Ni wivu au kushindwa kujiamini?

Unalo bibi linalokukaba na roho,basi ungemuandika jina usoni kuwa huyu wangu???

Si riziki yako yule,kanipenda nimempokea kwa mikono miwili,na nimetulia nae

Bibi mi sichukui wa watu,nawaweka ndani kwangu ati,na najua hasa kuwaweka.......

We endelea na maisha yako,acha bifu mi huniwezi ati hujalisoma hilo?

ulisema wa nini mi mwenzio nilikuwa nasali nikipate kama kile....sasa ndo imekuwa......

................wivu at work!!lol.....
 
wawa hivi...
kila saa simu u(uko wapi ee katavi??? hebu fanya urudi kazini si umetoka tangu saa 3.oo mpaka hii na nusu hujarudi )
akikamata cellphone yako mbio inbox..
ukiongozana nae akutizama machoni usije ukatiza mwanamke..
mkitizama tv usiweke picha yenye mwanamke mrembo ukamkodolea macho hakutalalika tena hapo...etc...

Mh, hiyo itakuwa kero sasa :car: :car:
 
asante Rose....wengine sie imegeuka kero kwa kweli, mie nilikuwa najijuaga nina wivu nimekuja gundua wa kwangu cha mtoto sana, mwanzoni nilidhani mambo yatarekebika tu lakini sasa nimeshaizoea hali japo ni kero kero....wivu sana unageuka kero kwa kweli.

lakini si ndio nyinyi Nyamayao,
mnalalamika kipindi ukijua bwana/mumeo hana wivu na wewe?
 
wivu ni kuni za kuchochea mapenzi yakaiva or yakaunguwa.

wivu mdogo-mdogo ni kuni ya kuivisha mapenzi,
wivu ukizidi ni kuni za kuunguza mapenzi,
lakini basi, wivu wa mwanamke sio wa mwanaume,

let me tell you!!

mwanamke akimuonea wivu mumewe mara nyingi mapenzi yazidi.
mwanaume akimuonea wivu mkewe, hapa fitina huwa inaanza.
 
Wivu ni aina fulani inayoonyesha Care kwa mpenzi wako lakini ikizidi ndiyo inakuwa na madhara Jaribu kutoonyehs hali ya wivu kwa mkeo uone naamini ipo siku atakuambia kuwa hunipendi kabisa.
Mkuu umegonga nyundo, kwa mpenzi inaweza kuwa sababu ya kuachana :playball:
 
wivu ni kuni za kuchochea mapenzi yakaiva or yakaunguwa.

wivu mdogo-mdogo ni kuni ya kuivisha mapenzi,
wivu ukizidi ni kuni za kuunguza mapenzi,
lakini basi, wivu wa mwanamke sio wa mwanaume,

let me tell you!!

mwanamke akimuonea wivu mumewe mara nyingi mapenzi yazidi.
mwanaume akimuonea wivu mkewe, hapa fitina huwa inaanza.

Unataka kusema hapo mwanaume hupaswi kuwa na wivu na mkeo kuepusha fitna?
 
teena ..... kwani ulikuwa wajua kero yafanyajwe ni vijivisa visa tuu vidogo vidog lakini ilimrad musuguane nafsi tuu baas...

NILHAM Misuguano inaweza sababisha majeraha makubwa, wengine wanaliazisha:suspicious:
 
teena ..... kwani ulikuwa wajua kero yafanyajwe ni vijivisa visa tuu vidogo vidog lakini ilimrad musuguane nafsi tuu baas...

Nilham, Blue Face kasema hapa mwanaume akiwa na wivu kwa mwanamke, basi aghalabu hugeuka kuwa kero!!!!!!!!
 
Wivu ni SUMU mbaya sana kwenye mapenzi wajameni...IT DEPENDS na jinsi mtu unavoweza kuuhandle

wengine unazidi hadi unakuwa GUBU kiabisa

Mi niulize tu katika muktadha huu, kwa nini nyumba ndogo 'zinauma' zaidi kuliko kubwa......hivi nao huo ni wivu ama GUBU.....

MJ1 hapa najua unaweza kuwa na 'a second thought'
Hii issue ni kweli kabisa, ufafanuzi kwa wenye uzoefu zaidi!!
 
Unataka kusema hapo mwanaume hupaswi kuwa na wivu na mkeo kuepusha fitna?

no, labda nimeandika sivyo - na-mean wivu wa mwanaume, sababu kubwa labda kamuona mkewe/gal wake anazungumza na wanaume wengine, hapa wanaume wanakuwa na wasiwasi labda partner wake anajuwana na wanaume wengi na inafikia kuwa na fikra mbaya..
 
bacha, hii kitu inaitwa wivu kwa wapenzi sometimes inaboa sana inafikia wakati. huli, hunjwi, huangalii, hupumziki, hutembei, hucheki.... aaaggghhh!
 
bacha, hii kitu inaitwa wivu kwa wapenzi sometimes inaboa sana inafikia wakati. huli, hunjwi, huangalii, hupumziki, hutembei, hucheki.... aaaggghhh!

sasa si uachane na hii kitu wivu,
kama inakupa mateso yote hayo?
kwanini utaabike, kwani huwezi kumpenda bila kumwonyesha wivu?
Kuna wengine wanadai wivu ni chachandu ya mapenzi,
lakini kumbuka kuna baadhi ya watu hawahitaji chachandu ili kunogesha mapenzi,
 
Back
Top Bottom