Ni wazi Tanzania sasa tunawahitaji akina Anna Hazare... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wazi Tanzania sasa tunawahitaji akina Anna Hazare...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sajenti, Aug 18, 2011.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nchi ya India kwa siku takribani 4 imekubwa na joto kali la maandamano yaliyochochewa na mwanaharakati na mpigania haki Anna Hazare. Mzee huyu mwenye umri wa miaka 74 alikamatwa na polisi wa India baada ya kuanza mgomo wa kutokula kuishinikisha serikali ya india ya india kufanya marekebisho katika muswaada wa kupambana na rushwa. Baadae alikamatwa na kuwekwa korokoroni halii iliyochochea maandamano katika miji kadhaa kama Mumbai, Chennai, Bangalore, Calcutta na miji mingine.

  Waandamanaji kwa maelfu walikusanyika nje ya kituo cha polisi alichoshikiliwa Hazare na yeye alishikilia mgomo wa kutokula hadi hapo serikali itakapoufanyia marekebisho muswaada huo. Polisi wamekubali kumtoa kizuizini mwanaharakati huyo kwa sharti kwamba mgomo wake wa kutokula kwa siku 15 akaufanyie katika bustani Ramlila mjini humo.

  Waziri mkuu wa India Manmohan Singh amemshutumu Hazare kwa kusababisha vurugu. Mwezi wa Aprili mwaka huu Hazare aliingia tena kwenye mtifuano na serikali ya Indian alipoishinikiza serikali kuandaa muswaada wa sheria itakayoruhusu maofisa wote wa serikali wanaotuhumiwa kwa rushwa kuchunguzwa na kushitakiwa endapo watabainika kushiriki katika kutoa au kupokea mirungula. Na ndio juzi mzee huyo alipoingia tena matatani pale alipogundua kuwa muswaada huo wa sheria unawaepusha viongozi wa juu wa serikali kuhojiwa na kushitakiwa endapo watakutwa na tuhuma za rushwa akiwemo waziri mkuu.

  My TAKE: Msimamo wa Hazare kwa ukweli kabisa umenifanya nione kuwa Tanzania kwa hali ilivyo sasa tunahitaji watu wa aina yake watakaotoa shinikizo kwa serikali legelege hii na sisi wananchi tuungane nao. Tuhuma za rushwa na ufisadi zinazowakabili viongozi kibao katika ngazi mbali mbali zinaimaliza nchi na serikali ipo tu inachapa usingizi.....Mbaya kabisa!!
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimependa kauri yake Mzee huyo ya kuishi ama kufa [Live or Die] kwa kihindi ni Kelenga Malenga

  Hakika Uwa nafurahi kuona kuwa wakati watanzania wengine wanaona kwa usahihi kule Taifa linakowenda Viongozi hawaoni wanakotupeleka,Yaani tulipofika wazee wengi ambao wana heshima zao wasimame waseme hapana na iwe mwisho,hasa wazee wa chama tawala kwa kuwa kukaa kwao kimya siku cheche [spark] ya umma ikiibuka hata wao pia watakuwa ni sehemu ya uovu.Na angalia kwa utu uzima huo wa miaka 74 mzee anasimamia haki Tanzania hatuna Wazee?

  Hakika utu uzima dawa watu wazima wa Tanzania watu wanamsaada gani kwa wajukuu zao wa sasa na kizazi chao kijacho.?
   
Loading...