Ushauri: Biashara ya kupaka rangi kucha za akina dada

Mimi Melki

Senior Member
Mar 31, 2022
155
256
Habari,

Leo nimekuja kwenu kupata mwongozo wa biashara ambayo nina mpango wa kuianza wiki ijayo ya upakaji rangi kucha na ubandikaji kucha za bandia wadada na wake za watu.

Ujuzi nilionao mpaka sasa ni kubandika kucha bandia na kupaka kucha rangi za kawaida hapa jijini Dar es salaam na biashara yangu nitaanza kwa kupita mtaa hadi mtaa, nyumba hadi nyumba, guest hadi guest na baa hadi baa!

Natarajia kuanza kuifanya nikiwa na malengo makubwa sana niliyojiwekea, hivyo ninatarajia kutengeneza pesa isiyopungua elfu kumi na tano kwa siku! Wazoefu wanambie kama inawezekana kutengeneza hiyo faida

Baada ya kuwa mzoefu na kupata pesa za kutosha, nitakusanya wateja wangu pamoja na kupanga chumba cha kawaida tu ili kuepusha gharama ya flem! Hapa nitakuwa nikifanya massage za nyayo, kuosha miguu, kupaka rangi za Gel, kusugua gaga na huduma nyinginezo muhimu

Nategemea wanawake waje waseme kwa hapa Dar nianze kuzungukia maeneo gani ambapo nitapata wateja!

Pia naombeni changamoto za biashara hii ili niwe tayari kuzikabili kutoka kwa wateja ikiwemo hata matumizi ya mafuta ya taa ili kupunguza mihemko pamoja na matumizi ya bastola ili kuepuka utatuzi!

Pia itapendeza nikipatiwa gharama ya kubandika kucha na upakaji rangi kucha ambazo mnatozwa (akina mama) ili niweke ofa kuwavutia wateja!

Muhimu:
Tumshukuru Rais
 
ngoja waje wabandika kucha
 
Jibu lipo kwenye huu uzi mkuu!
Sasa ndio ufikirie kufanya kazi ya kusugua miguu ya wake za watu?

Ni heri ukaanzishe kanisa utapiga hela nyingi za hao wake za watu, muhimu ujue tu kukemea mapepo 😀
 
Back
Top Bottom