NIDA, mbona wageni wana vitambulisho na sio namba?

Ni mambo ya kushangaza sana
 
Kuna mchina mmoja alikuja ofisi X akitaka huduma alikuwa na NIDA CHETI CHA KUZALIWA vyote vinaonyesha ni mtanzania mwenzetu, ila sasa shida ikaanza kwenye kuongea kiswahili
 

NIDA ilimshinda hadi Hayati Magufuli, hawa wengine waliobaki hawana hata uwezo wa kuitikisa wala kuihoji bora hata angekuwepo Magufuli labda mtu wa 2018 angepata 2024

Kwa hali ya sasa huyo wa 2018 aachane na mambo ya NIDA afanye mambo mengine kama hana hela.

Hatusemi kwa ubaya, sote tunajua namna tunavyoishi na hao Maafisa wa NIDA ni wabongo wenzetu mtaani
 
Kuna mchina mmoja alikuja ofisi X akitaka huduma alikuwa na NIDA CHETI CHA KUZALIWA vyote vinaonyesha ni mtanzania mwenzetu, ila sasa shida ikaanza kwenye kuongea kiswahili
Kwani hakuna Watanzaia ambao hawajui Kiswahili? Kuna raia wa kuandikisha na kurithi ambao wana toka nchi mbalimbali.
 
Mbona juzi tu Waziri Masauni kazindua ugawaji wa ID Musoma na kuahidi kuwapa wote mwaka kesho?
 
Mbona juzi tu Waziri Masauni kazindua ugawaji wa ID Musoma na kuahidi kuwapa wote mwaka kesho?

Yeye sio Waziri wa kwanza kuhudumu Mambo ya Ndani na kuahidi kumaliza tatizo la NIDA.

Soma upya NIDA alichemka Magufuli hawa waliobaki utasikia ahadi sana na zitabaki ahadi tu.
 
Yeye sio Waziri wa kwanza kuhudumu Mambo ya Ndani na kuahidi kumaliza tatizo la NIDA.

Soma upya NIDA alichemka Magufuli hawa waliobaki utasikia ahadi sana na zitabaki ahadi tu.
Duuh naona imani hakuna kabisa kwa NIDA na hii ndio inafanya hata watu wasifuatilie Vitambulisho vyao wakati vingine vipo tayari.
 
Tanzania inakosa taasisi imara za utendaji na usimamizi, zikiongozwa na ile nyeti ya urais. Zote zimejaa ubinafsi, ubabaishaji na wizi wa kutupwa.

Kama nchi huru hatukaweza kabisa kujenga taasisi imara, badala yake imeja mifumo ya wizi na ufujaji wa mali za umma . Wezi wote wakubwa kwa wadogo wamejificha chini ya mwamvuli wa ukada wa CCM.
 
Kalagaboho....penyeza rupia, kwani wewe ni mgeni na nchi hii?
 
Mimi mtanzania leo karibia natimiza miaka 10 ya kuwa na namba za NIDA ila sio kadi.

Halafu wahindi, waarabu na wakenya kibao ambao ni wageni Wana kadi za NIDA.

NCHI HII SISI WATANZANIA TUNAIHARIBU WENYEWE.
 
Nadhani huu ni ukweli mchungu!!!!!
 
Wageni wakaazi wanapokuja nchini hupata kibali (working permit) ya miezi sita tu, hivyo kwa vyovyote vile ni lazima wapewe vitambulisho vya Mgeni Mkaazi kabla ya muda huo wa kibali chake hakijakwisha muda wake. Lakini pia Kitambulisho cha Taifa anachpoewa raia huyo wa kigeni kina ukomo tofauti na raia mzawa ambaye Kitambulisho chake cha uraia hakina ukomo. Aidha, idadi ya wageni wanaoomba vitambulisho vya Taifa kwa category yao ni wachache sana si zaidi ya 50,000 ukulinganisha na mamilioni kwa mamilioni ya raia wazawa, na hawa wageni wana aina yao tofauti ya Vitambulisho. Hivyo si kweli kwamba kuna upendeleo kwa wageni hakuna kitu kama hicho.

Kuhusu rushwa, ni vema tukaelewa kuwa unapojisajili kwa mara ya kwanza huduma yote ya usajili mpaka kupata Kitambulisho ni BURE hakuna malipo yeyote. Kama mtumishi wa NIDA anakuomba rushwa na una uhakika kabisa kuwa ni Mtumishi wa NIDA na una ushahidi wa kuombwa hiyo rushwa naomba tutoe taarifa TAKUKURU au kwa uongozi wa NIDA ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika. Tusilalamike tu bila sisi wenyewe kuchukua hatua lakini pia na sisi tusikubali kutoa rushwa, na ni vema pia tufahamu wako matapeli wanaojifanya ni watumishi wa NIDA wakati siyo, tunawapa pesa sisi wenyewe wakitupiga tunaanza kuwalalamikia NIDA, hatutendi sawa, hebu sisi wenyewe tusaidie mapambano dhidi ya rushwa kwa kukataa kutoa na kutoa taarifa.

Tatizo la watu ambao hawajapata vitambulisho vyao tayari imekwisha tangazwa rasmi kwamba Vitambulisho vimeanza kuzalishwa kwa wingi, kusambazwa na kugawiwa kwa wingi kwa wananchi wenye namba za Utambulisho. Zoezi la ugawaji Vitambulisho kwa Umma limezinduliwa hivi karibuni Musoma mkoani Mara, hivi sasa Vitambulisho vinaendelea kugawiwa kwa watu wote wenye namba katik awilaya zote za mkoa wa Mara, Wilaya zote za mkoa wa Mtwara, Wilaya zote za mkoa wa LIndi, Kigoma na Kagera. Baada ya hapo itafuata mikoa mingine hatua kwa hatua na wamesema bayana kuwa mpaka kufikia Machi 2024 wote tuliosajiliwa na kupata Namba tutakuwa tumepata Vitambulisho vyetu.

Jambo muhimu sana kuelewa ni kwamba Kilicho muhimu sana ni mtu kuwa na Utambulisho wa Taifa yaani umesajiliwa na kupata Namba yako ya Utambulisho wa Taifa ambayo hiyo ndiyo inatumika kukutambulisha na kukuwezesha kupata huduma yeyote hata kama huna Kitambulisho (Kadi). Kitambulisho au Kadi kama wengine wanavyokiita ni end product lakini Utambulisho halisi ni namba yako.
 
Seconded, ufafanuzi na udadavuzi wa kina, na Mimi hiki ndicho ninachokifahamu asante sana. Wenzetu Kenya wathamini sana Huduma Namba si Kitambulisho.
 
Uyu jamaa wa NIDA msimsikilize[emoji16][emoji16]
 
Jambo lingekuwa rahisi sana kama vitamvulisho vya NIDA ndo vije kutumika kupigia kura utaona kama raia kama hawapati ID
Kutumia Vitambulisho vya Taifa kupiga kura ni moja ya matumizi yake nimesikia kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…