Nifanyaje kuhusu Ugomvi huu?

adonack

Member
May 16, 2021
55
24
Ndugu zangu, kuna mambo flani huwa yananichanganya

Kuna mtu mmoja tunaishii naye nyumbani (mimi nakaa kwa baba mdogoo bado sjafanikiwa kujitegemea). Mtu huyu ana nafasi kubwa kwa baba yangu mdogo zaid yangu, anasomeshwa chuo.

Pia, huyu mtu amekua akinifanyia mambo ya ajabu ni mtu wa kuninunia ovyoo kunisema kwa watu kama kuna mtu ni rafiki kwangu basi atagombana naye yaani kwa upande mwingine nadhani hata kuniona pale hataki na mimi sina cha kufanya kwasababu sina sauti kwa baba mdogo zaidi yake na mpaka sasa siishi kwa amani kabisa

Tunaishi na mfanyakazi wa ndani na shemeji yake na baba mdogo na kutokana na huyo mtu wamekua wakinitengaa.
 
Usiwachukie Huyo ndio ngazi yako ya mafanukio, Jitahidi kufanikisha malengo yako ili ujitegemee, Tatizo la watu wengi ni kutokujua kuwa mahali unapokaa umehifaziwa kwa muda, kwa hio wewe lazima uweke malengo, kwa mfano unakaa miaka 2, ndani ya hio miaka 2 uwe umejitegemea, Lazima ujue siku ya kutoka, kuanzia siku ya kwanza unaingia.

Binadamu kwa asili ni mvivu kwa hio ni lazima uhakikishe unaondoa huo uvivu,na kataa kupewa pesa au vitu vya bure kama zawali nk, ni sumu Kubwa sana kek maisha na huharibu maisha ya watu wengi sana bila kujua, Bali wewe Kuwa mtu wa kutoa zawadi au kusaidia wengine unapoweza na unapoona wana shida ya kweli.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Usiwachukie Huyo ndio ngazi yako ya mafanukio, Jitahidi kufanikisha malengo yako ili ujitegemee, Tatizo la watu wengi ni kutokujua kuwa mahali unapokaa umehifaziwa kwa muda, kwa hio wewe lazima uweke malengo, kwa mfano unakaa miaka 2, ndani ya hio miaka 2 uwe umejitegemea, Lazima ujue siku ya kutoka, kuanzia siku ya kwanza unaingia. Binadamu kwa asili ni mvivu kwa hio ni lazima uhakikishe unaondoa huo uvivu,na kataa kupewa pesa au vitu vya bure kama zawali nk, ni sumu Kubwa sana kek maisha na huharibu maisha ya watu wengi sana bila kujua, Bali wewe Kuwa mtu wa kutoa zawadi au kusaidia wengine unapoweza na unapoona wana shida ya kweli.
Ahsantee nitafanya hilo
 
Huyo mtu ana undugu gani na baba mdogo? Mwanae au nae wa kuja kama wewe?
 
Huyo mtu ana undugu gani na baba mdogo? Mwanae au nae wa kuja kama wewe?
Tena boraa mimi kidg naweza kusema ni baba mdogo yeye ni mtu alitafutwa kusimamiaa ujenzii wa hiyo nyumbaa lakn mpka leo yupo na anasomeshwaa na kama nilivyo sema ana ukaribuu mkubwa
 
Ndugu zangu kuna mambo flan hua yananichanganya


Kuna mtu mmoja tunaishii nae nyumbani (mm nakaa kwa babamdogoo bado sjafanikiwa kujitegemea) mtu huyu ana nafasi kubwa kwa baba yangu mdogo zaid yangu anasomeshwa chuo pia huyu mtu amekua akinifanyia mambo ya ajabu ni mtu wa kuninuniaa ovyoo kunisema kwa watu kama kuna mtu ni rafki kwangu basii atagombana nae yani kwa upande mwengine nadhani hata kuniona pale hataki na mimi sina cha kufanya kwasababu sina sauti kwa baba mdogo zaid yake na mpka sasaa siishi kwa amani kabisa tunaishi na mfanyakaz wa ndan na shemeji yake na baba mdogo na kutokana na huyo mtuu wamekua waKinitengaa....
Kwa jinsi ulivyoandika kwa tone ya kulalamika, inaonekana wewe ni binti. Manyanyaso yakizidi tafuta limjamaa muanze kuyajenga maisha mdogo mdogo. Beleave me! UTAKUJA KUNISHUKURU.
 
Kuna nyuzi humu inahusiana na watu walio wahi ishi kwa ndugu kuna madini kule kapitie
Note jina la nyuzi nimelisahau ila unaweza andika "tulio wahi fukuzwa kwa nfugu/nyanyaswa na ndugu"
 
Kuna nyuzi humu inahusiana na watu walio wahi ishi kwa ndugu kuna madini kule kapitie
Note jina la nyuzi nimelisahau ila unaweza andika "tulio wahi fukuzwa kwa nfugu/nyanyaswa na ndugu"
Sawaaa boss ngoja nitafute
 
Amnaa broo ni wa kiumee
Kama ni wa kiume itakuwa ni uzembe flan hv. Iko hivi, katika hali ya kunyanyasika, mwanaume anayejua uchungu wa maisha huweza kuyaanza mapambano ya maisha hata kwa mtani wa elfu kumi.

Cha mhimu asibague kazi, ajitahidi kuwa mwenye tabia nzuri ili asiwe kero kwa wengine na zaidi ya yote amuombe Mungu ampe afya thabiti. Maisha ni mapambano na pia malengo.
 
Kama ni wa kiume itakuwa ni uzembe flan hv. Iko hivi, katika hali ya kunyanyasika, mwanaume anayejua uchungu wa maisha huweza kuyaanza mapambano ya maisha hata kwa mtani wa elfu kumi. Cha mhimu asibague kazi, ajitahidi kuwa mwenye tabia nzuri ili asiwe kero kwa wengine na zaidi ya yote amuombe Mungu ampe afya thabiti. Maisha ni mapambano na pia malengo.
Nimekupata mkuu
 
Sawaaa boss ngoja nitafute
Alikuja kusimamia ujenzi babako mdog akaamua kumsomesha na ana ukaribu naye.
Basi hapo ndipo ujue jamaa alionyesha kuwa ana potential. Huenda anajiongeza anajituma kabla ya kutumwa.
Anza iba madini yake mkuu uige mazuri kutoka kwake
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom