Nipo Dar es salaam naweza kufanya kazi yoyote ambayo ipo ndani yahizo proffesional mbili nilizonazo mkuu
Nilijua utajibu hivi. Ndo maana hupati kazi. Hakunaga kazi yeyeto.
Tatizo la vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu, wanamaliza wakati hawwajui ni kina nani.
Mimi ningependa kuwaasa kama ivyuatavyo. By the time unaingia mwaka wa mwisho orodhesha kazi zote ambazo mtu aliye soma kazi yako anaweza kufanya. Fanya utafiti kidogo kujua ni titlez zipi ziko mtaani. Kwa mfano makazini hakuna computer scientist...ila vyuo watu wanasoma Computer science. Mtu aliyesoma computer science anaweza kuwa systems analyst, systems administrator, Database administrator etc.
So angalia kwa masomo yako unaweza kuwa nani.
Ukisha orodhesha tick kazi moja au mbili ambazo unazioenda na unadhani unaweza kuzimudu.
Mwaka wa tatu tumia muda wako kusoma na kujisomea fani uliochagua. Kwa mfano kama umechagua systems analyst angalia roles za systems analyst ni nini. Jikite huko ili uwe mbobezi na kama programme yenu ina final years project chagua final year project ambayo itakujengea ujuzi na uelewa katika fani uliyo ichagua.
Na hata unapomaliza shule endelea kujiendeleza kati fani uliyo chagua ili uwe nondo.
Unapoenda mahali kutafuta kazi usiende kutafuta kazi yoyote. Sema mimi ni sales person natafuta kazi ya sales...au mimi ni mtu wa marketing au mimi ni sytstems analyst etc.
Unapoenda mahali na kusema natafuta kazi yoyote hakuna mtu atakupa kazi. Kwa sababu utaonekana mbabaishaji.
Kampuni. zinataka mtu anayejua kazi siyo mtu atakayefundishwa kufanya kazi.