Nifanye nini cha Ziada????

Nifanye nini cha Ziada????

Sitaki kutoa pongezi kwa maamuzi ya kutafuta mtoto nje ya ndoa ila kwa mbali naona tatizo kwa mkeo.....Kama ulivyosema mkeo anakataa kwenda kupata vipimo vya afya yake ni wazi anajua chanzo cha tatizo lake na kwa kuwa aliidhamiria ndoa kuliko matokeo ya ndoa ni wazi hata ungemfunga mikono na miguu kamwe asingekubali kwenda hospitali...Matokeo ya ukatili wake ni sababu ya kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto kwani naamini yeye na hata familia yake inajua mchezo mzima. Angalizo..siku utakapo mwambia una mtoto out of ndoa atalipokea hili jambo kwa furaha ila amini usiamini wanawake wenye tatizo hili hawakawii kutoa uhai wa m2. Nakushauri ubadilishe staili ya kuishi nae, kwanza usiulize tena kuhusu kwenda hospitali ila jifanye kauzu, pili jitahidi kumpa nafasi ya upendo wake kama mke ambao naamini sasa umepungua au haupo tena kwani huko nyumba ndogo unavutwa na damu yako, tatu baada ya kitambo kidogo i.e hadi mwaka ukitekeleza kwanza na pili hapo juu kaa na mkeo katika hali ya kimahaba umuulize mkasa mzima, naamini utaambiwa vitu ambayo vinaweza kukuliza kwa kumwonea huruma au kukujaza hasira kwa kumwona mzembe ila upokee vyote katika hali ya upendo wa hali ya juu na Mwisho nakushauri umpe nafasi ya upendo moyoni mwako kwani miaka 10 ya ndoa yako inatoa picha ya maisha mazuri mliyokaa pamoja. Sina la kushauri kuhusu nyumba ndogo ila waweza rejea viapo vyako vya ndoa.
 
dah !nafikiri huyo dada analijua tatizo la yeye kutokuzaa ndio sababu hataki kwenda hospitalini lol hii dunia ione tu inazunguka jamani .wewe cheti chako cha ndoa kinaruhusu ndoa ngapi?tuanzie hapo

nivea cheti changu kinaruhusu ndoa moja.Huo ndio mtihani nilionao
 
NDUGU YANGU nimekaa na mawazo,Kuna muda nashikwa na hasira natamani nimuambie ukweli lakini naona kama naweza kusababisha madhara makubwa kama sio kwakwe,ni kwa yule mwanamke ambaye amekubali kunizalia mtoto wa kwanza,na amekuwa radhi kuniongezea mwingine,au hata kwangu pia maana nimeshaanza kuona dalili za ushirikina

Hapo utajua sasa wewe.......
 
Kaka tafuta wataalamu wa saikolojia uende na huyo mke wako,ingawa nakulaumu kwa maamuzi ambayo umeshayafanya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mjela
Kati ya ugomvi nilionae na bibie huyo ni kuwaeleza watu matatizo tuliyonayo.hata kwa mchungaji akuombee hataki ajue ndio sembuse huyo mtaalamu wa saikolojia unayemsema??/
 
Kupata mtoto ni majaliwa ya muuba wetu,umeamua kutoka nje ili uje kama wewe umzima au la na je yeye akiamua kutoka nje utamfukuza?fikiria kwanza kabla hujachukua maamuzi.
 
mjomba2011 naomba uni PM namba ya waifu wako, nina dawa ya kupaka ya kuleta watoto kwenye ndoa.
Dawa inapakwa usiku kwenye chumba chenye giza totoro, haruhusiwi kusindikizwa na mtu mwingine yoyote.

Bujibuji japokuwa una dawa hiyo, mimi mwenyewe pamoja na kuwa na matatizo na mke wangu (siyo ya uzazi) siwezi kuruhusu umpake hiyo dawa!
 
Sitaki kutoa pongezi kwa maamuzi yz kutafuta mtoto nje ya ndoa ila kwa mbali naona tatizo kwa mkeo.....Kama ulivyosema mkeo anakataa kwenda kupata vipimo vya afya yake ni wazi anajua chanzo cha tatizo lake na kwa kuwa aliidhamiria ndoa kuliko matokeo ya ndoa ni wazi hata ungemfunga mikono na miguu kamwe asingekubali kwenda hospitali...Matokeo ya ukatili wake ni sababu ya kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto kwani naamini yeye na hata familia yake inajua mchezo mzima. Angalizo..siku utakapo mwambia una mtoto out of ndoa atalipokea hili jambo kwa furaha ila amini usiamini wanawake wenye tatizo hili hawakawii kutoa uhai wa m2. Nakushauri ubadilishe staili ya kuishi nae, kwanza usiulize tena kuhusu kwenda hospitali ila jifanye kauzu, pili jitahidi kumpa nafasi ya upendo wake kama mke ambao naamini sasa umepungua au haupo tena kwani huko nyumba ndogo unavutwa na damu yako, tatu baada ya kitambo kidogo i.e hadi mwaka ukitekeleza kwanza na pili hapo juu kaa na mkeo katika hali ya kimahaba umuulize mkasa mzima, naamini utaambiwa vitu ambayo vinaweza kukuliza kwa kumwonea huruma au kukujaza hasira kwa kumwona mzembe ila upokee vyote katika hali ya upendo wa hali ya juu na Mwisho nakushauri umpe nafasi ya upendo moyoni mwako kwani miaka 10 ya ndoa yako inatoa picha ya maisha mazuri mliyokaa pamoja. Sina la kushauri kuhusu nyumba ndogo ila waweza rejea viapo vyako vya ndoa.
:smile-big:
 
