Ni wapi Serikali imefanikiwa kwa asilimia 100?

Ni wapi Serikali imefanikiwa kwa asilimia 100?

Najua sana tu. Penye AMANI pana UTULIVU unaokuja kama matokeo ya AMANI. Ila unaweza kuwa na UTULIVU bila ya kuwepo na AMANI. Ukienda gerezani mfano kuna UTULIVU wa hali ya juu na unauonekana dhahiri ila hakuna AMANI kwa sababu utulivu ule siyo matokeo ya AMANI. Iwe waitu umeeeeeeeelewa?

Ni mara chache sana kuwakuta watu wenye busara kuchangia mijadala ndani ya JF, nikupongeze kwa busara yako maana kuna watu wapo ili kuharibu hata sara zao ili waonekane na watu. Wape tena mambo mazuri mengi ya nchi yao inawezekana ushabiki ndiyo kinga yao badala hata lepe la dhamiri zao kuguswa hata na lepe la chembe ya ukweli.
 
Kuuziana nyumba za serikali, kwani hakuna aliye lalamika kukosa nyumba hizo !
 
Imefanikiwa Kwenye AMANI, UTULIVU, MSHIKAMANO na MUUNGANO wetu wa kupigiwa mfano Afrika nzima.

Tuna amani gani kwa umaskini tulionao?
Utulivu unaodumishwa kwa mtutu wa bunduki?
Muungano ulisha kataliwa serikali inalazimisha tu
 
Imefanikiwa Kwenye AMANI, UTULIVU, MSHIKAMANO na MUUNGANO wetu wa kupigiwa mfano Afrika nzima.

Tata..sema kwenye utulivu na mshikamano wa maskini kwa masikini..ila AMANI hamna watu wengi wagonjwa na wana njaa sema hatuwaoni sababu ya UTULIVU hivyo tunahisi wana AMANI.
 
Imefanikiwa Kwenye AMANI, UTULIVU, MSHIKAMANO na MUUNGANO wetu wa kupigiwa mfano Afrika nzima.

Tata..sema kwenye utulivu na mshikamano wa maskini kwa masikini..ila AMANI hamna watu wengi wagonjwa na wana njaa sema hatuwaoni sababu ya UTULIVU hivyo tunahisi wana AMANI.
Kwa hiyo kimsingi unakubaliana na hoja yangu ya awali kuwa kama hakuna AMANI basi kutakuwa na UTULIVU.
 
Binafsi nawaona wamefanikiwa sana:- Ujangili 100% , Maisha Magumu kwa Kila Mtanzania wamefanikiwa 100%, UFISADI wa ESCROW, MV Dar es Salaam, Mabehewa, Sukari, 100%, Kuwapiga sana Wapinzani 100%, Huduma duni za Afya, Maji, Elimu, Barabara wamefanikiwa 100% ... Kushuka kwa thamani ya shilling na Mfumuko wa Bei 100%, kuwalinda wakwapuaji wa Rasilimali zetu 100% ... Uchakachuaji wa kura, katiba 100% ... Nahisi matatizo makubwa yako kwa UKAWA na wananchi waliolala Usingizi wa PONO !!! ..
Nilikuwa najaribu Kufanya uchunguzi mdogo, kuona na eneo gani ambapo serikali yetu iliyo chini ya chama tawàla CCM. Kwa HAKIKA nimeshindwa kuona ni eneo gani ambapo serikali imemudu kufanya vizuri kabisa.

Hebu jaribu kuangalia maeneo yafuatayo( kama mifano tu)

1. Elimu: Shule za serikali ni matatizo makubwa.

2. Afya: Hospitali za serikali ni shida kubwa kuliko kawaida.

3.Usafirishaji: Barabara ni ajali kila kukicha. Bandarini ni malalamiko ya ubovu wa miundo mbinu, rushwa n.k. Usafiri wa ndege ( ATC) ni taabani, Uwanja wa ndege Dsm, mbovu, rushwa n.k.

