Nielewesheni Kuhusu 4G ya Voda!

Nielewesheni Kuhusu 4G ya Voda!

Mimi natumia MI 4LTE nayo kwenye 4g ya tigo wanasema haisapoti bali ya voda ikakubali ma mpaka sasa tigo siitumii kwenye 4g kwa sababu hiyo. Ni kweli yawezekana band wanazotumia ni tofauti.
Wanachotakiwa kukifanya ni kuwezesha simu zote zikawa na uwezo huo kama ilivyo kwa 3g
Vp kk..ulinunua wap hyo simu?na mm natafuta simu ya kampun hyo.
 
Mkuu pole kwa kukutana na kilaza mrembo...inshort ulikutana na bonge moja ya Kiazi kilaza afu nyeupe kichwani imejificha nyuma ya kidwati cha kastama kea
 
Tigo walipo Launch 4G walikua na Page ya kucheki simu yako kama ina support 4G kwa njia ya IMEI

Hivo unaweza kutumia IMEI kujua kama simu ina support 4G za bands fulani au la!

The issue is complicated ila ukienda pale customer care jiamini onesha evidence hata kwa ku google na kuwaonesha bands za simu yako na wao kama ni waelewa wanajua bands zinazotumika kwa mtandao wao watakubali tu.

Ila training wanayopewa ni feki sana...Mimi nilienda ku swap dada akaniuliza nimuonesha simu yangu cha ajabu eti akaenda settings>>>Mobile networks alipokuta LTE akaitumia kama criterion ya simu yangu ku support 4G ya Vodacom nkajua huyu amepotoshwa sababu simu inaweza kuwa na LTE huko ila iwe Bands kama 2300Mhz ambazo ni Smart tu wanatumia hapa home kwetu na si Voda.

Hivo knowledge side mbili inaitajika either kwa wewe unayeenda kununua line ya 4G pamoja na hao customer care kama wapo wanaopita hapa kusoma!
 
Mi Nafikiri hii huduma ya 4G itakuwa ya watu wachache sana kama inachagua simu na band wajaribu kujipanga upya kila mwenye simu ya 4G haweze kutumia kama ilivyo 3G lasivyo itakuwa ni lawama tu.
 
Mi Nafikiri hii huduma ya 4G itakuwa ya watu wachache sana kama inachagua simu na band wajaribu kujipanga upya kila mwenye simu ya 4G haweze kutumia kama ilivyo 3G lasivyo itakuwa ni lawama tu.
lipo nje ya uwezo wao. tatizo kubwa ni wafanya biasahara wetu wanaopenda kukomba simu used za kimarekani ambazo 4g zake ni tofauti
 
Juzi nilimua kwenda Mlimani City kwenye Duka la Voda kwa ajiri ya Kuswap line yangu ya Voda kwenda kwenye 4G kama wao wanavovyesema! Lakini Before Nilisha enda K/koo pale Msimbazi kwenye Duka la Tigo niliswap line yangu kwenda 4G bila longolongo!

Pale Mlimani city nilifika kwa yule muhudumu wao alikuwa wakike akasema nipe simu yako nikampa,akasema nipe IMEI number ya simu yako nikampa! Alivyo angalia akasema Simu yako haina LTE! Nikamuuliza kivipi akasema hiyo simu yako haisupport 4G nikashangaa kidogo

Nikamwambia mbona line ya Tigo ipo humu na inasoma 4G na simu yangu nikiangalia inanionesha inasupport 4G? Akasema hiyo 4G ya tigo mnadanganyana hiyo siyo 4G! Nikasema mimi sijakuelewa kabisa akasema njoo uone akanionesha kwenye Computer Message from TCRA baada ya kuhakiki simu yangu kwa kuingiza IMEI number ikaleta ujumbe ule ule wa siku zote wa kuhakiko simu! Yaani ikaletea aina ya simu HTC M9 na ndio aina ya simu yangu lakini yule dada akasema eti niibadirishe before June simu yangu sio geunie! Tena kwa Dharau kabisaa! Nikasema huo si ujumbe wa kawaida tuu wa TCRA hauhusiani na 4G? Mbina hiyo june simu yangu haijazimwa sasa akasema using'ang'anie simu yako haisupport 4G,nikaamua kuondoka!

Sasa Najiuliza maswali haya naombeni mnisaidie

1.Je ni kweli HTC M9 haisupport 4G? Au ni 4G ya Voda tuu?

2.Na Je ule ujumbe Wa TCRA unahusika katika kujua kama simu inasupport 4G au Vipi?

3.IMEI number inahusika vipi katika 4G? Mbona tigo sikuombwa hata IMEI number zaidi ya namba yangu ya simu na wakabadirisha haraka?

Hili la voda wataalamu limekaaje
Kama bado aujafanikiwa nenda Voda ya samora Avenue.. Pale kuna watu wa IT wazuri (sijui kama bado watakuwepo wale wale).. Pale nilifika nikaja za form, nikaenda kwenye desk yule mdada akaniuliza "unasimu yako hapo" nikasema "ndio ninayo" bila maswali mengi akanipa line nikaenda kwa hao ma IT wao pembeni , akaikata, akaiweka kwenye simu.

Bila maswali mengi fasta tu, nikapata 4gb zangu nikaondoka ..
 
Back
Top Bottom