka huu dogo alituomba muda akamilishe maswala yake kadhaa kisha atakuja kutuambia rasmi ni lini mipango ianze. Wakati huu akaenda pia na kwao binti ili kumkumbushia kuwa bado anaikumbuka ahadi ile na kwa bahati (sijui ni mbaya au nzuri) wakakutana kimwili na binti akapata ujauzito.

UTATA ULIPO:

Jana jioni nikapigiwa simu na rafiki wa karibu wa dogo akinitaarifa ya kuwa kijana wetu huyu wiki iliyoisha amefunga ndoa ya kiserikali na binti mwingine ambae walisoma wote chuoni.
Hii inamaanisha alifanya kinyemela na wala sisi hatuna taarifa yoyote. Rafiki yake huyu mwenyewe anadai tarifa hii hakuwa nayo bali alizipata news lately na kutafuta ushahidi na akagundua ndoa ilifungwa Bomani na kusherehekewa Kijenge Arusha ambako yeye yupo ikawa rahisi kwake kuthibitisha.

Hivi sasa ninapoandika, yule binti hajui kama mwenzake kaoa mwingine na kibaya ni kwamba kijana alimbeba mwenzake akampeleka kwenye nyumba anayokaa Mwanza na amemuacha huko akiwa amemwambia amekuja Arusha tu kwa majukumu kadhaa na atarudi mwakani mwanzoni wakati shule zinafunguliwa.

Kwa sasa binti anamtoto mchanga na amejifungua wiki chache tu zilizopita huku mshono wa operesheni ukiwa mbichi.

Sasa mimi ndie nilieko kati yao kama mwangalizi na mtu ambae ninapaswa kuchukua jukumu lolote, nimekaa usiku kucha kichwa kinaniuma najiuliza maswali mengi



  • Kwa nini dogo kanificha na kafanya upumbavu wote huu???
  • Kwa nini amemchezea mwenzake na kumdanganya namna hii???
  • Na kinachoniumiza zaidi ni nafanya nini mimi hasa nikimuweka huyu binti ambae nilitarajia ndo atakuwa shemeji yangu?? Je nimwambie sasa, je sitamuumiza kwa mshono alionao sasa??? huyu kijana nawezaje kuficha na inakuwaje??

Kwa kweli hata kufikiria nahisi kama nimefika mwisho wa uwezo wangu wa kufikiri na hapa nimekaa ofisini lakini hamna kitu kinaweza kwenda. Najaribu kuwaza kumtuma mke wangu aende kuonana na binti huyu huko Mwanza alipachwa (kwa sasa tuko Dom) lakini nashindwa kuelewa lipi sahihi la kufanya
 
kaka duniani kuna matatizo sana ila maji yakishamwagika hayazoleki mshauri huyo binti cha kufanya kisheria kwa kuwa amezalishwa hayo mengine yakukaa miaka 11 unamsubiri sio issue kabisa ktk dunia ya mapenzi watu wanaacha wake zao walioishi nao na kuzaa watoto kibao tena baada ya kulipwa mafao ya uzeeni sembuse huyo mwenye mtoto mmoja tu

naendelea kukushauri achana nao hao watu utaumiza kichwa bure na hautasaidia kwa chochote kama vp mtunze huyo mtoto wa ndg yako kama unamwonea huruma ila sio unaanza kumtafuta huyo dogo wakati ameshaoa na anaendeleza maisha yake na mkewe. Husiingile sana mambo ya watu utakufa bure siku si zako kwa presha ya kujitakia

Ahsante kwa mchango wako. Ni mchango mzuri sana.

But you do not know the cost of being a responsible minded person. Mchango huu ni wa muhimu na unaweza kusaidia wengine katika mazingira yao, ila kwa mazingira niliyopo na hali halisi i cant afford doing what you ask me to.

Hope umenielewa vizuri, this is a matter of someones life and making myself irresponsible i can count as one of my greatest failures in life.
 
Back
Top Bottom