Iron Lady
JF-Expert Member
- Mar 4, 2008
- 4,071
- 1,381
upo sahihi kabisa mkuu wa hapahapa,ufanisi wa NHIF upo chini sana,na kwa bahati mbaya hakuna kiongozi yeyote anayejali,walichofanya hawa viongozi wetu ni kuanzisha card maalum kwa ajili yao na wategemezi wao (NHIF GREEN CARDS) ambazo kimsingi zionawatofautisha wao na wanachama wengine wa NHIF kwa sababu kwa card zao wanapata huduma katika hospitali bora kabisa za binafsi jambo ambalo mimi na wewe hatutaweza kutibiwa!
sisi wa mijini tuna unafuu mkubwa sana maana angalau unaweza kuchagua kituo chenye unafuu,wenzetu hawana uchaguzi huo,wanalazimika kupokea huduma mbovu zilizopo karibu,na pia hata wakipewa fomu maalum ya NHIF ya kwenda kuchukua dawa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kuzifuata pharmacy zinazopokea prescription za NHIF na wao pia wanakunyima dawa kwa sababu bei ya NHIF haiwalipi.
Sasa wewe unaongelea miundo mbinu ya vijijini ulitegemea NHIF ifanye nini ikiwa hakuna vituo vyenye ubora huko huoni imejitahidi hata kuingia mikataba na maduka ya dawa muhimu na pharmacies pale ambapo dawa zinakosekana mahospitalini zahanati na vituo vya afya?
ni vema muelewe kuwa NHIF haimiliki kituo chochote cha kutoa huduma inachofanya ni kulipa madeni ya huduma za matibabu ambazo watu huenda kutibiwa iwe yupo karibu na zahanati hospitali ya wilaya au hospitali ya kidini iliyo karibu nae.
wewe umetembea vijijini au unasema tu mimi nimetembea maeneo mengi vijijini hata kama mtumishi asingekuwa na NHIF STILL ANGEKWENDA KATIKA VITUO HIVYO HIVYO VILIVYOPO MAENEO YALIYO KARIBU NAE. hapa tatizo sio NHIF tatizo ni vituo vyetu vyote vya serikali kuwa na huduma mbovu na ukosefu wa dawa na kuwa na uhaba wa vituo vingi vya binafsi vinavyoweza kumpa mtu uchaguzi.
mimi natumia jubilee card ukienda regency foleni ni ile ile huduma mbovu na majibu mabovu kutoka kwa wahudumu wa hospitali sote tunaipata sawa si wa NHIF,JUBILEE WALA AAR hakuna ubaguzi wowote unaofanywa.wote tunateseka tu ukiingia asubuhi unatoka mchana au jioni.
kuhusu green card unaongea usichokijua. jitahidi kujua green card ni kitu gani na utofauti wake na matumizi yake na upatikanaji wake. tafuta taarifa za kutosha ndio useme mambo mengine.