Ni wapi nitapata mwanamke wa kuoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wapi nitapata mwanamke wa kuoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gudboy, Oct 12, 2011.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani wandugu, heshima zenyu bana.

  Mimi ni kijana mwenye maisha na kipato cha kawaida, naona umri unasonga kwa kasi ya ajabu, na hivyo kuifanya nafsi yangu inishawishi ya kwamba wakati wa kuoa umefika. Na kweli hata mimi mwenyewe nimegundua kuwa kumbe ni kweli wakati wa mimi kuwa na mwenza ni huu.

  Maana jinsi ninavyoyaona haya maisha ni kama routine vile, hakuna cha zaidi kitakachonifanya nizidi kuchelewa kutafuta mwenza wa kuishi nae, zaidi ya yale yale ya kila siku (mfani, kwenda kazini, kurudi home, kula kwa mama lishe, week end kwenda kutembea na shughuli za hapa na pale kwa ajili ya kujiletea maendeleo).

  Kutokana na haya yote naona nimebakisha mambo ya muhimu mawili tu katika maisha ya hapa ulimwengu nayo ni KUOA NA KUFA. Sasa kabla hili la kifo halija overtake hili la ndoa ndio nimeona ya kwamba wakati umefika ili nikamilishe maisha kamili.

  Sasa huwa najiluliza je ni wapi naweza kupata mwanamke ambaye atakuja kuwa mke wangu? Nahitaji kuoa kwa nguvu zote bila ya kuchelewa au kupoteza muda. Wandugu je ni sehemu zipi naweza pata mke ambaye atakuwa na busara zote?

  Nawasilisha
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mwana naona kaa vile unakuwa na haraka kidogo...sasa hapa ndipo utakapojikuta unakosea katika uchaguzi wako....
   
 3. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  La kwanza je umeshatambua ni mwanamke wa aina gani unahitaji?wa sifa zipi? then mshirikishe mungu ili aweze kukukutanisha na aliyemuumba kwa ajili yako,Unaweza kumpata popote pale mungu atakapopenda awakutanishe, yaweza kuwa Maeneo yako ya kazi, humu mmu,kanisani,barabarani,unaweza waomba wazee wakutafutie kijijin kwenu km unataka wa kutoka kijini,kwenye daladala n.k.hiyo ni kwa upeo wangu,subiri wengine watakushauri vp!
   
 4. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Kwani wewe una umri gani Gudboy?
  Ni pm nikuambie pakumpata!
   
 5. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mkuu inawezekana ikawa ni kweli kabisa hapo penye nyekundu, lakini kulikua na kipindi nikiambiwa swala la kuoa nakua mkali na sitaki kabisa kusikia habari hizo, lakini mwaka huu naona nafsi yangu yenyewe bila ya kushurutishwa na yeyote, inahitaji kuwa na mke, sasa ili nisikurupuke natakiwa kusubiri kwa muda gani? Maana wakati mwingine kuoa ni kama bahati nasibu, mathalani mwenzako anaweza akakurupuka na kuoa na maisha yakawa shwari, lakini wewe unayesubiri, miezi sita tu ndoa chaliiiii
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
  daladala
  kanisani
  kazini
  mtaami
  chuo
  harusi
  au sherehe yeyote
  club
  msibani
  anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa ushauri wako mzuri, kwa kweli vigezi vya nimtakaye ninavyo, lakini wengi ninao kutana nao hawajatimiza hata robo yake. Naweza nikaa na mtu tukapiga story lakini nikimuuliza maswali ili kumjua, navunjika moyo kwa kuwa hana ninachohitaji
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  popote tu pale we kua mtu wa kujichanganya tu utawapata..................huh
   
 9. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Kaka muombe mungu, hilo ndo swali kubwa kuliko yote linasumbua sana vijana wa kiume kila mtu anajiuliza "HATA NIKITAKA KUOA NITAMUOA NANI? tunakuwa kwenye mahusiano mara nyingi lakini ukifikiria kumuhalalisha uliye nae roho inasita maana NDOA NI ZAIDI YA KULALA PAMOJA
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kamanda umeadimika kweli ndo mambo ya kusaka jiko nini?
  Nakushauri ukamate Mwalimu wa shule ya Msingi au wa O'Level
   
 11. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  nashukuru sana, lakini je nawezaje kumtambua kuwa ndie sahihi? Na pia natakiwa nimchunguze kwa muda gani, mathalani ndio nimempata?
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Umesahau bebii kuweka Bar vp tena jamani?
   
 13. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Pole Gudboy. Mi nishakuelewa vigezo unavyovitaka.
  Wanawake wenye vigezo hivyo wako wachache sana. Ndiyo maana nakuambia ni PM acha ubishi mi najua wanakopatikana. Loh!


   
 14. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni kweli mkuu, nilikua kimya mana hata simu nilipoteza, ila bila shaka yangu unayo, kama vp tufanye mawasiliano basi. Nimechoka maisha ya ukapera kaka, unaonaje kama nikirudi kule Tanga kaka?
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sasa wewe unataka tu kuletewa mke ina maana hata sifa za umtakae hujui sio.
   
 16. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  ni kweli kaka, hili jambo kwa vijana wa sasa ni gumu mno. huwa nawaambia watu sisi ambao bado hatujaoa tuna maisha magumu sana, lakini ukiangalia ni kweli, kumpata tu wa kuoa ni shughuli pevu
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kweli bwana ila nimemuambia kila mahali bus kwenye ndege mitumbwi meli kila sehemu kuna mwanamke bwana
   
 18. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Na hili ndio tatizo langu kubwa mkuu, mana nakua tight kiasi kwamba muda wa misele ya mara kwa mara sina, hata kwenye harusi nahudhuria chache sana. Na mara nyingi nakuwa safarini, hata kwenye usafiri kama sijakaa na mama mtu mzima basi ni mwanaume (hadi huwa naona sina bahati kabisa
   
 19. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  cheki kwa inbox yako mkuu
   
 20. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Kaka kama vp anza na Bebii huyo, si unaona alivyoizimikia thread,, dada bebii mwaga swaga zako za cv kabla wavaa CL hawajamuwai
   
Loading...