Nifanyaje ili nijitoe ktk mfuko wa bima ya afya

sasa maswali mengine hayana kichwa wala mguu. wewe ulijiunga vp hadi uulize jf ujitoe vp? huna HR hapo unapofanyia kazi? wakati unajaza fomu na kusubmit picha ulimpa nani? kamuulize huyohuyo utoke vp.

kumbe na ww unaweza ukasukummwa kama ng'ombe na ukaenda .....
jari huduma unayopata na unavyogharamia, pia na uhuru wa kuchagua sio kuwa mwanachama kwa SHURTI ktk Mfuko huo.
 
Sio BOT tu, hata Tanesco nao wanatumia AAR,,

Mashirika ya serikali makubwa yamegoma wafanyakazi wake kutumia nhif sababu wanajua ni magumashi..

Wafanyakazi wa BOT, Tanesco,etc wanatibiwa hospitali za nguvu as Aga khan, first track muhimbili, etc ambapo hizo hospitali haziitaki nhif

Wanachama wa NHIF hawana tatizo lolotea huduma kwenye mikoa mikubwa kama Dar, Morogoro, Arusha, Knjaro Mbeya Mwanza etc ila tatizo Lao lipo kwenye mikoa midogo na vijijini. Na hili siyo kosa lao maana hawajengi hospitali ila husajili zilizopo
 
Kujitoa Mfuko wa Bima ya Afya masharti yake ni kuhakikisha unafuata kanuni za afya wewe na familia yako bila kuugua. Ukifanya hayo ukaepuka kuugua hakika utakuwa umejitoa katika "Mfuko wa Bima ya Afya"
 
mimi nafanya kazi BOT card tunayotumia ni JUBILEE
Nafikiri mnaotumia JUBILEE pia hamjaonja adha wanazopata watumiaji wa NHIF. Hoja yangu bado iko palepale, Kwa nini nyie mliikataa NHIF na kuamua kuchukua JUBILEE?
 
kwa sheria namba 8 ya mwaka 1999 CAP 395 R.E 2002,
Mtumishi yoyote wa serikali kwa mujibu wa sheria hii ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya. uanachama ni lazima kwa watu hawa. sheria ilipitishwa na bunge la jamuhuri la muungano wa tanzania. bunge ni uwakilishi wa wananchi hivyo mimi na wewe tuliwakilishwa na wabunge wetu wakapitisha sheria hii.

hivyo basi kigezo cha kwanza kabisa cha wewe kuwa mwanachama ni wewe mtumishi wa serikali kama hutaki yafuatayo unatakiwa kufwata
1. kama mtumishi wa serikali acha kazi au jiajiri mwenyewe au ajiriwa katika mashirika binafsi uweze kuchagua bima ya afya unayoitaka.
2. mwambie mbunge wako apeleke hoja binafsi bungeni kutoa sheria hii. ikijadiliwa na kuonekana inafaa kutolewa au kurekebishwa na kuweka uhiari basi itafanyika kuwa hivyo.
Kwani JUBILEE nayo ni "mfuko wa Taifa wa Bima ya afya". Au BoT mmeamua kuvunja sheria?
 
Nafikiri mnaotumia JUBILEE pia hamjaonja adha wanazopata watumiaji wa NHIF. Hoja yangu bado iko palepale, Kwa nini nyie mliikataa NHIF na kuamua kuchukua JUBILEE?

Baadhi ya taasisi zinatengeneza mapato yao wenyewe na kufanya matumizi yao namna zinavyotaka kwa sheria zilizotengeneza taasisi hizo mfano ni BOT,TCAA,TBS,nk watumishi wake hawalipwi na hazina hivyo wanouamuzi wa kuchagua wanayoyataka kufanya.

hawa wanaolipwa na hazina wote sheria imewabana nadhani hii ndio sababu ya baadhi ya mashirika ya uma kutokuwa wanachama wa NHIF.
ikumbukwe kuwa NHIF haimkati mtumishi pesa za kila mwezi bali hazina kupitia mwajiri ndio anayekata na kupeleka lile fungu husika NHIF ili sasa NHIF iwapatie kadi za matibabu na kuanza kupata huduma za afya.
 
