Ni Woga gani huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Woga gani huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaalaamuna, Mar 10, 2011.

 1. M

  Mtaalaamuna Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado naendelea kufikiri jambo lililomfanya mkuu wa nchi kutangaza kuwa anataka kuondolewa madarakani kwa nguvu.

  Si jambo la kumwingia mtu akilini kwa Rais kusema jambo zito kama hilo la kuwatisha wananchi kuwa nchi inataka kupinduliwa, ukizingatia kuna vyombo mbalimbali vinavyofanya kazi zake kiufasaha na umakini, na kama ndivyo basi hizo njama za kupindua serikali zingehesabika ni UHAINI na si vinginevyo.

  Sidhani pia kama Mtoto akiona baba yake analewa kila siku ilhali yeye hana madaftari ya shule, hajalipiwa ada nk, akimshinikiza baba yake kuwa amlipie ada na kununua vifaa vya shule anakuwa amentusi na kumsaliti.

  Ninacho kiona ni WOGA na KUTOJIAMINI kwa Mkuu wa nchi
   
 2. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Anafahamu fika kuwa Dr.Slaa ni tishio kwake na tamko lake halina maana anataka Watz wamwonee huruma kuwa anabanwa pasipo sababu na Chadema. Ila yeye ni miongoni mwa viongozi wengi ndani ya serikali wasiolala usingiza kila wakisikia dr Slaa. na bado!!!!!!!
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya UMMa,inamkosesha raha
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  anatanga nanjia tu yule msaniii..................
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mkuu usimalizie kushangaa ili nami niunganishe mshangao wangu humo humo alaf tuhitimishe mshangao kwa pamoja. Hivi ni vioja vya nchi ya kusadikika ya TZ,hapa usalama wa taifa uko wapi kama watu wanakaa wanapanga kuipindua govt.na watawala wanakaa kuliakulia tu. Wasiri anasimama anakaa na kuueleza uma kuwa cdm wamepewa hela nyingi ili kuipindua nchi! Ivi sheria zinazohusu fedha haramu zimefutwa lini Tanzania?ukisoma Anti Money Loundering Act,ukasoma sheria za uhujumu uchumi,utashindwa kuelewa kama taifa lina serikali,mkuu anadai anapinduliwa,hapa si ndo Lema pia adai tumfanyeje Jk kama ataonekana kulidanganya taifa kuwa kuna wahaini? Kumbuka ikulu chini ya mkurugenzi wa mawasiliano Salva alishalitangazia taifa kuwa Dr.Slaa amezeeka vibaya na ameweuka,je mbona wanaendelea kumuandama?au wameamua kumjibu regardless kuwa ni 'mweu'?je mbowe?naye ni nani sasa! Sophia simba aliwaasa wanawake watunyime Unyumba kama tuk├Čipenda chadema,iyo akili au tope kichwani? Mh.dr.slaa usikate tamaa,kuikomboa taifa ni kazi sana,tulia maana wee ndo mkombozi wetu. Cdm ni chama pekee kinachoweza kunikomboa mimi kama maskini. Nawapongeza cdm,nawashangaa watawala wetu!
   
 6. M

  Mtaalaamuna Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia historia za africa utagundua, kama nchi ina machafuko au wasiwasi wa kupinduliwa au kuwepo na uasi basi rais wake hathubutu hata kutoa mguu wake kwenye nchi yake hata kwenda kwa jirani yake anaepakana nae, kwa hofu ya kupinduliwa atakubakishwa huko huko nje, Mbona JK tangu alipo toa tamko lake mpaka leo yeye ni kiguu na njia anakwea pipa hajatulia huku wabongo wanahali mbaya ya maisha. Kama maneno yake yangekua na ukweli angetoa mguu bongo TZ???

  Moto ule ule Tufanye mikutano na maandamano kwani lengo letu si kupindua nchi bali kutaka GVT ione uchungu wa people wake wana hali mbaya.
   
 7. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  hapo umenena rais wetu haigopi chadema wala dr wa ukweli anawaogopa wananchi anajua fika ushindi wake ulikuwa wa kupika hivyo nguvu ya umma ni dhahiri inaweza kumtoa
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Anafahamu kuwa aliingia mjengoni ndivyo sivyo, mwenyewe kustahili akitaka kuingia patakuwa hapatoshi.
   
 9. s

  salisalum JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hana uoga wala nini ni siasa tu. Wananchi hawatishwi nyau sasa hivi. Amani wakati mkono hauendi kinywani?
   
 10. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Huyo ndio asiye na "Kiherehere"......... ! Na anasema hivyo sasa kuwaambia wafuasi wake waamke maana hata yeye anakosa usingizi siku hizi....! Mbona Dr. Slaa na CDM walikuwa wasingemnyima usingizi?
   
 11. T

  TUWEKANE BAYANA Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uko dipu ndugu! na mimi naunganisha mshangao wangu na wako na wake.. kwaivo kuna mishangao mitatu...
   
 12. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Huwa hana hoja za kujibia hoja, anatafuta huruma kwa kuchezea dhamiri za wananchi, kwa upande mwingine ni dhaifu na mlalamishi kama wale wengine wanaolalamika toka enzi zile.
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,127
  Trophy Points: 280
  Rais mwoga anatuaibisha haoni wenzake Mbarack, Sadam hadi anatolewa madarakani bado anasema yeye ni rais, huyu kutikiswa kidogo tu analia lia.
   
Loading...