Niachieni CCM yangu

yaani nikiambiwa ni chague kati ya kifo au CCM nachagua Kifo. CCM ni kifo cha mateso na mahangaiko
 
Ni kweli imetutoa mbali,imetutoa kwenye neema na kutupeleka kwenye umasikini mkubwa,na bado inaeendelea kutoa ajira kwa vijana badala ya kuwapa.We endelea tu na ngonjera zako siku ikifika ndo utajua kilichomtoa kanga manyoya.
 
kama huwezi kubaliana na mimi..nenda sehemu yoyote like Kariakoo,Karume afu jaribu kuongea Loud kua we ni CCm,jaribu kuwadanganya kwa maendeleo yalioyafanya...kama autarushiwa mawe..hawa watu wanasema wamejivua gamba,hata nyoka huwa mbona anajivua...Mi sidanganyiki tenaaaaaaaaaa.!
 
we, we, we, we chunga sana nimeongea upupu mimi!!!! CCM ndio chama pekee kinachoweza kuiongoza nchi hii. Bila CCM hakuna nchi bwana. uko hapo?

Mataahira ni wengi dunia hii! Hili nalo limo

CCM nyoka tumwondoe,
Hata gamba aondoe,
Lazima na tumwondoe,
Sumuye kali mwondoe.
 
Hivi watu wa Tanzania mbona hamna shukurani? CCM imekutoeni mbali, kumbukeni CCM imezaliwa na TANU na ASP, kwa hiyo Bila CCM watu wa bara na visiwani msingepata uhuru.

Mazuri yote mnayoyaona yanatokana na CCM, elimu uliyonayo ni CCM, maisha yako ya zamani na sasa ni CCM, uhuru wa kuongea, kuabudu na vyombo vya habari ni CCM, jamani mbona mnalaumu uongo?

Kumbukeni hata hivyo vyama vyenu vya siasa mnavyoviita upinzani bila CCM visingekuwepo. Loh! niachieni CCM yangu.

Watu gani nyie msio na shukurani, baba ni baba tu, hata siku moja bega halizidi kichwa hata kama linaonekana ni kubwa. TCCM tutashinda siku zote na miaka yote.

Nawasilisha.

Kwa nini vyama vingi vilizuiwa miaka michache baada ya uhuru? Kwa nini akina marehemu Oscar Kambona walikimbilia uhamishoni? Uhuru uliopatika si wa kisiasa tu? History haisemi kuwa wakoloni waliamua kutoa uhuru?
 
Watu wengine bwana mnaniacha hoi kabisa,Mnang'ang'ana na ccm inayowanyonya WTZ,ustaarabu wa kiungwana ni kwamba nguo ikichanika unabadili nyingine iliyochanika weka kando,sasa ccm tuiweke kando tuvae CDM,au siyo.
 
CCM HAKITENDI HISANI KWA MTU YEYOTE NCHINI BALI NI KODI ZETU TU: HATA TLP YA MZEE MREMA KINGALIKUAPO ENZI HIZO YOOOTE HAYA YANGEFANYIKA

Acha kelele na vioja hapa kwani hapa ni hoja tu!!!

Hayo yoote hayakuwa HISANI kwetu bali ni kwamba yalikua niwajibu wa CCM kutekeleza hayo yoote kwa kutumia kodi zetu vema na sasa wajibu huo umesalitiwa vibaya mno na kila kitu ni TAFUNA TAFUNA kwa kwenda mbele kati ya ndugu, jamaa na marafiki wa wakubwa chama hicho.!!!!!!!!

Hivyo ni kusema kwamba hata kama kungalikuwepo TLP kama chama cha siasa kwa wakati huo nacho kingetufanyia hayo hayo unayoyaona. Kutangulia kuzaliwa kusiwe shida kwa vizazi vinavyofuatia na wala kusitumike kama leseni ya kubarikia mafisadi yoote haya yanayotuzunguka na kutukifu kama jamii ya Tanzania.