Ndugu yangu sio kukimbia kimbia,Hadi kufikia hatua ya kuamua kuzaa huko nje,ni Kiburi na maudhi yake,Kitu ambacho wakati wa uchumba hakikuwepo.mpaka imefikia hatua ya kwenda kwa waganga.Nimejitahidi kuwa mvumilivu kutokuongea lakini haisaidii.
Kuhusu uhakika wa mtoto nina uhakika kwa sasilimia zaidi ya 90,kwann nasema hivyo?nimefuatilia siku za dada niliyezaa nae zaidi ya mwaka moja na nusu,mpaka kuamua kuzaa nae tayari alishatoa mimba zangu zaidi ya 3,ilikuwa ikiingia namwambia toa,NIKIWA NAJIPA MOYO LABDA HUMU NDANI ITAKAMATA,WAAAAPI HADI LEO

Kwenda nje ya ndoa sio dawa, ila ni kuongezea matatizo kwenye ndoa yako.
Sema na mkeo ili mkaangalie vipimo vya uzazi kwa wote waliwi (wewe na mkeo).
Baada ya hapo ndio utajua la kufanya. Ila kwa nanma yoyote ile, ufumbuzi sio kwenda nje ya ndoa.
Kwenda nje ya ndoa ni kero kubwa sana, maana utajisikiaje ikiwa mkeo nae anaenda nje ya ndoa na kupata ujauzito huko ??
 
Kumbe kuna wakati wanawake mambo mengine tunajitakia wenyewe!
 
Kumbe kuna wakati wanawake mambo mengine tunajitakia wenyewe!

mkempia kweli huwa mnasema wanaume wakorofi lakini kuna muda mwingine huwa nyie mnazidi,kiukweli swala la kuzaa nje ya ndoa nilikuwa naona kama ni ajabu nilivyokuwa mdogo lakini nimeamini ule usemi wa KUWA UYAONE,NIMESHAYAONA MWENYWE
 
Cha ziada ni kutunza wanao - na uwe na amani na mkeo hadi ukiona mood imetulia then unaweza mkalisha chini na kumwambia kuwa nina watoto. Ila kama mtu anajihusisha na ushirikina ni hatari sana , tena sana . Usifubie macho hayo matatizo haswa ya ushirikina -- ni vema kuongea na mzee wa busara hata kanisani, maana yatajakutokea puani. Mkeo anahitaji msaada wa hali ya juu hivyo usikubali apotee huko gizani.
 
maelezo yako yanaonesha wewe ndio umeolewa/ mke anabehave kana mume... Unathubutu kuadmitt eti umeshindwa kwenda nae hospitali mguu kwa mguu.. pathetic
 
Mkeo anajua ujana wake alifanya nini, ndiyo maana hataki kwenda kufanyiwa vipimo ili kujua tatizo liko wapi.


Kuna kaka mmoja tulikuwa tunafanya naye kazi, alipata mchumba siku si nyingi akatangaza ndoa. Kumbe mke yule alishatolewa kizazi katika usichana wake. Ndoa ilivunjika baada ya muda mfupi sana.

Nenda naye taratibu muda si mrefu kila kitu kitakuwa wazi juu yake.
 
mjomba2011 hizo mimba tatu una uhakika nazo kwa maana ya vipimo? Kama anaweza kubeba mimba ina maana mke wako hana matatizo; chunguza sababu inayopelekea mimba kutoka inaweza kuwa unamfanyiza sana kazi au wewe ni mkali sana kwa mkeo[/QUOTE
Ndachuwa.Mimi ni msomi wa degree tena sio moja ndugu yangu,Mimba ninazokuambia sio kwamba ni za mke wangu wa ndoa.MKE WANGU WA NDOA HAJAWAHI HATA KUSHIKA MIMBA IKAHARIBIKA,Hizo tatu ninazokuambia ni za huko nje ila sio kwa wanawake tofauti hapana ni kwamwanamke mmoja
mjomba2011 kumbe tayari una mji mwingine hofu ya nini? Mtambulishe tuu watumbuane akitaka kuondoka umruhusu ili uweze kulea watoto wako kwa uhuru zaidi
 
Last edited by a moderator:
mh leo sina la kuchangia. wacha nipite tu. anyway, hongera kwa watoto, its good to be a father. mi sitakuhukumu maana sio kazi wala wajibu wangu kutoa hukumu. Nashangaa hapa watu wanavyokuhukumu kwa kuzaa nje. congraturations baba fulani
 
Sasa apo tatzo liko wapi ndoa n maelewano watoto majaliwa.we huna raha ndan ya ndoa alafu uzaz hakuna ,umetoka nje umepata mtoto sasa unataka nn timua mke mkubwa na jeur zake vuta mke mdogo unaeelewana nae kwan ndoa n lazma au kifungo?
 
Back
Top Bottom