Ni yapi majukumu ya ofisi ya taifa ya takwimu tofauti na yale ya kuratibu na kufanya utafiti na sensa

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,201
2,000
Wadau Mimi ni mwanachuo leo nimeenda kwenye moja ya ofisi ya taifa ya takwimu huku mkoani kuomba takwimu zinazohusu masuala kadhaa ya elimu ( Gross enrollment rate,net enrollment rate, transition rate, droupout rate n.k ) kwa takwimu za elimu msingi na zile za elimu sekondari kwa ajili ya matumizi yangu ya kujifunza kwa takwimu za miaka 5 (2014-2018)

Cha kushangaza mtalaam wa takwimu ( meneja wa takwimu mkoa) ananiambia kuwa ofisi yake haina hizo takwimu na akaniambia labda niende ofisi ya mkuu wa mkoa kwa maana ofisi hiyo pia ina watu wa takwimu yawezekana watakuwa nazo.

Nikamwambia pia, kwa kuwa takwimu za elimu huna basi naomba kujua kwa mkoa wako hali ya matukio ya uhalifu ikoje hadi kufikia mwezi desemba,2018 ( crimes statistics) napo akasema takwimu hizo hana labda niende kwa kamanda wa polisi mkoa kwani wao ndio wanaohusika na masuala ya uhalifu.

Swali langu la mwisho nikamuuliza mtalaam wa takwimu kutoka ofisi ya taifa ya takwimu ( meneja takwimu mkoa) kuhusu mfumuko wa bei ukoje kwa mkoa wake kufikia mwezi wa January, 2018?, vile vile nikataka kujua ni wilaya gani mkoani kwake inaongoza kwa vifo vya akina mama ( martenal mortality rate) kwa takwimu zilizoishia mwaka 2018.

Cha kushangaza tena meneja akaniambia kuwa hizo takwimu hana kwenye ofisi yake labda niende ofisi ya mkuu wa mkoa au hospital ya mkoa ndio wanaweza kuwanazo.

Nikatoka nje kidogo nikaanza kuangalia kibao kikisomeka ( ofisi ya taifa ya takwimu, mkoa....).

Nikawa siamini kama nimekoswa hizo takwimu kutoka ofisi ya taifa ya takwimu kwani niliamini ndio ofisi rasmi ambayo mtu yeyote mwenye uhitaji wa takwimu anaweza pata takwimu kwenye hiyo ofisi ( kama jina lake lilivyo).

Kwa hapo tu, ndugu zangu naomba kufahamishwa majukumu makuu ya ofisi ya taifa ya takwimu.

Sambamba na hilo naomba kujua ni ofisi ipi ya Serikali inapaswa kukusanya, kuchambua na kuhifadhi takwimu zinazozalishwa kwenye sekta mbalimbali nchini ( takwimu za papo kwa papo, currently data)?

Lakini pia naomba kujua uhusiano uliopo kati ya ofisi ya taifa ya takwimu na ile ofisi ya Rais tamisemi kwenye masuala yanayohusu takwimu.

Nipo kwa ajili ya kujifunza ili kuongeza maarifa zaidi.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abshallom

JF-Expert Member
May 19, 2018
224
500
Hayo yote uliyoyauliza yanapaswa kuratibiwa na NBS. Mind you mkuu, kazi ya kukusanya takwimu siyo ndogo na inahitajika mfumo mzuri Sana ya kukusanya, kuchakata na kuhifadhi takwimu. Kwa sasa miundombinu hiyo NBS hawana. Kwa kifupi ni kama hawajui wanachokifanya.

Hata hivyo NBS ni shirika changa sana, na bado linajijenga, so I hope huko mbeleni watakuwa vizuri tu. Mimi ni mtakwimu na mchumi kwa taaluma, nafahamu Changamoto zilizopo na gharama ya kukusanya takwimu.

Tatizo jingine la NBS ni kuwa na ubinafsi kwa kutoshirikisha taasisi nyingine zenye kuzalisha takwimu za muhimu, kama vile mahospitalini, mabenki, migodini, bandarani, tpdc, n.k,

Hata hivyo Nina Imani huko mbeleni watayarekwbisha maana kuorganize takwimu ni kazi ngumu sana yenye kuhitaji rasilimali fedha nyingi sana na wataalamu wengi wa takwimu. Hivyo usimlaumu sana huyo Ofisa, japo alipaswa ajiongeze kikawaida tu na kukupatia baadhi ya data.

Umejibu vizuri, napenda pia kujua mfumo wa taifa wa ukusanyaji takwimu ukoje. Yaani kuanzia ngazi ya wizara hadi lower level government (LLG).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom