Kwanza pole kwa kuuguliwa na pole kwa mkanganyiko unaoendelea ktk familia yako. Hata mimi nikiwa sekondari niliwahi kujiambia kuwa nikshafanikiwa katika maisha kamwe baba asinitafute na sitokua tayari kumsaidia kwa hali yeyote. Lakini nadhani angekuepo leo ningemsaidia kwa kuwa nilijifunza kusamehe japokua Mungu alishampenda kwa sasa.
Ninakushauri kama mama yako yuko tayari kumhudumia na mumeo ameridhia basi jaribu kukaa na mama mumsihi dada pia asahau yaliyopita na mumsaidie huyo mzee. Nasema hivi kwa kuwa huezi jua ni kwa nini haya yanatokea na moyo wako kwa kiasi flani unakusukuma umsaidie, alafu huyo ndiye baba yako hata iweje ukweli utabaki hivyo tu.
Alafu unasema hujamuachilia kabisa kwa aliyotenda. Akifariki hukumsaidia huoni unaweza kuwa guilty zaidi utaishi maisha gani dhamira inakusuta? Yeye alichagua kutokuwasaidia tena ikiwa ni wajibu wake na Mungu amewapigania mmefanikiwa mwache akajibu sehemu yake ila we fanya yako . Achana na style ya maisha aliyoyachagua zamani ambayo utakapomsaidia dhamira yake kumsuta ni adhabu tosha kwa kuwa anajua alichowafanyia. So please msimuadhibu kwa mara nyingine imetosha. Jiulize kama Mungu akihesabu makosa utakua wapi then fuata moyo wako. Ila nakusihi usimuache kaeni nyie watatu msaidiane.