Nafikiri mnaotumia JUBILEE pia hamjaonja adha wanazopata watumiaji wa NHIF. Hoja yangu bado iko palepale, Kwa nini nyie mliikataa NHIF na kuamua kuchukua JUBILEE?

si hivyo ndugu yangu nimebahatika kufanya kazi mikoani na kuwa natumia kadi hiyo ya jubelee mahasibu ni yaleyale foleni na maudhi mbalimbali ya hospitali na vituo vyetu vya kupata huduma za afya. kama nilivyoeleza awali kuna tatizo nchini la huduma mbovu katika vituo vyetu vya kupata huduma za afya lakini pia kuna tatizo la uhaba wa vituo binafsi vyenye ubora wa kutoa huduma stahiki kutokana na miongozo iliyowekwa nchini ya afya kupitia wizara husika.

na utaona vituo vizuri viwe vya serikali au binafsi watu wote hukimbilia huko na kusababisha msongamano mkubwa bila kujali kadi gani ya bima aliyonayo iwe ya nhif,jubilee,strategies au AAR tunakutana hukohuko wote na kutibiwa sawa sawa na kupata adha sawa.
 
Nafikiri mnaotumia JUBILEE pia hamjaonja adha wanazopata watumiaji wa NHIF. Hoja yangu bado iko palepale, Kwa nini nyie mliikataa NHIF na kuamua kuchukua JUBILEE?

nilisha wahi kutumia kadi ya NHIF na hadi sasa ninayo pia amini nakwambia kwa mifumo mibovu ya nchi yetu adha za watumiaji wa kadi za bima hazina utofauti. na wakati mwingine NHIF members haswa mijini wana nafuu sana kwani kifurushi chao cha mafao kina mambo mengi ambayo kwenye kadi zingine huwezi kupata.

sababu
nhif kwa vile ni shirika la uma haipo kufanya biashara bali kutoa huduma, tofauti na bima za afya za makampuni mengine ambao wao kwa asili yao wanafanya biashara.
wana madaraja na limitation nyingi.
 
si hivyo ndugu yangu nimebahatika kufanya kazi mikoani na kuwa natumia kadi hiyo ya jubelee mahasibu ni yaleyale foleni na maudhi mbalimbali ya hospitali na vituo vyetu vya kupata huduma za afya. kama nilivyoeleza awali kuna tatizo nchini la huduma mbovu katika vituo vyetu vya kupata huduma za afya lakini pia kuna tatizo la uhaba wa vituo binafsi vyenye ubora wa kutoa huduma stahiki kutokana na miongozo iliyowekwa nchini ya afya kupitia wizara husika.

na utaona vituo vizuri viwe vya serikali au binafsi watu wote hukimbilia huko na kusababisha msongamano mkubwa bila kujali kadi gani ya bima aliyonayo iwe ya nhif,jubilee,strategies au AAR tunakutana hukohuko wote na kutibiwala sawa sawa na kupata adha sawa.
Mimi niliumia sana nilipolazimishwa kunywa dawa ambazo situmii, kwa sababu ninazotumia hazipo kwenye orodha ya dawa zinazolipiwa na NHIF
 
dawa zinazotolewa na NHIF ni zile zilizoaiinishwa na WIZARA ya afya na ustawi wa jamii, huwa wao wanafocus katika content ya dawa sio trade names, mfano minyoo huwa wanaangalia mabendazole na albendazole na nyingine content ni sawa. isipokuwa wapi imetengenezwa na imepakiwa vipi. mfano mgonjwa yeye anapenda ile ya kenya au ya india kumbe ya kenya india na pakistani contents za dawa ni sawa utofauti upo katika namna ilivyopakiwa na wapi imepakiwa ukienda hospitali daktari anakwambia bima ya afya wanatoa mabendazole wewe unakasirika na kusema wamenipa dawa mbaya ya bei ya chini kumbe dawa ni nzuri na haina tofauti na zile zingine ki matibabu.

