NIDA-Kwa nini msiwezeshe maombi ya online?

kizito2009

Senior Member
Jan 6, 2010
172
223
Mimi binafsi nincho kitambulisho cha TAIFA ila baada ya kufikiri nimeona kwamba kwa sababu tayari tunao uwezo kuomba Passport online kwa nini mifumo ya NIDA isibadilishwe kumwezesha mtu kuomba kwa njia ya online na kisha taratibu za uthibitisho na kukusanya kitambulisho ndo ziwe manual.Hii itawezesha mtu kupata namba ya kitambulisho iwapo amekidhi vigezo.Ukusanyaji wa nyaraka nyingine unaweza kufanyika kwa utaratibu uliopo ila yale mambo ya kawaida yafanyika online.

Hii itawezesha kupunguza ucheleweshaji unaotokana na kupotea kwa fomu
 
Natamani hyo kitu ingewezeakana ila hii nchi urasimu ni mwingi sana kias kwamba mambo meng yanakwamishwa.
 
Watakula wapi..!!
Bongo vitu vingi vinaachwa hovyo ili kuruhusu mianya ya upigaji, na hii inachagizwa na hali ya wananchi wengi kutokuwa na uelewa.... tunasubiri tamko.
 
Napenda kutoa malalamiko yangu kwa Nida , hebu punguzeni urasimu wa vikwazo vya utoaji wa vitambulisho. Kweli Mzee wa miaka 73 ana kitambulisho cha kura, cha mkazi Lin anaambiwa alete cheti cha kuzaliwa? Na hakuwahi kufanya kazi kazaliwa kijijini , Wazazi wake wameshafariki, tarehe za kuzaliwa Wazazi wake na yeye mwenyewe kajaza vizuri. Kweli huku Moshi tunapata shida kupata vitambulisho vya Taifa.

Back
Top Bottom