NIDA Kusogeza mbele Malipo ya waliokua watumishi wake 597 wa mikataba

Mchokozi Huru

Member
Apr 17, 2016
7
5
NIDA na Tangazo lake la kisanii kwa waliokua wafanyakazi wa Mikataba.
Tarehe 13 waliitwa kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti la mwananchi la tar 11/04/2016 kwamba wafike BMTL kwaajili ya kulipwa, lakini leo tar 18/04/2016 wamekuja na tangazo la kuendelea na uhakiki wa nje ya NIDA.
Hapa kuna usanii

IMG-20160418-WA0003.jpg
 
NIDA na Tangazo lake la kisanii kwa waliokua wafanyakazi wa Mikataba.
Tarehe 13 waliitwa kupitia nitangazo lililochapishwa kwenye gazeti la mwananchi la tar 11/04/2016 kwamba wafike BMTL kwaajili ya kulipwa, lakini leo tar 18/04/2016 wamekuja na tangazo la kuendelea na uhakiki wa nje ya NIDA.
Hapa kuna usanii

View attachment 340308
Tuje tarehe gani sasa?
 
Mmmh!NIDA nao ni tatizo kwakweli.
Ni tatizo kubwa sana mkuu, hapa kuna UONGO unaendelea, KAIMU MKURUGENZI amekua akiudanganya umma kwa njia ya media. Leo Watanzania wanajua wale watu wamelipwa, lakini kiuhalisia bado wanahakikiwa. Ni bora tangazo la awali kupitia gazeti la Mwananchi lingeweka wazi kwamba kutakua na mazoezi mawili, la kwanza ni uhakiki wa ana kwa ana na wa pili ni wa vyombo vingine vya serikali ili kuthibitisha uhalali wa malipo. Ila kama mtu alifanya kazi na anakudai miezi mi3 huna budi kumlipa kwanza stahili yake hiyo.
 
Daaah ama kweli hapa kazi tu....yule mkurugenzi wao anavyojifaraguaga kwenye migazeti na tv hadi leo wale watoto hawajalipwa??wana maisha magumu sasa hivi masikini ila mheshimiwa raisi ni msikivu sana hapa kuna tatizo km siyo jipu basi wasisumbue hao vijana waseme tu hamna chenu wakalime.
 
Kwa uelewa wangu wa kawaida hapo kuna wengi lazima wameingia garama zisizo za lazima, kuna aliyesafiri kutoka mkoani au visiwani kuja kufata malipo kisha akakutana na zoezi tofauti, hawezi kurudi kwa wakati kwa sababu hajui lini ataitwa tena. Kuna walioacha ishu zao nyingine lakini wanakutana na kitu tofauti. Ieleweke kwamba zoezi la uhakiki ni zuri na lina tija, lakini kitendo cha kuwadanganya hakiko sawa. Huwezi ukawa unaenda sokoni halafu ukaaga kwa rafiki zako kwamba unaenda kanisani, hiyo sio busara. Mheshimiwa Rais Dr. John P. Magufuli anatakiwa aelewe kwamba kuna watumishi wake wanawanyanyasa sana watu walio chini yao.
 
YANI HAPO KINACHOONEKANA KUNA KITU KINAENDELEA NYUMA YA PAZIA AMBACHO INAWEZEKANA ALIYEAMURU WALIPWE HAJUI MAANA UKIANGALIA KWA UMAKINI HILO TANGAZO HALINA SAINI NA WALA HALINA TAREHE KUA LIMETOKA LINI INAOKEKANA HAPO WAMETOA TANGAZO NI KAMA FUNIKA KOMBE@%$#@@%APITE CHA KUFANYA HAPO VIJANA KOMAENI MPAKA KIELEWEKE MAANA.MPAKA WAMETOA MATANGAZO YA KULIPA INAMAANA HELA WANAZO ILA KUNA WAPIGAJI WACHACHE WANATAKA KUFANYA YAO HAPO.. VIVA VIJANA WA NIDA POLENI KWA YOTE.
 
Sure! Kuna janja inataka kufanyika hapo.
 
Duh nyie viongozi kuweni na Huruma mbona mnasumbua watu kiasi hicho wape watu stahiki zao waondoke uongozi mnatumia vibaya Mnaamua lolote mtakalo muwe na Huruma jueni haki ni kitu gani
 
Hapa shida ni uongozi ambao haujali hata kidogo ubinadamu. Watu wamefanya kazi, na ushahidi kuwa walikuwepo Kazini kisheria upo, jamani kigugumizi cha nini katika kuwapa stahiki Zao? Mkurugenzi mpya hana utashi wa kuwalipa hawa watu, lakini akumbuke kuwa yeye sio Mungu, Leo ana nafasi na anatamba na kuwanyanyasa hawa wafanyakazi tena wa hali ya chini kabisa ambao kwa sasa wanataabika mtaani, Mungu anayemtumika IPO siku atamshusha na kumwonjesha machungu ili ajue kuwa Mungu ni watu wote. Sio rahisi MTU kama Mkurugenzi tena swahiba wa mwenye nyumba kuota kupata shida hata siku moja lakini Hata Sadam Hussein alikuwa Rais tena mwenye nguvu kubwa....
 
Back
Top Bottom