ila ipo changamoto sasa ya mabadiliko ya bei na ile list ya dawa za wizara na bei zake.unakuta dawa zinapanda bei lakini list ya wizara haijafanyiwa review hapo ndio shida inapokujaga NHIF hukaa na wadau na kujitahidi kuendana na mabadiliko haya ya mfumuko wa bei za dawa na hapohapo kuangalia fuko lisizidiwe likafa kwa kutodhibiti mfumuko huo wa bei za dawa wakishirikiana na wadau ambao ni wizara husika watoa huduma n.K
 
wanachama wa nhif hawana tatizo lolotea huduma kwenye mikoa mikubwa kama dar, morogoro, arusha, knjaro mbeya mwanza etc ila tatizo lao lipo kwenye mikoa midogo na vijijini. Na hili siyo kosa lao maana hawajengi hospitali ila husajili zilizopo

mkuu nakuomba uje unisaidie kuelewesha nipumzike, wananchi wenzetu wengi wao wanalalamika pasipo kuwa na taarifa sahihi na wamekuwa hawataki kutafuta taarifa sahihi.
 
kwa sheria namba 8 ya mwaka 1999 CAP 395 R.E 2002,
Mtumishi yoyote wa serikali kwa mujibu wa sheria hii ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya. uanachama ni lazima kwa watu hawa. sheria ilipitishwa na bunge la jamuhuri la muungano wa tanzania. bunge ni uwakilishi wa wananchi hivyo mimi na wewe tuliwakilishwa na wabunge wetu wakapitisha sheria hii.

hivyo basi kigezo cha kwanza kabisa cha wewe kuwa mwanachama ni wewe mtumishi wa serikali kama hutaki yafuatayo unatakiwa kufwata
1. kama mtumishi wa serikali acha kazi au jiajiri mwenyewe au ajiriwa katika mashirika binafsi uweze kuchagua bima ya afya unayoitaka.
2. mwambie mbunge wako apeleke hoja binafsi bungeni kutoa sheria hii. ikijadiliwa na kuonekana inafaa kutolewa au kurekebishwa na kuweka uhiari basi itafanyika kuwa hivyo.
Nimekusoma
 
mkuu nakuomba uje unisaidie kuelewesha nipumzike, wananchi wenzetu wengi wao wanalalamika pasipo kuwa na taarifa sahihi na wamekuwa hawataki kutafuta taarifa sahihi.

hata mm, nimekuelewa sana, pale ulipoweka na kifungu cha sheria.
lakini kama mdau au mchangia pia naamini ana haki ya kutoa HOJA, au kujadilina na kujua mawazo mbadala.
pia ktk huduma za NHIF wateja wao wanaburuzwa tu japo kiac huduma zinatolewa lakini chini ya kiwango....
 
MKUU,
napenda uelewe kuwa kitu chochote kinachopitishwa bungeni maana yake mimi na wewe tumechangia na kutoa hoja zetu kupitia wabunge wetu ingekuwa sheria imekuja tu pasipo kupita bungeni tungesema hatujahusishwa hatujahoji hatujatoa maoni yetu.kitu ambacho hakipo.
tuna haki ya kutoa hoja ndio hoja zilizotolewa wakati huo na zikapitisha sheria hii sasa kuibadili mtumie mbunge wako arudishe swala hili ili lichangiwe upya na kubadilishwa. ni hivyo mkuu. nchi yenye wananchi wengi kama tulivyo tanzania ni ngumu kuwa na mkutano wa pamoja kama ilivyokuwa ATHENS by then walivyokuwa wana direct democracy. hapa tuna wawakilishi ambao kwa akili zao na utashi wao na maslai yao wakifika mjengoni hupitisha ama kutopitisha vitu vingi tu na vikisha pita mimi na wewe tunalazimika kuvifuata kulalamika tu hakutasaidia chochote.
 
