Ni wakati wa kuwa na CDF Mwanamke baada ya kustaafu Venance Mabeyo

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wanawake wanaweza sana. Tuna Rais Mwanamke, Waziri wa Ulinzi Mwanamke, Waziri wa Utalii Mwanamke, Kamishna wa Uhamiaji Mwanamke!

Hizi ni nafasi nyeti katika kuisukuma nchi.

Ni wakati sasa wa kuwa na CDF Mwanamke baada ya Venance Mabeyo.
 
Hivyo vyeo havitolewi kufurahisha watu au gender balance, vina kwenda kwa rank, mtu hajafikia hadhi ya mnadhimu halafu unataka awe cdf kisa gender. Hicho cheo sio ukuu wa wilaya wanaopewa kufurahishana Jeshi ni kitu kingine
 
Yoyote mwenye uwezo awe CDF
Tutofautishe UTENDAJI wa MTU na matumizi ya JINSIA kwenye majukumu
 
Hivyo vyeo havitolewi kufurahisha watu au gender balance, vina kwenda kwa rank, mtu hajafikia hadhi ya mnadhimu halafu unataka awe cdf kisa gender. Hicho cheo sio ukuu wa wilaya wanaopewa kufurahishana Jeshi ni kitu kingine
Mabeyo alikuwa mnadhimu?maamuzi ya rais kwa vyeo hivyo mkuu
 
Hivyo vyeo havitolewi kufurahisha watu au gender balance, vina kwenda kwa rank, mtu hajafikia hadhi ya mnadhimu halafu unataka awe cdf kisa gender. Hicho cheo sio ukuu wa wilaya wanaopewa kufurahishana Jeshi ni kitu kingine
Msuguri alikuwa cdf akiwa na cheo cha meja jeneral?mkapa akampandisha kuwa general mwaka 2002 akiwa ameshastaafu
 
Hivyo vyeo havitolewi kufurahisha watu au gender balance, vina kwenda kwa rank, mtu hajafikia hadhi ya mnadhimu halafu unataka awe cdf kisa gender. Hicho cheo sio ukuu wa wilaya wanaopewa kufurahishana Jeshi ni kitu kingine
Kwa katiba yetu rais wa nchi kwa mamlaka aliyonayo anaweza kukuteu hata wewe Leo hii ukawa cdf anakuvalisha mavyeo biashara inaisha
 
Magufuli alimuongezea muda mwamunyange mwaka mmoja na kumteua mabeyo kuwa mnadhimu kumuandaa kuwa cdf
 
Wanawake wanaweza sana. Tuna Rais Mwanamke, Waziri wa Ulinzi Mwanamke, Waziri wa Utalii Mwanamke, Kamishna wa Uhamiaji Mwanamke!

Hizi ni nafasi nyeti katika kuisukuma nchi.

Ni wakati sasa wa kuwa na CDF Mwanamke baada ya Venance Mabeyo.
Kwanza naunga mkono hoja, the first female kufikia the highest ranking military officer ndani ya jeshi letu ni two star general, alikuwa ni Maj. Gen. Zawadi Madawili, ili mtu awe CDF, lazima kwanza apande vyeo kwenye logical progression hadi amefikia rank ya a 3 Star general, Lt. Gen, ndio awe CDF. Kwa sasa ndani ya Jeshi Letu, hakuna mwanamke yoyote ndani ya jeshi letu amewahi kufikia ngazi hiyo hivyo hakuna uwekano wowote wa Mabeyo kurithiwa na Mwanamke, tena na Kwa sasa sina hata uhakika if we have hata a 1 star general mwanamke!.
Huko nyuma niliwahi kutoa hoja hii Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu?. Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?
Hoja yangu hii kuhusu CDF still stands na huu sasa ndio wakati muafaka ikazingatiwa.

P
 
Back
Top Bottom