Nifanye nini biashara yangu ikue?

Nifanye nini biashara yangu ikue?

Unajua mkuu wewe unachanganya mambo ndio maana hunielewi. Kuna tofauti kati ya mtu anayefanya biashara ili apate miambili ya kula leo na anayefanya ili aidhi kidon. Ninachokisema mimi, hio 500 ni nyingi sana hio, sasa ninaposema nyingi wewe unaanza kuwaza afanye biashara ya 500k apate faida anunue gari, ajenge aishi vizuri, hapana. Ukienda uswahilini kuna akina mama wanachoma mandazi, chapati au vitumbua. Mtaji wao hata 100k haufiki. Anaamka asubuhi achoma maandazi, kufika saa5 yameisha. Anachukua faida ananunua unga na fungu la samaki mchana umepita, jioni wali maharage, kesho tena. Hio ni biashara, vipi huyo wa 500k?

Sheria ya biashara ni moja tu, pamoja na kuwa na akili, uendeshaji sahihi nk, ila pia ili upate faida kubwa lazima u wekeze zaidi, hilo halikwepeki. Ukiuza pipi utawekeza kidogo na faida itakua ndogo, ukiuza magari utawekeza zaidi na faida itakua kubwa.

Narudia tena 500k ni hela kubwa sana na biashara za huo mtaji zipo nyingi. Amini kwamba 500k ni dream mtaji wa watu wengi sana, kuna watu wanaitafuta hata nusu tu ya hio ili waamze safari zao. Narudia usichanganye kupata faida kubwa, kubadili maisha na huo mtaji mdogo, havitawezekana kirahisi
Hapo mkuu nimekuelewa mazima aiseee yaani hapo nimekupata daah..
Maana nayoona hapa kwangu naona kabisa kuja kujenga daaah nikaze sana an sana sana mno
 
Hapo andaa pesa za kutosha gari kuivuta mpaka hapa toka dubai unaujua ushuru wa TRA kwa kila gari unataka ufungue showroom yenye gari 2? Yard inabidi iwe na gari kuanzia 100 sasa una kamtaji kako ka laki 5 unataka ufungue Yard hio si pesa ya kufungua Genge la nyanya na viazi mviringo
Unanitukana mkuu 😂😂
Unataka kusema niuze genge
 
Narudia tena 500k ni hela kubwa sana na biashara za huo mtaji zipo nyingi. Amini kwamba 500k ni dream mtaji wa watu wengi sana, kuna watu wanaitafuta hata nusu tu ya hio ili waamze safari zao. Narudia usichanganye kupata faida kubwa, kubadili maisha na huo mtaji mdogo, havitawezekana kirahisi
Ukochomoa buku tu ushaanza kupukutika yaan hizo 10 10 siku hizi buku 10 masaa mawili mengi imeisha
 
Mkuu nilishaibiwa aiseeee an kuna mda unapata kiasi ambacho huna budi kujifungia ndani na kuanza kulia kwa kwikwi
😂😂😂 ndo ukubwa huo. Tukitoka nje tunacheka cheka utafikiri tuko sawa. Tukiwa pekeetu vichwa vinauma, kila muda unajifanyia kikao😂
 
Ukuaji wa biashara yako unaenda sambamba na ukuaji binafsi wewe kama mmiliki,yaan kiwango chako cha ufahamu na maarifa.

Are you grow?

Hauwezi kwenda zaidi ya maarifa ulyonayo kuhusu unachofanya.

Mwingne akaenda mbali zaid kusema huwez kuwa zaid ya tabia yako.
 
Back
Top Bottom