Ni yapi matokeo ya ongezeko la wanawake wanaobandika kucha bandia na kupaka rangi kucha?

Mimi Melki

Senior Member
Mar 31, 2022
155
256
Habari,
Matokeo pekee ya ongezeko la akina dada na akina mama wanaopaka rangi kucha na kubandika kucha bandia katika vidole vya miguu na mikono yao ni utatuzi wa tatizo la ajira.

Nami nimeamua kujikita rasmi kwenye mawazo ya jinsi gani ninavyoweza kuitumia kama fursa!

Ningelipenda kufahamu kutoka kwa wazoefu wa kazi hii kuwa ni vifaa vipi vinavyohitajika katika upakaji wa rangi za maji pamoja na ubandikaji kucha za bandia? Je, vipi kuhusu gharama zake? pia na wapi kwa hapa Dar naweza pata hivyo vifaa? (Mimi mgeni kwenye hili jiji) pia mitaa yenye wateja wake wengi! Mtaji unaohitajika hasahasa kwa mimi nitakayeifanya shughuli hii kwa kuzunguka nyumba hadi nyumba bila kusahau faida ya siku!

Nahisi kwa sasa nimepata elimu ya kutosha kufanya biashara hii baada ya kufuatilia mafunzo mbali mbali kupitia mitandao ya kijamii

Kwa wateja wa huduma hizi ingelikuwa vyema mkanifahamisha kuhusu kiwango mnachotozwa kwenye issue nzima ya upakaji rangi kucha, ubandikaji kucha za bandia na uchoraji kucha!

Pia ingelikuwa vyema kama mngenishauri kama itanilipa nikiamua kuongeza ujuzi wa ubandikaji kope, kusugua gaga, massage za miguu, kusambaza vipodozi na viatu vya kike!

Mwisho, naomba kufahamu kuhusu manufaa na changamoto za hii biashara ili niweze kuchukua tahadhari mapema kabla ya kujitosa rasmi!

Nawasilisha:
 
Back
Top Bottom