Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Good day people;
Ukiachana na umaarufu wa tarehe yenyewe ambayo inafahamika duniani kote kuwa ni siku ya wajinga, hapa Nchini tarehe na siku hiyo ndiyo wanayoisubiria Watanzania walio wengi, Makada wa Vyama vya Siasa, Viongozi waandamizi wa Vyama na Serikali na zaidi ni Wananchi wa Arumeru na hasa Arumeru Mashariki ili kujua ama ni SUMMARI au NASSARI. Kila mmoja wetu macho na masikio yetu yameelekezwa huko nyakati hizi Kampeni zinapoelekea mwisho mwisho.
Pamoja na hayo yote ni wakati vile vile kwa Vyama vya Siasa, mashabiki na hata makada kuendelea kuwa na imani ama matumaini ambayo hayajajikita sehemu ama upande mmoja nikiwa na maana wakati huu ni lazma tusimamie mawili kama vile ambavyo mtu anakwenda kupima maambukizi ya Virusi vya Ukimwi majibu yategemewayo ni ama + au - ila ukienda kwa kujiamini kuwa wewe ni + na ukakuta uko - unakuwa umekwisha jitengenezea kaburi lako ghafla kwani zaidi ya majibu hayo uliyopewa ambayo hukuyategemea basi wasiwasi, woga, mshtuko ni baadhi ya mengi yatakayokukumba baada ya majibu hayo kwani haukuwa na utayari wa yote mawili. Vivyo hivyo basi kwa Vyama husika hasa hivi viwili vyenye nguvu its either + or -.
Kumekuwa na hulka ya kuanza kujitengenezea mazingira tetezi mara kura zinaibiwa mara ununuzi wa kadi mara utishiwaji wa wapiga kura na mambo kadha wa kadha na haya yamekuwa sana yakitolewa na Vyama pinzani dhidi ya Chama tawala kwa upande wake Chama tawala mara nyingi pale panapotokea kushindwa basi lawama hurushwa kwa wao wenyewe aidha kwa kutoonesha umoja ama ushirikiano katika Kampeni na haya tumeyashuhudia sana katika uchaguzi wa mwaka 2010 na si vinginevyo.
Sasa kama Vyama hivi shindani havitakwenda kwenye Uchaguzi na wazo la ama kushinda au kushindwa hasa CDM manake imeonekana kuna imani kubwa kupita hata ile punje ya haradani basi yatakuwa kama vile walivyokwisha sema wahenga kwamba "mbaazi ikikosa tunda basi husingizia jua" hivyo CCM waendelee kujiandaa kupokea lawama, kejeli, vitisho, na mambo yafananayo na hayo ila vile vile sidhani katika lawama hizo vile vile Zitto Zuberi Kabwe atapata pa kutokea, naye ajiandae vile vile manake kama Chama chake kitashindwa basi kushindwa huko kutajumlishwa na kauli yake aliyoitoa hivi karibuni na ataambiwa alisababisha wale wanaoitwa makamanda na wanaharakati kukata tamaa ama kukosa nguvu katika mapambano kutokana na kauli yake. Haya ni lazma tuanze kujiandaa nayo kadri siku zinavyokaribia kwisha.
Come out may, kubwa ni kuendelea kuomba amani, utulivu, hekima, na busara viendeleee kutawala katika nyakati hizi za kumalizia Kampeni na hata siku yenyewe ya Uchaguzi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama sharti vitambue kuwa utu wa Mtanzania kama ilivyoainishwa katika KATIBA-JMT, UDHR, AU-Charter, na Sheria zinginezo za Kitaifa na Kimataifa ndio mkubwa kuliko hata hiyo kura yenyewe hivyo manyanyaso, vitisho, na mengineyo yasiwe na nafasi katika siku hiyo husika. Watimize wajibu wao kama iwapasavyo.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Arusha, Mungu Ibariki Arumeru, Mungu Ibariki Arumeru Mashariki.
Naomba kutoa hoja.