Nielewesheni; Magufuli alisema hatutafanya lockdown kwani nchi jirani zinategemea bandari zetu, nchi jirani zinazuia magari toka kwetu kuiingia kwao!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Mara nyingine nashindwa kuelewa kama mie ndio mwenye tatizo la kuelewa mabo au ni wale ninaowasikiliza wenye tatizo hilo.

Hap nyuma tuliambiwa kwamba hatutakuwa na lock down kwa ajili ya corona kwa kuwa nchi jirani zinatutegemea kuwafikishia bidhaa zao. Hata mifano ikatolewa ya Rwanda, Zambia, DRC na kdhalika.

Baada ya muda nikasikia kwenye mpaka wetu na Rwanda madereva wa malori toka Tanzania wanazuiwa kuingia nchini Rwanda kuwapelekea bidhaa zinazoingia kupitia bandari zetu. Na sasa nasikia Zambia nao wamefunga mpaka japo sisi tuko tayari kuwendelea kuwapelekea bidhaa zao zinazoptia hapa kwetu.

Hebu nielewesheni, kwa nini hawa jamaa wanafanya hivi wakati lengo letu ni kuwaonyesha roho yetu nzuri kwa majirani? Kwa nini hawatuelewi lakini? Hawaoni kwamba raisi wetu ana ufikirio sana kwao?
 
... wanachohitaji kutoka Tanzania ni bidhaa na huduma sio maradhi! Mkishaanza kuwapelekea maradhi hakuna mwenye akili timamu atakayekubali kuangamiza watu wake kwa maradhi kutoka kwa jirani kwa kisingizio cha bidhaa! Si kuna kanuni muhimu "jikinge na umkinge mwenzio?"; mbona kama nchi tumeshindwa kuitekeleza?
 
Do you know the meaning of self mwambafying?
Hii imenikumbusha enzi za utoto, unajifanya mbabe kila mtu anakuogopa na unakuwa tegemezi la wenzio, halafu siku moja tu anatokea bwana mdogo zaidi yako anakusulubu. Ndio hili lililotokea, kujijengea dhana ya kuwa tegemezi la wengine halafu hao unaodhani wanakuhitaji wanagundua kuwa wewe ni dhaifu tu.
 
Ndio ujue!!, Tanzania haijakuzuia kupeleka mizigo yako, unazuwiwa na mamlaka ya nchi nyingine, hasira zako zielekeze kwenye nchi uliyozuwiwa kuingia mkuu
 
Hii imenikumbusha enzi za utoto, unajifanya mbabe kila mtu anakuogopa na unakuwa tegemezi la wenzio, halafu siku moja tu anatokea bwana mdogo zaidi yako anakusulubu. Ndio hili lililotokea, kujijengea dhana ya kuwa tegemezi la wengine halafu hao unaodhani wanakuhitaji wanagundua kuwa wewe ni dhaifu tu.
Sasa sijui sisi tutasemaje tena...!
 
Mra nyingine nashindwa kuelewa kama mie ndio mwenye tatizo la kuelewa mabo au ni wale ninaowasikiliza wenye tatizo hilo.

Hap nyuma tuliambiwa kwamba hatutakuwa na lock down kwa ajili ya corona kwa kuwa nchi jirani zinatutegemea kuwafikishia bidhaa zao. Hata mifano ikatolewa ya Rwanda, Zambia, DRC na kdhalika.

Baada ya muda nikasikia kwenye mpaka wetu na Rwanda madereva wa malori toka Tanzania wanazuiwa kuingia nchini Rwanda kuwapelekea bidhaa zinazoingia kupitia bandari zetu. Na sasa nasikia Zmbia nao wamefung mpaka japo sisi tuko tayari kuwendelea kuwapelekea bidhaa zao zinazoptia hapa kwetu.

Hebu nielewesheni, kwa nini hawa jamaa wanafanya hivi wakati lengo letu ni kuwaonyesha roho yetu nzuri kwa majirani? Kwa nini hawatuelewi lakini? Hawaoni kwamba raisi wetu ana ufikirio sana kwao?
WHO wamewambia Nchi jirani endapo wataendelea kuwambukiza wananchi wao kwa makusudi kwa kuruhusu Raia wa Tanzania kuingia kwao watakosa pesa za kupambana na corona, WHO wana taarifa kuwa CCM hawataki kupambana na corona ndiyo maana wameruhusu watu wakae vijiweni vibarazani wabanane misikitini makanisani waambukizane kwa wingi wafe ili CCM wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu , WHO hawataki watanzania waambukizane Nchi jirani
 
... wanachohitaji kutoka Tanzania ni bidhaa na huduma sio maradhi! Mkishaanza kuwapelekea maradhi hakuna mwenye akili timamu atakayekubali kuangamiza watu wake kwa maradhi kutoka kwa jirani kwa kisingizio cha bidhaa! Si kuna kanuni muhimu "jikinge na umkinge mwenzio?"; mbona kama nchi tumeshindwa kuitekeleza?
Lakini hata hivyo, ilikuwa muhimu sana kwa Tanzania kuwa na mkakati wa pamoja na hizi nchi ukizingatia kuna suala la bidhaa zao kupitia kwetu. Sasa ajabu hatuna mawasiliano ya hivyo hata Museveni kasema hivyo. Mkutano wa SADC raisi wetu kasusia!
 
WHO wana taarifa kuwa CCM hawataki kupambana na corona ndiyo maana wameruhusu watu wakae vijiweni vibarazani wabanane misikitini makanisani waambukizane kwa wingi wafe ili CCM wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu
Makubwa haya! Lakini Zanzibar wameshasema uchaguzi utafanyika - sasa uchaguzi utafanyikaje Zanzibar na bara usifanyike?
 
Bado Kenya na Uganda..
Kenya uganda wanazuia watanzania wanakaa siku 14 mipakani wanapimwa sana, watanzania wamesuswa na Nchi Jiran baada ya kuona wabunge waziri na viongozi wengi wamekufa kwa uzembe tu
 
Back
Top Bottom