Mchokozi Huru
Member
- Apr 17, 2016
- 7
- 5
Tuje tarehe gani sasa?NIDA na Tangazo lake la kisanii kwa waliokua wafanyakazi wa Mikataba.
Tarehe 13 waliitwa kupitia nitangazo lililochapishwa kwenye gazeti la mwananchi la tar 11/04/2016 kwamba wafike BMTL kwaajili ya kulipwa, lakini leo tar 18/04/2016 wamekuja na tangazo la kuendelea na uhakiki wa nje ya NIDA.
Hapa kuna usanii
View attachment 340308
Ni tatizo kubwa sana mkuu, hapa kuna UONGO unaendelea, KAIMU MKURUGENZI amekua akiudanganya umma kwa njia ya media. Leo Watanzania wanajua wale watu wamelipwa, lakini kiuhalisia bado wanahakikiwa. Ni bora tangazo la awali kupitia gazeti la Mwananchi lingeweka wazi kwamba kutakua na mazoezi mawili, la kwanza ni uhakiki wa ana kwa ana na wa pili ni wa vyombo vingine vya serikali ili kuthibitisha uhalali wa malipo. Ila kama mtu alifanya kazi na anakudai miezi mi3 huna budi kumlipa kwanza stahili yake hiyo.Mmmh!NIDA nao ni tatizo kwakweli.
Tangazo lake halijaweka wazi, nadhani mngempigia simu awaeleze lini mkachukue chenu. Sio haki wala busara kwa kinachoendelea kufanyika na kiongozi huyo mwenye chembe chembe za udikteta.Tuje tarehe gani sasa?
Kwa uelewa wangu wa kawaida hapo kuna wengi lazima wameingia garama zisizo za lazima, kuna aliyesafiri kutoka mkoani au visiwani kuja kufata malipo kisha akakutana na zoezi tofauti, hawezi kurudi kwa wakati kwa sababu hajui lini ataitwa tena. Kuna walioacha ishu zao nyingine lakini wanakutana na kitu tofauti. Ieleweke kwamba zoezi la uhakiki ni zuri na lina tija, lakini kitendo cha kuwadanganya hakiko sawa. Huwezi ukawa unaenda sokoni halafu ukaaga kwa rafiki zako kwamba unaenda kanisani, hiyo sio busara. Mheshimiwa Rais Dr. John P. Magufuli anatakiwa aelewe kwamba kuna watumishi wake wanawanyanyasa sana watu walio chini yao.Daaah ama kweli hapa kazi tu....yule mkurugenzi wao anavyojifaraguaga kwenye migazeti na tv hadi leo wale watoto hawajalipwa??wana maisha magumu sasa hivi masikini ila mheshimiwa raisi ni msikivu sana hapa kuna tatizo km siyo jipu basi wasisumbue hao vijana waseme tu hamna chenu wakalime.
Sure! Kuna janja inataka kufanyika hapo.YANI HAPO KINACHOONEKANA KUNA KITU KINAENDELEA NYUMA YA PAZIA AMBACHO INAWEZEKANA ALIYEAMURU WALIPWE HAJUI MAANA UKIANGALIA KWA UMAKINI HILO TANGAZO HALINA SAINI NA WALA HALINA TAREHE KUA LIMETOKA LINI INAOKEKANA HAPO WAMETOA TANGAZO NI KAMA FUNIKA KOMBE@%$#@@%APITE CHA KUFANYA HAPO VIJANA KOMAENI MPAKA KIELEWEKE MAANA.MPAKA WAMETOA MATANGAZO YA KULIPA INAMAANA HELA WANAZO ILA KUNA WAPIGAJI WACHACHE WANATAKA KUFANYA YAO HAPO.. VIVA VIJANA WA NIDA POLENI KWA YOTE.