4. Utumishi: Watumishi wa serikali kila siku ni malalamiko ya hali duni ya maisha, yanayosabàbisha utendaji mbovu ktk ofisi za serikali.

5. Kilimo: Hakuna miundombinu rafiki kwa wakulima. Wakulima wamekuwa yatima!

6. Posta na Simu: Chali !! Hakuna kinachoendelea huko!

Jamani, ivi ni sehemu gani ambapo serikali imefanya angalau kutufanya wananchi (wapigakura) tujivunie?? Au ni Intelligencia ya polisi PEKEE ndo iko vizuri? Inawezekana ...!!

Wana JF nisaidieni kunikumbusha basi. Kama sivyo nini kifanyike ili angalau tuwe na eneo moja la kujivunia??
 
Kuvunja katiba 100% refer katiba ya znz 2010,wizi wa pesa za umma kila mwaka CAG ripoti inaonyesha,kupora ardhi za wananchi masikini kuwapa matajiri,migogoro na wafanyakazi,migogoro na wanafunzi wa elimu ya juu,migogoro na wafanyabiashara,migogoro na wafugaji,migogoro na wakulima,kuendelea kutuchafua kwa mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi
 
njeleson

Mkuu huko ulikojikita kutafuta mafanikio ya serikali kwenye maendeleo ya wananchi siko. Ukitaka kutafuta mafanikio ya serikali yetu jikite kwenye Esrow, epa, richmond na maufisadi ya namna mbalimbali yanayofanywa na viongozi.

Na research yako wewe ni kuhudhuria mikutano yao. Kule utakuta wanajisifu mambo ya majoka yenye makengeza, hela za mboga nk.Ukitaka kutafuta serikali ilikoshindwa 100% ndo ujikite kwenye hizo mada zako 6.
Ongeza na foleni za magari.
 
Kama umeenda shule kidogo utaelewa kuwa AMANI na UTULIVU ni vitu viwili tofauti. Na kama kimojawapo hakipo Tanzania basi lazima kingine kipo. MSHIKAMANO upo kwa hakika japo tunaanza kuona mmomonyoko wa mshikamano. MUUNGANO upo na anayebisha ana matatizo. Kinacholeta mtafaruku kwa sasa ni muundo wa muungano.

Muungano umekufa ilipokufa tanganyika.
 
Ikishafanikiwa 100% itakuwa na kazi ipi tena?

Wewe binafsi yako umeshafanikiwa 100%?
 
Ikishafanikiwa 100% itakuwa na kazi ipi tena?

Wewe binafsi yako umeshafanikiwa 100%?
Kama ufisadi unapukutisha mbongo kwa kiasi hiki?basi tuache wizi otherwise hata watoto wetu watatushangaa,
 
Kwenye wizi, upokeaji rushwa Ikulu na Bungeni, mauaji ya Tembo nchini, kuficha pesa za wizi kule Uswiss, kuwasafisha na kuwakingia kifua wezi, wapokea rushwa na mafisadi.

Kwenye ufisadi mafanikio110%
 
Kuthibiti Uwezekano Wowote wa kupata Katiba Iliyorejesha Mamlaka kwa Watanzania
Kuingiza Miswada Bungeni Bila kushirikisha Wadau Waathiriwa wa moja kwa moja na miswada hiyo
Kusheherekea Mwenge, Mapinduzi, Uhuru, Muungano
Kujilipa maslahi mazuri
Kupitisha sheria zinazo kandamiza haki, usawa, utu, uhuru na mawazo
 
Kama ufisadi unapukutisha mbongo kwa kiasi hiki?basi tuache wizi otherwise hata watoto wetu watatushangaa,

Nimeuliza maswali mawwili myepesi sana, naona unakuja kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Hata kupora mke wa mtu ni ufisadi tena wa maadili kabisa ambao ni ufisadi mbaya kuliko ukoma.
 
Back
Top Bottom