Tafadhali, hebu chukua hicho kiji-CCM yako hiyo na ukatupishe njia haraka!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi watu wa Tanzania mbona hamna shukurani? CCM imekutoeni mbali, kumbukeni CCM imezaliwa na TANU na ASP, kwa hiyo Bila CCM watu wa bara na visiwani msingepata uhuru.

Mazuri yote mnayoyaona yanatokana na CCM, elimu uliyonayo ni CCM, maisha yako ya zamani na sasa ni CCM, uhuru wa kuongea, kuabudu na vyombo vya habari ni CCM, jamani mbona mnalaumu uongo?

Kumbukeni hata hivyo vyama vyenu vya siasa mnavyoviita upinzani bila CCM visingekuwepo. Loh! niachieni CCM yangu.

Watu gani nyie msio na shukurani, baba ni baba tu, hata siku moja bega halizidi kichwa hata kama linaonekana ni kubwa. TCCM tutashinda siku zote na miaka yote.

Nawasilisha.
Mbona mambo yako yanafananafanana kama Steaven Wassira?.... au wewe ndiye?....anyway nilikuwa napita tu
 
Jamani ya nini tubishane nae?? si anataka ccm yake?
Haya Chimpanzee Baba/Mama chukua CCM yako, na sisi tuachie Tanganyika/Tanzania yetu....
We are even!!
 
Kazi nzuri, kwa kutuambia ccm ni kila kitu, maana mabaya yote na mateso yote wanayopata watz, kwa huduma mbovu na ufisadi yameletwa na ccm, endeleeni kuvaa na kuvua magamba!
 
Hakuna humu ndani mtu aliyekuwa na mawazo na fikra pevu kama Mwalimu, kama yupo anyooshe mkono. Na yeye Mwalimu aliisha sema ' BILA CCM IMARA NCHI ITAYUMBA' na ndilo linalo dhihirika hivi sasa
Mwalimu pia aliongezea angalizo hili: Ikiwa CCM itashindwa kutoa uongozi bora, Watanzania watautafuta kwingineko. CCM imeshashindwa kutoa uongozi ndio maana wako bize wanajivua magamba. Watanzania tunatafuta uongozi bora kwingineko.
 
Kweli nimeamini CCM wanawaza kwa kutumia tumbo na sio ubongo, kama alivyowahi kusema kijana wao wa UVCCM kule Arusha!
 
Hivi watu wa Tanzania mbona hamna shukurani? CCM imekutoeni mbali, kumbukeni CCM imezaliwa na TANU na ASP, kwa hiyo Bila CCM watu wa bara na visiwani msingepata uhuru.

Mazuri yote mnayoyaona yanatokana na CCM, elimu uliyonayo ni CCM, maisha yako ya zamani na sasa ni CCM, uhuru wa kuongea, kuabudu na vyombo vya habari ni CCM, jamani mbona mnalaumu uongo?

Kumbukeni hata hivyo vyama vyenu vya siasa mnavyoviita upinzani bila CCM visingekuwepo. Loh! niachieni CCM yangu.

Watu gani nyie msio na shukurani, baba ni baba tu, hata siku moja bega halizidi kichwa hata kama linaonekana ni kubwa. TCCM tutashinda siku zote na miaka yote.

Nawasilisha.
Sasa kama unauhakika wa kushinda wakati wote na miaka yote una lalamika nini?
 
Ile kauli ya makamu mwenyekiti ilinipa wasiwasi kidogo ila sasa naona wanafanya opposite badala ya 'kuhujumu' JF wamewahimiza vilaza wa pale Lumumba kujiunga kwa wingi kumwaga upupu

By the way si kulikuwa na uzi uliodai kuna dada alitimuliwa na Ma-rope kwa kuvinjari JF? Karibuni, mtufikishie salamu kwa Mwenyekiti!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom