Nichukue hatua gani hapa?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,597
1,810
Wadau, habari za jioni?
Naombeni ushauri wenu katika hii ishu kuna binamu yangu mtoto wa shangazi yangu anataka kunifanyia uhuni kwa Girlfriend wangu.
Nina Mpenzi wangu ambaye tumeanza kuwa na mahusiano kama miezi minne sasa baada ya kuwa marafiki wa muda mrefu, nilijuana na huyu binti tangu akiwa kidato cha pili mpaka amemaliza kidato cha sita mwaka tulikuwa tukiwaasilana na kutembeleana kila alipopata likizo mpaka sasa tumejikuta tupo katika uhusiano.
Nimeandika thread hii kuomba ushauri wenu kabla ya kutaka kuchukua maamuzi yangu binafsi, kifupi, nina binamu yangu ambaye huwa namchukulia kama kaka na rafiki yangu wa damu lakini kwa kitendo alichofanya jana amenichefua na nimemuona hafai..
Kwa kuwa namchukulia kama rafiki sikuweza kumficha kuhusu Girlfriend nikampa mpaka namba za simu na kuna siku tulienda pamoja mpaka kwa Girlfriend wangu na akaonana nae, kwa hiyo tangu siku hiyo wamekuwa wakiwasiliana kila mara na huwa wanataniana sana, GF wangu ni Mcheshi na ni muongeaji na anamchangamkia kila mtu hata binamu yangu na yeye ni muongeaji na anapenda sana utani...
Jana usiku kampigia GF wangu simu akawa anamwambia ni lini atakuja Dar? Anataka kuonana nae lakini asiniambie mimi na akija atachukua hotel wataspend the whole night pamoja.
GF wangu alichomjibu akamwambia hawezi kuja dar bila mimi kupata taarifa.. na akazidi kumwambia kwa sasa uwezekano wa kuja Dar ni mdogo kwani tarehe 3 October anaenda Chuo Iringa Tumaini. Kwa hiyo hawezi kuja na kama akija basi atakuja kwa sababu maalum.
( GF WANGU KWA SASA YUKO KWA BIBI NA BABU YAKE MOSHI)
MAZUNGUMUZO HAYA GF WANGU ALIKUWA ANAYAREKODI NA AMENITUMIA SOUND CLIP KWENYE EMAIL.
Alilazimika kurekodi na kunitumia baada ya kuona jamaa anaanza kuongea ishu ambazo sizo, na GF wangu hajapendezwa na hili jambo kabisa.
Inshort Binamu yangu ana motto wa kiume ana miezi alizaa na msichana wakati wakiwa chuo huku Malaysia.
Kwa kweli alichokuwa anakiongea huyu jamaa kimenisikitisha na kimenifanya nimuone mshenzi wa tabia na ambaye hafai katika jamii sasa nifanyaje??/
Nilichokuwa nimepanga:-
1. Nimemwambia shangazi ambaye ni mama yake au dada yake
2. Nimchane live
3. Nimwambie mke wake ambae amezaa nae na ikiwezekana nimpelekee na ile Sound clip asikilize
4. Au niwambie washikaji zake ili wampe live.
Lakini kabla sijachukua haya maamuzi nikakumbuka kuna wadau wa MMU naomba ushuri wenu wadugu kabla sijaamua kuchukua hayo maamuzi n iliyotaja hapo juu, ingawa najua yatasababisha mahusiano yetu kuwa mabaya...
Please advice wakuu:
Note: my cousin- 27 years. Me 24(kesho) and my GF is 21

Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
26,493
37,619
Si tayari girlfriend wako ameshaonyesha hana muda nae?!MPOTEZEE.

Au mjulishe tu kwamba unajua madudu yake na hujayafurahia.

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,136
4,118
M face mwenyewe na umueleze unajua anachofanya na hujapenda. Next time uwe makini nae maana umeshamfahamu tabia yake sio.

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,219
91,806
Ukimshtakia kwa mama yake
trust me...utamuongezea ujiko..ingawa ni ujinga..

Wamama wakilietewa kesi za watoto wao wa kiume kutongoza
mioyoni huona sio kesi kabisaaaa
ingawa mbele za watu atajifanya kakasirishwa lol

BlackBerry

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
1,839
948
Du pole sana rafiki yangu, mie nachokushauri mwambie tu kwamba unajua kwamba anamtaka GF wako, then baada ya hapo we mchangamkie kama kawaida, ila mwambie iwe mwanzo na mwisho kuwasiliana nae,kwa upande wa msichana hadi kuchukua clip du hapo alienda mbali, mie ningekuwa huyo msichana ningemchana huyo jamaa na kumwambia akirudia tena nakwambia asingeendelea kumtongoza, pole sana yamalize kiutu uzima

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,718
1,378
Mwambie gf wako ajifunze kukabiliana na mitongozo. Huko chuo anapoenda atakuwa anakushtakia kila anapotongozwa?
Namsikitikia Manyanza mpaka huyo binti anamaliza chuo anaweza kupata ugonjwa wa moyo,vitu vingine amalize mwenyewe bana-huo muda wa kurekodi mpaka maongezi duh!

