Niambie utapenda ukute nini

hongera sana.umefanya jambo nzuri sana kutaka kujua kutoka kwa wateja wanahitaji nini. mimi nitakushauri kwa ujumla.
Ok. kwanza uwe na variety ya kutosha ya vitafunwa sio unakuta maandazi na chapati tu.
same kwa mchana, sio unaenda kwa mama ntilie unakuta ana wali nyama na ugali tu.
2. hakikisha vyakula vinakuwepo kwa muda mrefu na viwe vya moto ,sio unaenda saa 9 chakula kimeisha au unakuta cha baridiii.
3. usafi, hakikisha hakuna vyombo vinazagaa hovyo sio banda limejaa nzi na mimajimaji isiyoeleweka .
4. usafi wa wafanyakazi wako pia, wavae vizuri na wawe wasafi ,itapendeza wakivaa epron zile nyeupe.
5. kama huna huduma za vinywaji basi viwepo jirani na wewe.
6. wewe na wafanyakazi wako wawe na kauli nzuri kwa wateja wako.
7. kuwa mbunifu wa vyakula au mixers ambazo wengine hawana .
 
Asante sana, napata darasa ili nifanye vz zaidi ,ukifika usiboreke.
Karibu sana
 
Najitahidi .asante
 
Dah,Asante sana,madini ya kutosha .natamani nikualike one day kwa kweli, umenigusa zaidi .thanx
 
Sehemu nikikuta chapati na maharage kwa bei fair hapo lazima patanihusu. Chapati moja 300 maharage bakuli 500.

Nafikiri watu wengi wataafford hii.
 
Sehemu nikikuta chapati na maharage kwa bei fair hapo lazima patanihusu. Chapati moja 300 maharage bakuli 500.

Nafikiri watu wengi wataafford hii.
Umenichekesha kweli kwani umenikumbusha mtindo wa Dar wa kula maharage asubuhi. Halafu watu wengine wanaweka sukari. Du! looong time na-mis this stuff.
 
Mtori na mishikak ya nunduπŸ˜‹
 
Kwenye biashara ya chakula inataka ubunifu hasaaaa.Mara nyingi mtu anaweza pika varieties ila visiwe na kiwango cha kuridhisha wateja yeye ilimradi kapika vingi.
Nafikiriaga ungekua na vyakula aina 2 au 3 unavyoviewezea hasaaaa ,unaivipika vizuri so hata mtu akitaka maybe ndizi nyama au pilau anajua yours is the best.
Kariakoo sokoni kuna restaurant wanauza Ndizi Nyama tuuu japo wana aina nyingine lakini ndizi nyama ndio trademark yao na wapo vizuri.
Waweza fanya hivyo ukajitofautisha na wengine

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…