Dusabimana
JF-Expert Member
- Oct 24, 2019
- 278
- 246
Kama kichwa habari hapo juu kinavyosema. Hivi hamuoni kuwa mnasababisha usumbufu kwa kubandika namba za NIDA za Wilaya nzima eneo moja tu. Watu wasafiri toka Vijijini kuja Mjini kuangalia namba za usajili wao, kwa kulipia nauli! Mfano kutoka Kagerakanda, Asante Nyerere, Makere na huko kwingine, nauli ndani ya Gari ikiwa chini ni 5000 au 7000 kwa Mtu mmoja, hapo nikuja Mjini bado kurudi! Bado Msongamano utakao kuwepo hapo Community Center mlipo bandika hizo namba!
Mbaya zaidi namba zimebandikwa ndani ya Compound ambayo ina kieneo kidogo. Leo jion tu ilikuwa ni varangati kwa Watu waliopo hapa Mjini, wakati wakitafuta namba zao, kuanzia kesho si ndo itakuwa kizaa zaa! Mmeshindwa kitu gani kwenda kubandika hizo namba Vijijini na kwenye Mitaa Watu walipo jiandikishia?! Mwaka jana wakati Wananchi wa Kata ya Murusi pekee tu wakipeleka fomu zao za NIDA pale community Center.
Mama mmoja aliyekuwa ana Mtoto Mgongoni bahati mbaya alianguka chini akakanyagiwa chini kwaajili ya Msongamano na Mtoto akapoteza Maisha! Bado hamjifunzi kitu hapo.Badilikeni nasiyo kufanya mambo hovyo hovyo utadhani bado tupo enzi za Ujima. Magari yapo, Barabara zipo.
Pelekeni hizo namba Vijijini na kwenye Mitaa.