Ni wenye pesa tu ndo watakaohudhuria mahafali ya 40 UDSM

sasa kama ni kula kulala we unadhan anashindwa kulipiwa. Watu wanahustle kupa hela ya kodi ya nyumba, maji, umeme na misosi na siyo kunenepesha matumbo ya wachache.

nani amekuambia mimi ni kula kulala? Mimi mbishi ndio maana kama mwanaume wa dhati hiyo hela hainifanyi nilie. Watoto mayai ndio wanaomaliza chuo wanakaa nyumbani na wanashindwa kupata hata 45000
 
hivi hata wabunge wanapolia kuhusu ukosefu wa dawa, maji nao huwa ni walengwa? Na hili ndilo tatizo letu, huwa tunasubiri yawe upande wetu ndipo tulalamike.

Tindikali ndugu yangu, nalijua hilo, na ndio maana nimekuuliza. Sijakuambia kuwa ww ni mlengwa.
 
Hao hawaazimishi majoho, "wanauza"!
Mimi nd'o maana nilisepa nalo kwa thamani ya sh. 10,000.
Nimeliweka kwenye kabati maalumla vioo kwa ukumbusho.
Mtu akitaka kulishika tu anatoa pesa kwanza na hakuna anayejaribu kulivaa kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kujiita Dr. Ndodi au Professor Majimarefu. Teheteheteheeeeeeeeeeee!

hongera sana, umewaweza.
 
Umefulia nini? Boom hakuna siku hizi.. Hiyo ndo serikali ya magamba..mtu unamaliza chuo hata sh 500/= kazi kuipata.
 
Yaani 45,000 tu? Aaaaah jamani

Kweli kabisa wandungu 45,000 sio nyingi sana, kwa mfano waweza kwenda bar saa 10.00 jioni mpaka kufika saa 2.00 usiku ukawa umetumia zaidi ya 100,000!...... lakini kuna watanzania hawana hata 1,000 ya kula kwa siku! ..... sasa wewe unaeshaanga 45,000.... yawezekana unao wezo wa kupata hizo pesa,
 
Kiwango cha pesa kilichowekwa na chuo kikuu cha dar es salaam kwa ajili ya kukodi majoho kwa ajili ya mahafali ambacho ni zaidi ya 45000; kimeonekana kuwa tatizo miongoni mwa wahitimu wengi. mpaka sasa ni zaidi ya rafiki zangu kumi wamesema watashindwa kulipa pesa hiyo kwani ni nyingi mno na wengi ni masikini na mpaka sasa hawajapata kazi.
hivyo utofauti upo kati ya maskini na matajiri udsm

Kwani mmehitimu ili muajiriwe tu ndo muweze kuishi??? Kwanini hawataki kujiajiri kama wanaona ajira ngumu ama elimu yao ya degree haijawasaidia? kama haijawasaidia basi hawastahili hata kuhitimu na kwenda kwenye mahafali hayo
 
Kwani mmehitimu ili muajiriwe tu ndo muweze kuishi??? Kwanini hawataki kujiajiri kama wanaona ajira ngumu ama elimu yao ya degree haijawasaidia? kama haijawasaidia basi hawastahili hata kuhitimu na kwenda kwenye mahafali hayo

mara nyingi wanaopiga kelele za kujiajiri hawajawahi hata siku moja kufikiri kufanya hivyo. Jaribu kufikiri zaidi ya hapo mkuu.
 
Wanataka mpaka majoho yawe included kwenye mikopo jamani
45000 ni inclusive na fund raising nini?
 
Yaani 45,000 tu? Aaaaah jamani

Unashangaa nini? jaribuni kuwa mnatembelea sehemu za vijijini hapa TZ.
Kuna watu wanaishi TZ hii kipato chao kwa mwezi ni Tsh.600/=, We unashangaa mtu kukosa 45,000/=!!
Fanyeni ziara mikoani na hasa vijijini ambako hata gari hazifiki mjionee waTZ wanavyohangaika na maisha ya kila siku.

ASIEKUWA NA BUSARA APINGE MANENO YANGU.
 
Back
Top Bottom