ingekuwa ni hivyo basi sheria zingekuwa hazifanyiwi mabadiliko....
pia kama Mbunge wangu au wa mwingne hana mikutano na wananchi wake..... sasa haya yatasemwa wapi ?? au kutolewa taarifa wapi ?? hili watendaji wajirekebishe au wabuni njia madhubuti za kutoa huduma.
lakini kuwa kimya.... hii ndio hatari zaidi,
 
Huu mfuko hauna maana kabisa,nimeshuhudia watoto wa marehemu wakinyangaywa kadi wiki mbili baada ya mzazi wao ambaye alikuwa mwanachama kufariki,pia nimewahi kuona kikongwe kadi yake ikiwa confisticated kwa madai kuwa mwanae aliyekuwa anachangia amefariki dunia.Hii ni policy chafu sana ya kuhudumia wategemezi pale mchangiaji anapokuwa hai na mara anapofariki huduma inasitishwa mara moja bila kujali mwanachama wao kaacha watoto wadogo,wazee wasio na uwezo wa kujihudumia,kumnyaganya mfiwa kadi mara tu baada ya mpendwa wao kufariki ni kuongeza machungu juu ya machungu.kwa maoni yangu huu mfuko hauna maana kabisa kutokana na policy zao mbovu.
 
ni kweli kabisa huu mfuko/ taasisi ni ya kifisadi au wezi tu.......

hapo ktkr red, inashangaza kuona shirika/taasisi badala ya kuongeza wateja, wnyewe wanaridhika kupunguza wateja au kutojari wateja/wanachama wapya.... hii inatia mashaka sana.

najiuliza wameridhika kiac gani, au wamesahau kwamba mwanachama mmoja anaweza kuongeza matumizi/mapato kulingana na huduma anayopata na kuongeza thamani ya kuwa mwanachama/ mapato.
 
dawa zinazotolewa na NHIF ni zile zilizoaiinishwa na WIZARA ya afya na ustawi wa jamii, huwa wao wanafocus katika content ya dawa sio trade names, mfano minyoo huwa wanaangalia mabendazole na albendazole na nyingine content ni sawa. isipokuwa wapi imetengenezwa na imepakiwa vipi. mfano mgonjwa yeye anapenda ile ya kenya au ya india kumbe ya kenya india na pakistani contents za dawa ni sawa utofauti upo katika namna ilivyopakiwa na wapi imepakiwa ukienda hospitali daktari anakwambia bima ya afya wanatoa mabendazole wewe unakasirika na kusema wamenipa dawa mbaya ya bei ya chini kumbe dawa ni nzuri na haina tofauti na zile zingine ki matibabu.

ila ipo changamoto sasa ya mabadiliko ya bei na ile list ya dawa za wizara na bei zake.unakuta dawa zinapanda bei lakini list ya wizara haijafanyiwa review hapo ndio shida inapokujaga NHIF hukaa na wadau na kujitahidi kuendana na mabadiliko haya ya mfumuko wa bei za dawa na hapohapo kuangalia fuko lisizidiwe likafa kwa kutodhibiti mfumuko huo wa bei za dawa wakishirikiana na wadau ambao ni wizara husika watoa huduma n.K

sikubaliane nawe unaposema kwamba dawa zinazotengenezwa hapa nchini bora kuliko za kutoka kenya, india, pakistan, ulaya, marekani na kwingineko. Dawa zinazotengenezwa katika nchi hii ya ufisadi na uchakachuaji ndizo za hali ya chini na za ovyo kuliko dawa zote ulimwenguni...na haziwezi kuwa exported kwenda nchi yeyote...haziwezi kukubalika kamwe...huwa zinachakachuliwa mno. Na ndio maana zinauzwa kwa bei ya chini pamoja na kwamba gharama za umeme ziko juu...tungetegemea ziuzwe kwa bei ya juu kwa kuwa bei ya umeme ipo juu.

NHIF sio wa kuwaonea huruma financially...wanazo fedha nyingi sana hadi zingine 'wanawakopesha' serikali (Tsh 3.6 trilion)--hizi hazilipiki--pesa za umma zinapotea bure bilashi!
 
Back
Top Bottom