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,899
3,390
mkuu kwa jinsi navyokuona kwenye avatar najua wewe ni mature"kama hiyo avata ni wewe"
mambo ya relationship na wanawake kwa ujumla jifunze sana kupotezea la sivyo utakonda mkuu!!

OTIS

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
2,237
799
Taratibu mkuu usije ua mende kwa nyundo.
Mwambie gf wako amwambie jamaa kuwa tayari ameshamsemea kwako kwa usumbufu anaomletea.
Na wewe usimfuate jamaa baada ya hapo hadi pale ukiona amezidi.

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,597
1,810
Si tayari girlfriend wako ameshaonyesha hana muda nae?!MPOTEZEE.

Au mjulishe tu kwamba unajua madudu yake na hujayafurahia.

nimekusoma Lizzy, halafu huyu cousin yangu ana mtoto na lakini tabia zake ni mbovu tu. Naendelea kupata maoni ya wadau

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,597
1,810
mkuu kwa jinsi navyokuona kwenye avatar najua wewe ni mature"kama hiyo avata ni wewe"

mambo ya relationship na wanawake kwa ujumla jifunze sana kupotezea la sivyo utakonda mkuu!!

its me kwenye avatar mkuu, siumii na chochote mkuu lakini kumbuka huyu jamaa ni binamu yangu damu na kumnyamazia tu haifai ndio maana nipo hapa kupata maoni nini cha kufanya.

SaraM

Senior Member
Sep 8, 2011
162
109
Kwa kweli msichana mwenzetu hapo amechemsha, hatusemeagi huwa tuna deal nao na kuwaonyesha misimamo kwa kuwatolea macho, sio kuwa entertain kuwaongelesha weeee ili waongee zaidi na tuwarekodi, hapana. nakushauri hata usimuulize ndugu yako ili mradi ushajua

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Mwambie gf wako ajifunze kukabiliana na mitongozo. Huko chuo anapoenda atakuwa anakushtakia kila anapotongozwa?

Heheheee ajifunze kukabiliana na Mitongozo sio??, kuna Matongozo mengine Makubwa yanaweza kumshinda umri.

Peter lilayon

Member
Aug 13, 2011
52
7
Mwanamke asikugombanishe na ndugu rafiki mwambie Gf wako ampotezee, na wewe mpoteze. Huyo gf 2 mwanangu?. unawewaza kugombana na ndugu kisa mwanamke akaja akakutenda huku umegombana na ndugu ukakosa pa kukimbilia. Mwambie huyo demu ndo amuambie c wewe we mwanaume bwana acha usamba

Gaga

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,562
1,941

its me kwenye avatar mkuu, siumii na chochote mkuu lakini kumbuka huyu jamaa ni binamu yangu damu na kumnyamazia tu haifai ndio maana nipo hapa kupata maoni nini cha kufanya.
Manyanza mdogo wangu,nakushauri mwache tu, haifai kugombana na ndugu yako kwa swala kama hilo, haya mambo yapo ila shukuru msichana amekuwa na msimamo, ila kukwambia ndio kachemsha nahisi, sidhani kama ni jambo la busara kugombanisha ndugu,kwani msichana kasisitiza umwambie?

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Ndugu ni ndugu huwezi gombana nae. Lakini kumbuka kuwa hata mwanamke ukishamuoa anakuwa na thamani kama ndugu au zaidi ya ndugu.

Ushauri wangu ni kuwa wala usimface huyo ndugu yako ila cha msingi kuwa nae makini saaana. Nasema hivyo kwa kuwa huyu mdada amemtolea nje na yawezekana mdada asiwe girlfriend wako wa mwisho; ila kukupa taharifa imekusaidia kujua what your cousin is capable of. Kuna ma player wana ethics na wanajua limits. Kuna wasio na limits. Jamaa atakuwa na katabia ka kuwinda wasichana wa wenzie ndio hao wanaozaa na wake za ndugu zao.

Keep a big distance from your so called cousin other wise akikwaa maugonjwa yake mnaondoka familia nzima. Who knows kama atakuwa anatolewa nje na wasichana wako wote? Who knows kama hajawahi kukumegea wasichana wako walopita??? Shukuru kwa taharifa kwani imekupa tahadhari no matter whether alichofanya mdada ni right au ange keep it as secret. Kwangu mimi si kila kitu ni worth to be called siri. Ikifichuka usingeamini kuwa alimtolea nje jamaa.

Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
We mchane live ajue kabisa kuwa madudu yake anayoyafanya sio issue na umeshayagundua. We mpaka gf wako kakwambia ujue yamemshinda!

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

5 Reactions
Reply
Top Bottom